Chadema yaunguruma Dodoma; Operesheni Sangara yapaa!

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2010
Posts
899
Reaction score
1,103
CHADEMA yaendeleza harakati za ukombozi wa raslimali za umma dodoma, wakazi wajitokeza kwa wingi kuunga mkono, wa muahidi MBOWE wapo tayari kwa lolote litakalo tokea kwa mabaya au kwa mema mpaka ukombozi upatikane wasema raudi hii chama cha chukua chako mapema hakina nafasi, waingiwa na imani kubwa na harkati za chadema ZIKIONGOZWA NA MBOWE, wazee wasema tupo nyuma yako mwenetu tusaidie kutupatia ukombozi wa kimaendeleo na siyo chuki fitna kama tunavyo fanyiwa kwasasa,
 
Kumpukeni Sheria ya kutumia "Mpunga" imesainiwa kwa "mbwembwe", Lakini bila "Mpunga" operesheni kama Sangara zitafanikiwa?
 
kaka tulia uone ukombozi unavyo fanywa kwa watu waliyo na dhamira ya kweli kumkomboa mtanzania kuna milima na mabonde lazima wanaharakati kama hawo wayapitie yote
 
MIKUTANO maarufu inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imeanza mkoani Dodoma kwa kumshughulikia Mbunge wa Mtera, John Samwel Malecela.
Mwenyekiti wa chama hicho, Freema Mbowe, alisema Malecela ambaye amekuwa akitumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kampeni mbalimbali, ndiye anaongoza mipango ya kuiba kura.
"Huyu sina naye ugomvi, lakini napenda kuwaambia kwamba yeye ndiye anayeandaa michoro ya wizi wa kura ndani ya CCM katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika nchini," alisema Mbowe.
Alisema kokote ambako CCM imekuwa ikishiriki uchaguzi, CCM imekuwa ikimtumia ili awasaidie kufanikisha malengo yao, jambo ambalo linamjengea sifa mbaya kiongozi huyo mkongwe.
"Sina ugomvi na Malecela, namheshimu sana mzee wangu, ila tatizo langu kwake ni wizi wa kura unaofanywa kila mahali anapopelekwa katika chaguzi," alisema.
Mbowe alitoa kauli hiyo kwenye viwanja vya Barafu wakati wa uzinduzi wa mikutano hiyo mjini hapa ambako mamia ya wananchi wa Dodoma walifurika.
Mbowe aliwasili katika viwanja hivyo majira ya saa 11 jioni jana, ambapo alitumia muda mwingi kuponda sera za CCM zinazoonekana kuwakandamiza wananchi na zimekuwa zikilea mafisadi.
Huku akishangiliwa na wananchi waliosikika wakisema: "Hakuna kushuka mpaka kieleweke," Mbowe aliwaambia wananchi kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo lipo Dodoma linalea mafisadi ambao wanapaswa kuchukuliwa hatua.
Kuhusu mfumo wa ugawaji wa viwanja katika mji wa Dodoma unaofanywa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), Mbowe alisema umelenga zaidi viongozi kuliko wananchi.

Source: Tanzania daima 18/03/2010
 
Mwenye picha jamani tunaomba mtuwekee tuone jinsi Mbowe alivyo vuna watu wengi kuja kumsikiliza.
 
