Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea kutoa wito kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kulifumua Jeshi la Polisi nchini kwa kile ilichodai kuwa limeshindwa kutimiza majukumu yake na kwamba interejensia yake imefeli kwa kiasi kikubwa
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya nje wa chama hicho John Mrema amezungumza hayo wakati akizungumza na wanahabari leo, Ijumaa Agosti 30.2024, mkutano uliolenga kukanusha taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi iliyotoka mapema leo ikidai kuwa viongozi wa chama hicho wamepanga njama za siri za kufanya matukio ya uvunjifu wa amani ikiwemo kuvamia kwenye vituo vya Polisi
Kuhusu uwepo wa madai ya watu kutekwa na kupotea, CHADEMA imeendelea kumshauri Rais Dkt. Samia kuingilia kati jambo hilo na kuunda tume maalum yenye hadhi ya kijaji ili ifanye uchunguzi wa mambo hayo kwa kuwa haikubaliki kuona Jeshi la Polisi linalotuhumiwa kuhusika kwa matukio hayo kwa namna moja au nyingine kuonekana likifanya uchunguzi
Katika hatua nyingine CHADEMA imetoa wito kwa Jeshi la Polisi nchini kuacha kuwachukulia viongozi wa chama hicho kama wahalifu, na kwamba Jeshi hilo linapaswa kutoka hadharani kufuta kauli hiyo