Usilete siasa kwenye masuala ya maafa na maisha ya watu. Ndio shida yenu ninyi Machadema kuleta siasa hadi kwenye vifo vya watu utafikiri mnaombeaga nakusubili maafa na majanga yatokee ili mpate hoja ,hasa baada ya kuwa na ukame wa hoja na kufirisika kisera kwa chama Chenu.
Nani kakwambia kuna mashindano ya kutoa salamu za pole na rambirambi mpaka useme mmekuwa wa kwanza?
Kwani sasa hujuwi kinachoendelea na kinachopiganiwa ni kuokoa maisha ya watu,kutafuta waliopotea na hawajulikani walipo,kutoa huduma za haraka kwa majeruhi,kuzuia na kuwaondoa walio katika maeneo hatarishi zaidi,kutoa misaada ya kibinadamu kwa ambao makazi yao yameharibiwa na kusombwa na maji?
Kazi hiyo imeanza kufanywa na CCM mkoa tangia zilipotoka taarifa ya janga hilo.hiyi ndio kazi inayoendelea kufanywa na CCM kwa kushirikiana na wananchi wa huko,tofauti na ninyi mnaipiga porojo huku mkiwa kwenye makochi yenu na kunywa mipombe yenu.
Acheni na msilete siasa kwenye maisha ya watanzania,ndio maana mnapuuzwa sana na watanzania.nani kawaambieni kuna riadha ya kuwahi kutoa taarifa za pole.kwa sasa riadha iliyopo ni kuokoa maisha ya watu na kuwasaidia wahanga.
Ndio maana Rais Wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama samia suluhu Hasssan yupo njiani kurejea nchini ili aende eneo la tukio na wakati huo huo tayari ameshatoa maagizo mazito yaliyowatetemesha watendaji wa serikali ili wafike haraka sana eneo la tukio.