kaongea Point moja tu hapo, kubadilisha katiba. Mengine yote yote upupu mtupu na amechelewa sana. Kubadilisha katiba naunga mkono
Ukikubali kwamba kubadilisha katiba ni muhimu ili kuwe na mchakato wa uchaguzi ulio wa huru na haki, huna budi kukubali kwamba hili linatokana na ukweli kwamba sheria za uchaguzi, ambazo msingi wake ni katiba, nazo ni mbovu. Kwa maana nyingine, huwezi kukubali kwamba katiba ni mbovu, halafu akaja mtu kupinga kuanzia sheria za uchaguzi mpaka katiba, halafu wewe ukasema kupinga sheria dhalili za uchaguzi zinazotokana na katiba dhalili ni upupu. Utakuwa unajikanganya mwenyewe.
Nakubali kwamba msingi wa matatizo yote ni katiba, katiba inayompa rais mkono wa chuma sawa na Draco au Hammurabi na uhuru wa kisultani. Lakini hili halina maana kwamba mtu hawezi kuanza kuonyesha ubovu wa katiba kwa kuangalia sheria zinazotokana na katiba hiyo na kupanda juu mpaka kufikia kwenye katiba.
Kama mfalme yuko uchi, ashakum si matusi, mtu hashindwi kuanza kwa kusema kwanza hajavaa viatu, kisha hana hata soksi, tena suruali hana, he hata kaptula hana, na kutoka hapo kusema kumbe hata shati wala nguo za ndani hana.
Si lazima mtu aende moja kwa moja kwenye ubovu wa katiba, mwingine anaweza kutaka kufundisha ubovu wa katiba unaathiri vipi maisha ya kila siku, na hivyo kuona bora aanze kwa kuonyesha ubovu wa athari za katiba kwatika sheria zinazotumika kila siku.
Napenda wananchi wanapoeleweshwa kwa nini ni muhimu kubadilisha katiba kwa kupitia mambo yanayoathiri maisha kila siku kama hivi. La sivyo wengine wanaweza kuona mabadiliko ya katiba ni kama zoezi fulani la constitutional lawyers na madokta fulani hivi tu.
Kwa hiyo, tunapoongelea katiba dhalili, ni muhimu tuelewe kwamba katiba dhalili ni mzizi unaozaa matunda ya sheria dhalili, na mara nyingi kuwaonyesha watu mzizi si kitu rahisi kama kuwaonyesha watu matunda. Kwa hiyo yeyote anayeweza kuwaonyesha watu uhusiano wa matunda dhalili na mzizi dhalili anakuwa amefanya kazi nzuri na kamwe hatakiwi kuitwa amesema "upupu".
Labda kwa wale wenye pupa tu.