Animal Farm
JF-Expert Member
- Nov 16, 2024
- 234
- 281
Kule kkoo polisi mbona hawakuwa machachari kama kukabili chadema?Ccm ni majizi ya kura na Kodi za wananchi! Pumbavu sana!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kule kkoo polisi mbona hawakuwa machachari kama kukabili chadema?Ccm ni majizi ya kura na Kodi za wananchi! Pumbavu sana!
Chama cha Milele...Ni chama la mapumbavu!
Nendeni kwenu Kilimanjaro cc mbeyahatuwatakiWakuu,
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kuwa viongozi wake akiwemo Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe pamoja na Mwenyekiti wa Kanda ya Nyassa Joseph Mbilinyi (SUGU) pamoja na wanachama wengine wamekamatwa na Jeshi la polisi mkoani Songwe.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje John Mrema imeleza kuwa viongozi hao wamekamatwa leo Novemba 22 katika Pori la Halungu lililopo wilayani Mbozi.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa polisi walivamia msafara na kumkamata Mbowe pamoja na viongozi mbalimbali aliokuwa ameambatana nao. Viongozi waliokamatwa wengine ni pamoja na Pascal Haongo ambaye ni Mbunge wa Mbozi Mashariki mstaafu na Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo Wilaya ya Mbozi Ezekia Zambi.
Wengine waliokamatwa ni Appolinary Boniface Mkuu wa Digital platform, Paul Joseph na Calvin Ndabila ambao ni maafisa habari Kanda ya Nyassa, Mwanaharakati Mdude Nyagali pamoja na wasaidizi wa Mbowe ambao ni Bwire, Adamoo na Lingwenya.
Hata hivyo CHADEMA imelaani kitendo cha kukamatwa kwa viongozi hao huku ikitoa wito kwa jumuiya za kimataifa kushirikiana nao kwa kile walichokiita uvunjifu wa kidemokrasia.
Jambo TV imefanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Agustino Senga hata hivyo kupitia afisa habari wa Jeshi la polisi mkoani humo amesema kuwa watatoa taarifa rasmi baadae.