Chagua jambo moja tu la kuliondoa katika hii dunia

Chagua jambo moja tu la kuliondoa katika hii dunia

all about

Member
Joined
May 28, 2022
Posts
69
Reaction score
103
Mimi nitaondoa "UJINGA"

Kwasababu...

Nilikuwa nikifikiria jibu la hili swali, ghafra akili yangu ilikumbana na haya mambo manne.

Umasikini, vita, njaa, na kifo.

Na nilikuwa nikifikiria kuondoa mojawapo ya hayo.

Nilitambua kuwa dunia haitawahi kweli kuwa huru kutokana na matatizo hayo manne ikiwa tutaendelea kuwa wajinga.

Fikiria
Binadamu wameyashinda magonjwa kwa tiba, lakini wapo baadhi ambao wanaendelea kuwa na wasiwasi na kuogopa kuwa tiba hizo zitakuwa hatari kwao. Wanaishia kufa.

Ujinga
Binadamu wameishinda njaa kwa kubadilisha vinasaba (DNA) za mimea, na kuifanya iwe bora na yenye afya zaidi kwa kila mtu. lakini angalia kila kukicha watu wataendelea kuteseka na kufa kwa njaa.

Ujinga
Binadamu wamezishinda vita kupitia diplomasia na uvumilivu, lakini utashangaa wanaanza kuwashambulia wale ambao hawapo upandea wao au si wa kundi lao. Vurugu zitaanza upya, na wengi wataendelea kufa tu.

HITIMISHO,
ningependa kuondoa "UJINGA" .
 
Back
Top Bottom