Chaguzi mbili kuu pale unapogundua mkeo anakusaliti

Chaguzi mbili kuu pale unapogundua mkeo anakusaliti

1. ACHANA NAYE na ulee watoto wako uliowapata ukiwa na mkeo. Unaweza kuamua kuoa mwanamke mwingine ama kubaki mseja daima.

Kumbuka ukiamua kuoa tena hutapata malaika mwingine bali utapata mke mwenye moyo kama wa yule utakayemuacha.

2. MSAMEHE mkeo kisha tafuta mtaalam wa kukusaidia kushughulika kuponya maumivu yako.

Weka mkakati wa namna bora ya kukusaidia usiingie katika mahusiano mapya.

Leeni watoto wenu pamoja hata kama mu wanandoa mliochana.

Vile utakavyo amua ni chaguo, huyo mwanamke ni mkeo ulimpenda ukamuoa, ni chaguo lako.

Kwa upande wangu binafsi ningechagua njia ya MSAMAHA kwa sababu mimi ni zao la msamaha. Yesu mwenyewe alisisitiza MSAMAHA 7×70 na wala hakusisitiza talaka, hivyo mie ninaishi ndani ya msamaha.

Pamoja na kumsamehe lakini ikitokea akaendeleza - maisha ya uzinzi - udanganyifu wa kudumu - hapo nitamwangusha kama kizazi cha moto. Lakini sitavunja ndoa yangu kwa sababu ya wingu linalopita.

Tafadhali usiue wala usijiue kwa sababu ya mkeo kukucheat bali chagua hatua mojawapo kati ya hizo mbili nilizozitaja.

Ubarikiwe.
Hyo option ya pili ulochukua HAIJAWAHI kumwacha mtu salama kiriho wala kimwil had kifo.....hasa kwa ss wanaume..........na huyo ni option ya Simps zao la Oneitis...................solution ni African polygamous culture
 
Lengo la talaka ni kuharibu saikolojia ya watoto,Shetani uleta talaka kwa wanandoa baada ya kuchungulia kesho Bora ya watoto wako wataenda haribu ufalme wake.
Uwahi mapema kwa talaka wazazi ili awawini watoto.
 
Ingefaa vyema watu waishi pamoja kwa faida ya watoto japo tunakosewa sana au wenza kuwa na tabia ngumu sababu ya tofaut ya malezi na kukosa elimu ya mahusiano na kuchagua mwenza Bora
 
Back
Top Bottom