MIKUTANO maarufu inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imeanza mkoani Dodoma kwa kumshughulikia Mbunge wa Mtera, John Samwel Malecela.
Mwenyekiti wa chama hicho, Freema Mbowe, alisema Malecela ambaye amekuwa akitumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kampeni mbalimbali, ndiye anaongoza mipango ya kuiba kura.
“Huyu sina naye ugomvi, lakini napenda kuwaambia kwamba yeye ndiye anayeandaa michoro ya wizi wa kura ndani ya CCM katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika nchini,” alisema Mbowe.
Alisema kokote ambako CCM imekuwa ikishiriki uchaguzi, CCM imekuwa ikimtumia ili awasaidie kufanikisha malengo yao, jambo ambalo linamjengea sifa mbaya kiongozi huyo mkongwe.
“Sina ugomvi na Malecela, namheshimu sana mzee wangu, ila tatizo langu kwake ni wizi wa kura unaofanywa kila mahali anapopelekwa katika chaguzi,” alisema.
Mbowe alitoa kauli hiyo kwenye viwanja vya Barafu wakati wa uzinduzi wa mikutano hiyo mjini hapa ambako mamia ya wananchi wa Dodoma walifurika.
Mbowe aliwasili katika viwanja hivyo majira ya saa 11 jioni jana, ambapo alitumia muda mwingi kuponda sera za CCM zinazoonekana kuwakandamiza wananchi na zimekuwa zikilea mafisadi.
Huku akishangiliwa na wananchi waliosikika wakisema: “Hakuna kushuka mpaka kieleweke,” Mbowe aliwaambia wananchi kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo lipo Dodoma linalea mafisadi ambao wanapaswa kuchukuliwa hatua.
Kuhusu mfumo wa ugawaji wa viwanja katika mji wa Dodoma unaofanywa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), Mbowe alisema umelenga zaidi viongozi kuliko wananchi.

Source: Tanzania daima 18/03/2010
HIVI ulitegema mwandishi wa gazeti la simba kuacha kuremba timu yake?
 
Ulitaka aandikeje kama kweli Simba ni bingwa au ulitaka usikie Yanga bingwa kwa vile wewe ni mpenzi wa Yanga tha is the reality
 
usiichukulie negative... point yangu ni kwamba habari hiyo ipo gazeti moja tu!!! ni ishara tosha kwamba uenezi kwa chadema unaanza kuchoka sio kama sangara ilivyoanza!!!
there are many ways to kill a man... i was delivering the message to CHADEMA kwamba uenezi wao umeishia zero grazing... na good analysists hawawezi weka mkazo kewnye gazeti la mbowe linaposifia mbowe

Time for change is passing by!!!
 
OK De Nono hili nalo ni gazeti la Mbowe

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ameuponda utaratibu unaotumika nchini katika kuwateuwa wakuu wa mikoa na wilaya kwa sababu hauzingatii maslahi ya wengi.
Akizungumza wakati akizindua operesheni Sangara katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma jana, Mbowe, alisema kuwa utaratibu huo haupi mamlaka wananchi kuchagua kiongozi ambaye anafaa.
“Mimi sina shida wala ugomvi na Dk. Nsekela (Mkuu wa Mkoa wa Dodoma), ugomvi wangu ni utaratibu unaotumika katika kuwapata viongozi hawa,” alisema.
Mbowe alisema utaratibu mzuri ambao unazingatia maslahi ya wengi ni wa kuwaacha wananchi kuwachagua viongozi hao kwa kutumia utaratibu wa kupiga kura.
Idadi kubwa ya watu walijitokeza katika mkutano huo kusikiliza, ingawa ulichelewa kuanza.
Mkutano huo ulianza saa 11:00 jioni na baada ya muda unaoruhusiwa kisheria kumalizika saa 12:00 wananchi walimsihi Mbowe aendelee kuhutubia, lakini aliwaambia kuwa alikuwa ameongozana na wabunge ambao ndio watungaji wa sheria, hivyo inamlazimu ausitishe hadi leo.
Leo chama hicho kitafanya mikutano katika Jimbo la Dodoma Mjini na kesho watakwenda Mtera, ambalo ni Jimbo la mwanasiasa mkongwe, John Malecela.
Aidha, watu wengi walijitokeza na kununua kadi za uanachama wa chama hicho.

CHANZO: NIPASHE
 
Mwenye picha jamani tunaomba mtuwekee tuone jinsi Mbowe alivyo vuna watu wengi kuja kumsikiliza.

