Chaguzi za Kanda CHADEMA na jinsi zilivyo muhimu kitaifa

Chaguzi za Kanda CHADEMA na jinsi zilivyo muhimu kitaifa

Sikupata kujua kama Chadema ni maarufu na muhimu kiasi hiki kuanzia ngazi ya chini hadi pale Chaguzi za viongozi wa kanda zilipoanza.

Ni ajabu kuwa chaguzi hizo zimefuatiliwa kwa ukaribu sana na nchi nzima, hasa ccm imeonyesha kuwa inaangalia kwa ukaribu sana kuliko hata Chadema wenyewe.

Nina hakika kwa sasa viongozi wakuu wa CCM wakiongozwa na mwenyekiti wao Rais Magufuli wanajua kila kanda mwenyekiti na makamu ni nani na hata idadi ya kura walizopata. Pia watu wao walio wachomeka wameangukaje.

Hii ni ishara kuwa Chadema ni chama kikubwa na tishio kwa watawala na wanauwezo wa kuwatoa madarakani CCM kama uchaguzi wa haki na huru.

Kula tano, tena hapo pa kupita bila kupingwa ndio wamefunika kila kitu. Ifahamike hiyo kupita bila kupingwa ni mbinu kubwa ya jiwe toka akiwa mbunge, na sasa ndio mbinu inayowapa ccm ushindi wa 90% kwenye chaguzi zote. Kwa maneno marahisi hiyo kupigia kura mtu hata akibaki mwenyewe imewauma sana ccm, na ni kama imekuja kudharaulisha mbinu kuu ya ushindi ya ccm.
 
ufisadi uliopo chadema unatisha, mbowe na wenzie wachache wanakula mamilioni ya ruzuku peke yao.
 
Unamdhalilisha msajiri wa vyama aliye teuliwa na Rais.kumbe aliteuliwa kwaajili ya kusajiri viccoba
Ina maana ndani ya miaka 30 katika wanachama wote wa chadema hakuna mwanachama tofauti hata mmoja wa kufanya kazi ya mbowe? Kama hamna utaratibu wa kupokezana madaraka madogo ndani ya chama, mtakua nao mkishika madaraka makubwa ya nchi?

Yaani ninyi kwenye democracy hamna la kuwashauri watanzania kabisa sababu democracy kwenu haipo
 
Kwahiyo wanachama wenu ni wasomi tu
Ona unavyo zidi kujishusha. Kuna tofauti ya usomi na uelewa.
Usomi waweza kuwa wa kupata vyeti hadi vya juu kabisa lakini ukakosa uelewa hadi kudhani Kuwaiti imepakana na Zimbabwe.
Uelewa ni broad knowledge ambayo mwenye usomi na asiye na huo usomi waweza kuwa nayo.
Hiyo ipo sana Chadema
 
Ina maana ndani ya miaka 30 katika wanachama wote wa chadema hakuna mwanachama tofauti hata mmoja wa kufanya kazi ya mbowe? Kama hamna utaratibu wa kupokezana madaraka madogo ndani ya chama, mtakua nao mkishika madaraka makubwa ya nchi?

Yaani ninyi kwenye democracy hamna la kuwashauri watanzania kabisa sababu democracy kwenu haipo
Hivi huko shule mnaenda kusomea nini? (By FaizaFoxy)
Jambo hili mnafafanuliwa lakini mbona hamuelewi? Au na nyie mmekuwa Jiwe kama mzee wenu?
 
Back
Top Bottom