Ndugu Tayari ametoa changamoto kuwa elimu bure haiwezekani, akizingatia zaidi kuwa gharama za kufanya hivyo ni kubwa sana na wahisani (benki ya dunia na mashirika mengine ya missaada) hawatakubaliana na jambo hilo. Amejibiwa kuwa gharama ya kutoa elimu bure kwa hali ilivyo leo Tanzania inahitajika ongezeko la Shilling kama billion 100 tu. Argument yake ikahamia kwenye masharti ya watoa misaada na kuwa ni vibaya kutoa elimu ya bure kwani wasiostahili watapewa bure na kusababisha wale wanaostahili kushindwa kupata.
Napenda nianzie kwenye arguement ya watoa misaada; kwa kweli inasikikitisha na kutia kinyaa kwa mtanzania anayeonekana kuwa na maarifa kiasi hicho kutoa maelezo kuwa, tutashindwa kuongeza kwenye bajeti yetu kiasi cha shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kutoa elimu ya bure, kwa kuwa benki ya dunia watakataa. Nakubaliana kabisa kuwa hawa mabwana wana nguvu sana juu yetu. Hili la kusema eti watakataa matumizi zaidi ya shiling billioni 100 kwa ajiri ya kutoa elimu ya bure hadi kidato cha sita ni kuwasingizia. Mara nyingi udhaifu wetu tumekuwa tukiuhamishia kwa benki ya dunia. Benki ya dunia haiwezi kuingilia jambo ambalo tume-onesha kuwa tunaweza kulifanya, tena jambo la manufaa kama elimu ya bure eti tu kwa kuwa hawataki. Benki ya dunia watatuzuia kufanya hivyo ikiwa kwa kufanya hivyo tutalazimika kwenda kuomba zaidi hizo fedha.
Kuna mifano mingi sana ya matumizi makubwa ambayo benki ya dunia walilalamika na tuliendelelea na matumizi hayo lakini hawakusimamisha misaaada. Ununuzi wa ndege ya rais na ununuzi wa rada ni mfano mmoja wa matumizi makubwa ambayo tuliamua kuyafanya hata bila benki ya dunia kukubaliana na sisi. Kuna mifano mingine ya mikataba ya umeme wa IPTL. Benki ya dunia walikataa na wakashauri sana kuwa Tanzania kujiingiza IPTL ilikuwa kumeza ndoano, hata hivyo miradi hiyo iliendelea na matokeo yake wote tunajua. Kwa hiyo kujitetea eti Slaa atashindwa kuongeza bajeti ya elimu kwa shilingi billion 100 kwa sababu development partners watakataa ni uongo ulio wazi kabisa na kuzusha visingizio vya kusingizia pasipo na ukweli wowote. Tena benki ya dunia itashukuru iwapo serikali mpya itaonesha creativity kwa kupunguza aina nyingi za matumizi ambazo zinaendelea wakati benki ya dunia wanakuwa hawataki. Tusiwasingizie benki ya dunia na development partners kwa kushindwa kwetu eti watakataa, hilo nimethibitisha haliwezekani, pengine ndugu Tayari aje na argument nyingine.
Sasa nije kwenye hiki kigezo dhaifu kabisa ambacho nakiona ni kama ulimbukeni kinachotumiwa; eti kutoa elimu ya bure kutasababisha wale wasiostahili kuipata bure!! Kutoa elimu ya bure hadi kidato cha sita gharama zake si kubwa kama tunavyofikiria, nchi inao uwezo wa kufanya hivyo (tunakosa nia ya kufanya hivyo tu). Sasa ikiwa hilo tunaliweza, tutapata madhara gani, ikiwa watanzania wachache wenye uwezo (chukulia kama asilimia 5%) wataweza kulipiwa wakati wana-uwezo? Hii si inakuwa ni sawa na kuwapunguzia kodi wenye uwezo ili wawekeze zaidi na kuzalisha nafasi za ajira zaidi? Lakini ni kwa nini tuangamize mamilioni ya watanzania maskini (chukulia asilimia 40%) wasio na uwezo wa kulipia ada eti tu kwa kuwa tunaogopa tukifanya hivyo wale asilimia tano wasiostahili watanufaika?? Hao asilimia Tano wanaonufaika bila kustahili hawawezi kuwa kigezo cha kuwanyima haki watanzania maskini (40%) kusomeshwa bure. Hili wazo ni muflis na halitusaidii mbali ya kuwa linazidisha matatizo.
Ndugu Tayari, labda utusaidie hiyo partial education for all unayoizungumzia inafanyaje kazi? CCM wameshindwaje kuitumia hiyo mbinu? Mbona maelfu ya watanzania wanaoishi vijijini bado wana-drop out kwa kushindwa kulipia ada na gharama nyingine za elimu kama hiyo partial education for all inafanya kazi? Tusitafute visingizio vya world bank, wala watanzania walio na uwezo! Benki ya dunia haitaweza kuzuia jambo noble kama hilo kwa ongezeko kidogo la bajeti (hata ingekuwa bilioni 200), provided serikali mpya ioneshe nia dhabiti ya kupunguza matumizi makubwa yasiyo na tija ya serikali.
Serikali yetu inatoa marupurupu ya kupindukia, kwa maofisa wakubwa wa serikali kuliko serikali nyingi duniani. Kwa mfano, maofisa wengi wanapewa magari makubwa ya 4x4, wakijaziwa mafuta full tank (masaa 24), wakitumia less than 50% of their working time maofisini mwao (muda mwingine wako safarini), wakilipwa allowances katika dollar rates katika vikao vinavyofanyika maofisini mwao humo humo, n.k. Matumizi yote haya benki ya dunia hawayapendi, na hawawezi kutuambia tuache kufanya hivyo kwani siku wakituambia tuache tutasema wanatuletea ukoloni mambo leo. Tukiondoa matumizi ya namna hiyo, halafu tukaongeza bajeti kwenye elimu (naam hata bilioni 500), benki ya dunia wako nyuma yetu tena watatusaidia. Huo ndo ukweli halisi!