''Chagua moja, JF au mimi''

''Chagua moja, JF au mimi''

...shemeji anakutakia mema huyo,
punguza hiyo addiction kaka!...
ingekuwa ni yeye, ungemuelewa?
 
fanya kila jambo kwa wakati kuna wakati wa bibie kupata ma burudani na kunawakati wa Jf.
 
Mi wangu yupo humu humu. Nilishamshtukia. Ila hatujuani.
 
Mhh mwenzetu inategemea unakuwa ktk topic gani within JF !! Isijekuwa ile ya nanino sasa either anaona kila ukiwa pale suruali inatuna au ktk picha anaona kuna kila dalili za kuikuta yake soon na uka- m-Isangura au kum-Matumla 🙂 🙂 🙂 Dunia ina vituko hii na usicheze na binadamu.... lol

Ni kauli ya mpenzi wangu toka juzi hatuna story anasubiri jibu, nichague kuwa na yeye au jamii forums.....nakiri kuwa toka nimejiunga na JF ni mimi na simu,..simu na mimi, nikiamka jf, nikienda toilet jf, nikiwa na kazi zangu pia jf nipo nayo, nikilala jf pembeni, yaani sitaki kupitwa na kitu humu jf...sasa bibie kaseemaa wee mwishowe kachoka na kasusa kushiriki chochote na mimi mpaka nimpe jibu eti either nibaki na yeye au niendelee na jf....nifanyeje wanajamvi? Kiukweli nampenda sana lakini at this point kuiacha jamii forums ni ngumu pia...
 
Me hii kitu huwa sijamwambia kabisa wife, coz nlikuwaga facebook nikajifuta coz ilitaka kuvunja ndoa kabisa nikaona mambo ya kijinga nikaaga marafiki nikafuta na ss ni mwaka na nimeshazoea tu, Uzuri wa humu jamii ni hakuna mapicha picha si unajua tena mambo ya photoshop zinavyowapendezesha watu.
Kwahiyo ni bora tu uwe na mda maaumu wa kuona hivyo vitu kwani unaweza jikuta umevunja ndoa kimchezo tu.
 
usiombe na yeye akajiunga,kibao kitakugeukia!!
 
kam tatizo ushalijua nina imani halito kusumbua mpe muda wake na jf ipe muda wake haiwezekani uwe hivyo naye akae kimya ebu jiulize wewe ungependa kama naye angekuwa busy na simu kama wewe
 
Back
Top Bottom