Mwenye picha jamani, big up chadema

Operesheni Sangara Dodoma

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akisalimiana na baadhi ya wananchi wa mji wa Dodoma, mara baada ya kuhutubia mkutanowa uzinduzi wa Oporesheni Sanga mkoani Dodoma,uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu jana.
Mwenyekiti wa Chamacha Demokrasiana Maendeleo (CHADEMA), FreemanMbowe,akishirikiana na baadhi ya wabunge wa chama hicho,kuandikisha kadi kwawanachma wapya waliojiunga na chama hicho,mara baada ya mkutano wa uzinduzi wa Oporesheni Sangara mkoani Dodoma,uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu jana.
 
OK De Nono hili nalo ni gazeti la Mbowe

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ameuponda utaratibu unaotumika nchini katika kuwateuwa wakuu wa mikoa na wilaya kwa sababu hauzingatii maslahi ya wengi.
Akizungumza wakati akizindua operesheni Sangara katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma jana, Mbowe, alisema kuwa utaratibu huo haupi mamlaka wananchi kuchagua kiongozi ambaye anafaa.
“Mimi sina shida wala ugomvi na Dk. Nsekela (Mkuu wa Mkoa wa Dodoma), ugomvi wangu ni utaratibu unaotumika katika kuwapata viongozi hawa,” alisema.
Mbowe alisema utaratibu mzuri ambao unazingatia maslahi ya wengi ni wa kuwaacha wananchi kuwachagua viongozi hao kwa kutumia utaratibu wa kupiga kura.
Idadi kubwa ya watu walijitokeza katika mkutano huo kusikiliza, ingawa ulichelewa kuanza.
Mkutano huo ulianza saa 11:00 jioni na baada ya muda unaoruhusiwa kisheria kumalizika saa 12:00 wananchi walimsihi Mbowe aendelee kuhutubia, lakini aliwaambia kuwa alikuwa ameongozana na wabunge ambao ndio watungaji wa sheria, hivyo inamlazimu ausitishe hadi leo.
Leo chama hicho kitafanya mikutano katika Jimbo la Dodoma Mjini na kesho watakwenda Mtera, ambalo ni Jimbo la mwanasiasa mkongwe, John Malecela.
Aidha, watu wengi walijitokeza na kununua kadi za uanachama wa chama hicho.

CHANZO: NIPASHE

safi sana luteni... hapa tuko pamoja... na mimi nachukua hii habari ya NIPASHE aisee, nimependa kwamba ipo kwingine

Hapa mezani nina CITIZEN, GUARDIAN na DAILY NEWS... sioni kitu ya namna hiyo... meaning, kazi bado sana!! coverage ni muhimu mno kipindi hiki
 
Ni kweli De Novo hizo habari hazimo kwenye CITIZEN, GUARDIAN na DAILY NEWS ukiangalia ni wangapi huko vijijini hata mijini huwa wananunua magazeti achilia mbali magazeti hayo ya kiingereza
 
Operesheni Sangara Dodoma

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akisalimiana na baadhi ya wananchi wa mji wa Dodoma, mara baada ya kuhutubia mkutanowa uzinduzi wa Oporesheni Sanga mkoani Dodoma,uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu jana.
Mwenyekiti wa Chamacha Demokrasiana Maendeleo (CHADEMA), FreemanMbowe,akishirikiana na baadhi ya wabunge wa chama hicho,kuandikisha kadi kwawanachma wapya waliojiunga na chama hicho,mara baada ya mkutano wa uzinduzi wa Oporesheni Sangara mkoani Dodoma,uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu jana.

Asante sana fidel80
 
Hakuana cha CCJ wala nini, ni CHADEMA tu ndiye mkombozi
 
Ulitaka aandikeje kama kweli Simba ni bingwa au ulitaka usikie Yanga bingwa kwa vile wewe ni mpenzi wa Yanga tha is the reality
nikweli alitegemea tuandike uongo kama wanacyo fanya labda alitaka tuandike MBOWE akosa watu ndiyo angeridhika kwa ufinyu wa upewo wake wa kuona mbali tanzania ya sasa siyo ya kudanganywa kwenye ukweli ni ukweli uongo hauna nafasi, tuiunge chadema mkono kwenye harakati kama hizi jamani wameonyesha zamira ya kweli
 
Back
Top Bottom