SI KWELI PreGE2025 CHADEMA yazidiwa, yapanga kununua wanachama feki kwa elfu 10

SI KWELI PreGE2025 CHADEMA yazidiwa, yapanga kununua wanachama feki kwa elfu 10

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
photo_2025-06-05_17-37-25 (2).jpg
photo_2025-06-05_17-37-27 (2).jpg
photo_2025-06-05_17-37-25.jpg
photo_2025-06-05_17-37-24.jpg
photo_2025-06-05_17-37-27.jpg
 
Tunachokijua
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kinaendesha kampeni ya ajenda yake ya 'No reforms, No election iliyozinduliwa kanda ya Nyasa jijini Mbeya na sasa ikiwa imefikia kanda ya kati dhumuni likiwa ni kushinikiza kufanyika kwa mabadiliko na maboresho ya mifumo ya uchaguzi ikiwemo sheria za uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru na haki. Chama hicho kimekuwa kikisisitiza kuwa bila mabadiliko hayo hakutakuwa na uchaguzi.

Tarehe 03 Juni 2025, makamu Mwenyekiti wa Chama hicho bara John Heche aliongoza kikao cha Kamati Kuu makao Makuu ya Chama Mikocheni Dar es salaam ambapo ilikaa na kujadili taarifa aliyoitoa msajili wa vyama vya siasa kwa umma tarehe 27 Mei, 2025 akisitisha kutoa ruzuku kwa CHADEMA hadi pale watakapotekeleza maelekezo ya Ofisi ya Msajili kutokana na kutokuwa na Viongozi wanaoweza kusimamia mapato, matumizi na marejesho ya fedha hizo za Umma.


Taarifa inayosambazwa mtandaoni kuhusu CHADEMA

Ipo taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa viongozi wa CHADEMA wanapanga kununua wanachama kwa elfu 10 ili kuonesha chama hicho kinakubalika. Machapisho yenye taarifa hiyo yana utambulisho wa Mwnanchi, Jambo TV, Wasafi Media na Millard Ayo.

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search), umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli bali imetengenezwa na wapotoshaji.

Aidha machapisho yaliyotumika kusambaza taarifa hizo ni ya kughushi, kwani hayajachapishwa na vyombo hivyo (Mwnanchi, Jambo TV, Wasafi Media na Millard Ayo.

Vilevile machapisho hayo yamebainika kuwa na mapungufu kadhaa ambayo yanadhihirisha kuwa yametengenezwa na wapotoshaji kwani ni tofauti na machapisho rasmi ya vyombo hivyo ikiwemo matumizi ya fonti zisizostahili, makosa ya kisarufi.

Aidha chama hicho kinawahamasisha wanachama wake kukichangia kupitia kampeni yake ya 'tone tone' ili kukiwezesha kuendesha shughuli zake za kila siku.​
Back
Top Bottom