Chagua sababu yako Kuu Kati ya hizi zifuatazo ya kwanini TFF imeisogeza Kariakoo Derby hadi tarehe 3 July, 2021?

Chagua sababu yako Kuu Kati ya hizi zifuatazo ya kwanini TFF imeisogeza Kariakoo Derby hadi tarehe 3 July, 2021?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
a) Kuipa Yanga SC muda mrefu wa Kujiandaa kwakuwa Kocha wao bado ni Mgeni na wasije Wakafungwa Kikatili na Simba SC.

b) Kuihujumu Simba SC hasa Kimapato kutokana na kwamba Kimahesabu hadi tarehe mpya iliyopangwa Simba SC atakuwa ameshatangazwa Bingwa hivyo hata idadi ya Mashabiki itapungua kwakuwa Mechi itakuwa imeshakosa Mvuto wake.

c) Ratiba za Michuano ya CAF na FIFA bila kusahau na ile ya ASFC Kuingiliana hivyo kupelekea tarehe pekee iliyobakia ni hiyo ya 3 July, 2021.

d) Shinikizo kutoka kwa Warushaji Azam Tv au Shinikizo kutoka Serikalini (hasa Ikulu) kuwa hueanda Siku hiyo Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan nae angependa kuwa Mhudhuriaji na Mtazamaji ili atume Ujumbe kwa Wanamichezo kuwa nae ni Mwanamichezo mzuri na mkubwa tu.

Kuna mahala ( hasa katika Kanuni ) za Mechi zilizohairishwa tena hizi za Derby (kama za Simba na Yanga) na kuona kuwa kumbe hata ikitokea zimeota mbawa kwa sababu zozote zile inatakiwa ichezwe ama ndani ya Wiki Moja na ikichelewa sana basi iwe ni Wiki Mbili tu na siyo kama ilivyopangwa sasa baada ya Will Sita au Saba.

Mpira wa Tanzania una Vioja 24/7 tu.
 
Back
Top Bottom