Nimemuona kamishna wa operation na mafunzo wa Polisi Bw.Chagonja akielezea kuhusu kukamatwa kwa Mbowe.Napenda nimkumbushe tukio dogo tu mabalo halijasahaulika nalo ni kushindwa kumkamata Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala licha hakimu kutoa amri ya kukamatwa.
Pia ameshindwa kujibu hoja ya kwa nini kibali kiliomwa ofisi ya bunge kabla ya kumhoji Mbunge wa CCM toka Shinyanga??
Unawapa wapinzani umaarufu ukiamini kuwa unakisaidia Chama tawala,Pole sana!!!!!

Hawa jamaa ni vipofu kuanzia mzee wa kaya mpaka mtendaji kata, hawawezi kuudanganya umma wa Tanzania kwamba ndivyo sheria zinavyofanya kazi hapa Nchini, au labda angesema kuna double standard tungemwelewa
watastaafu na kujiunga nasi kwenye kulima mchicha halfu tutwauliza waliyatumiaje madaraka yao?Mkuu!
Ndio hapo unapopima busara inayotoka midomoni mwao unashindwa kuelewa uwezo wao wa ufahamu wa mambo na kujitambua kwao kwamba wana nafasi gani katika nchi yetu. Wanaongea kana kwamba wananchi wote tupo katika kambi za polisi na wote hatuna haki ya kuhoji ukweli wa kauli zao.
Kwa kauli zao, naanza kuamini pasipo kua na shaka kwamba mauaji ya Tarime yalitekelezwa kwa kufuata ushauri wa viongozi kama hawa ambao wanajiamini wako sahihi muda wote kiasi kwamba hawathubutu kupima kauli zao zinapokelewa vipi na jamii.
Viongozi wa namna hii nawafananisha na Kamanda Zombe ambaye alijiona Mungu mtu enzi zake lakini kibao kilivyomgeukia na kuonja joto la jiwe, nae sasa analishutumu jeshi la polisi kwamba halitendi haki wakati akiwa kundini aliona kila kitu kiko sawa.
.
Anasema alitimiza maagizo ya mahakama, japo hasemi mamlaka ya kumwita Mbowe mhuni anayatoa wapi. Alitakiwa tu kutuambia kwamba aliagizwa kumkamata period. Inasikitisha sana kiongozi wa nafasi yake anashabikia mambo asyopaswa kufanya. VIONGOZI WA NAMNA HII NI JANGA LA KITAIFA:glasses-nerdy: