CHAI Day 5 Feb 2011 Dar: Kujadili fursa katika Kilimo na ufugaji

CHAI Day 5 Feb 2011 Dar: Kujadili fursa katika Kilimo na ufugaji

kanyagio

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2009
Posts
1,021
Reaction score
366
MKUTANO WA KUJADILI FURSA KATIKA KILIMO TAREHE 5 FEBRUARI 2011 SAA 8 KAMILI MCHANA LUNCH TIME HOTEL

wakuu wa JF, heshima zenu!! nachukua nafasi hii kuwafahamisha kuwa baada ya kujadili kwa kina masuala ya kilimo na ufugaji kupitia hapa JF (hasa kupitia thread yaTujiunge na kuanzisha JAMII FARM na nyinginezo tumeona ni vema tufanye mkutano maalum kujadili masuala ya uwekezaji katika kilimo na ufugaji. Madhumuni ya mkutano huu ni kubadilishana taarifa na uzoefu katika uwekezaji katika sekta ya kilimo na ufugaji. aidha itakuwa ni kikao muafaka katika kupeana taarifa mbalimbali za fursa katika kilimo na ufugaji. Huu utakuwa ni mwendelezo wa mkutano tuliofanya mwaka jana.

mkutano huu tarehe 5 Februari 2011 jijini Dar es salaam pale LUNCH TIME HOTEL kuanzia saa 8.00 kamili mchana. Gharama ya kushiriki ni 15,000/= kwa kila mtu (ukumbi na refreshments). hotel ya Lunchtime (LUNCH TIME HOTEL) ipo along Mandela Road opposite na kituo cha Mabibo Hosteli na si mbali kutoka Ubungo EXTERNAL)

mpaka sasa waliothibitisha kushiriki ni wafuatao:


  1. KANYAGIO ----- mchango tayari
  2. MALILA ----- mchango tayari
  3. TITO ----- huyu kalipa advance ya ukumbi (so keshalipa)
  4. MGOMBEZI ---- keshatuma kwa MPESA (15,500)
  5. MGOMBEZI FRIEND ---- keshatuma kwa MPESA (15,500)
  6. ELNINO- kasema katuma ila sijazipokea, naomba afuatilie tafadhali
  7. Mouna Lyaruu (KASOPA FRIEND NO. 1)
  8. Raiya Rashid (KASOPA FRIEND NO. 2)
  9. ZAHOR SALIM --- keshatuma kwa MPESA (16,000)
  10. NEW MZALENDO -- kasema katuma ila sijazipokea, naomba afuatilie tafadhali
  11. TGS D
  12. REALTOR
  13. MASAKI
  14. STREET SMART
  15. LEN
  16. BABALAO
  17. THE INVESTOR--- keshatuma kwa MPESA (15,000)
  18. MASIKINI JEURI
  19. SABI SANDA
  20. DORISVETY
  21. CARMEL
  22. RAMTHODS
  23. BENNET (wa mitiki blog)
  24. GAMAHA
  25. AMBASSADOR
  26. KIBANANHUKHU
  27. TZ_Investor
  28. REALTOR FRIEND
  29. Maxence Mello
  30. JOKA KUU (nimekuweka ingawa kwenye post yako hujaonyesha kama unashiriki)
  31. MKESHAHOI
  32. ELNINO FRIEND
  33. JF MARKETER
  34. KAGEMULO
Mshiriki ambaye hatakuwepo ila ametoa 10,500 ni Maamuma


naomba kuwafahamisha kwamba mchango kwa ajili ya gharama za mkutano zimeanza kupokelewa. kwa hiyo naomba mtumie MPESA kuweka 15,000 tulizokubaliana.. namba ni 0759 44 45 46. ukitaka kunipigia ku-confirm naomba utaje jina lako kama lilivyo hapo juu niweze kujua.nitakuwa natoa update kila siku kuhusu hali ya michango kwa uwazi!!.


Ratiba imeambatanishwa

ukiwa na swali usisiste kuuliza

"PAMOJA TUNAWEZA"
 
Kwa uwezo wa mola mimi naahidi nitakuwepo siku hiyo ya 5february jioni kwa ajili ya mkutano huo.

Naomba nichangie baadhi ya maada tutakazo jadiliana nazo.

1. Je kilimo,ni shughuli ambayo mwajiriwa anaweza kuifanya bila kuathiri ajira yake?
2. Je eneo lipi la kilimo linaweza kuwa na tija siku za usoni?
3. Matatizo makubwa ktk kukusanya mtaji wetu ni yapi?

nk
 
Asante Mkuu Kanyagio!

Itakuwa ni jambo jema kuwa na mwendelezo wa CHAI DAY, Nami naahidi kuhudhuria mkutano huu. Kutokana na umuhimu wa siku hii napendekeza tuwe na muda wa kutosha ili mada zitakazowakilishwa na kujadiliwa kupata wasaa wa kutosha, tukiweza kukutana kwa siku nzima (asubuhi mpaka jioni, lunch inclusive).

Tukiweza kuwapata wataalamu katika sekta husika itakuwa vyema, eneo mojawapo ambalo nafikiri linaweza kuangaliwa ni juu ya sheria za umiliki wa ardhi na upatikanaji wake. Sina hakika kama lilishawahi kujadiliwa hapa jamvini au la!

Napendekeza KANYAGIO na MALILA kufanya maandalizi na kutupatia taarifa.
 
Mkuu namuomba mungu anipe uhai na afia njema na nawaombeeni ninyi pia ili muweze kufanikisha azimio hili napia nawashuruni kwa kunipa nafasi ya kushiriki kikaoni ntahuzuria kwa hali na mali mkuu Kanyagio muheshimiwa Malila naimani INAWEZEKANA
 
ahsante Malila, Mgombezi na Kasopa kwa maoni yenu. Ngoja tusubiri maoni zaidi. KIKUBWA ZAIDI NI CONFIRMATION YA WAJUMBE.
mida hii nimetoka kupiga simu RomboView Hotel na kuongea na Meneja wao ambaye kasema kuwa ukumbi unagharimu Tsh 200,000/= ila kama itakuwa ni siku ya mgao wa umeme bei inaongezeka kuwa 300,000/=. kanipa link ya website yao http://www.rombogreenviewhotel.com/conference_halls.php . Aidha, jitihada zinafanyika kufuatilia ukumbi wa LUNCH TIME HOTEL ambao Malila et al wana uzoefu so tutapata details zaidi. Ni vema kuwa na alternative nyingi halafu tunachagua ipi ni good deal na convenient kwa watu wengi
 
Zahoro Salim, ahsante kuthibitisha kushiriki. keep reading this post ili kupata update za mkutano..
waiting to hear from others.. SAA YA VITENDO NI SASA SI KESHO
 
nimeangalia hii hoteli http://www.rombogreenviewhotel.com/conference_halls.php
Imekaa vizuri sana,je Tunatarajia watu wangapi?kunabaadhi ya hoteli huwa wanaruhusu mkusanyiko wa watu chini ya 15,hapo hamtalipia ukumbi mtalipia vinywaji vyenu tu. confirmation za watu itatupa picha ya watu tutakaofika.
Itapendeza tukialika wataalama wa Ufugaji samaki na Nyuki.
 
Mkuu mzalendo mimi naungana na Mkuu Mlilo kwa kikaohiki sidhani kama kuna umuhim wa kualika watutoka nje ya jamii kwakuwa hiki nikikao cha mikakati hawa jamaa hatuwahitajii kwasasa tujipange tukishakuwa namuelekeo ndotunaweza kuwaalika napo lada baada ya vikao viwili mpaka vitatu vijavyo ni maoni tu wakuu kama kunaulazima sio mbay

nimeangalia hii hoteli http://www.rombogreenviewhotel.com/conference_halls.php
Imekaa vizuri sana,je Tunatarajia watu wangapi?kunabaadhi ya hoteli huwa wanaruhusu mkusanyiko wa watu chini ya 15,hapo hamtalipia ukumbi mtalipia vinywaji vyenu tu. confirmation za watu itatupa picha ya watu tutakaofika.
Itapendeza tukialika wataalama wa Ufugaji samaki na Nyuki.
 
Mkuu mzalendo mimi naungana na Mkuu Mlilo kwa kikaohiki sidhani kama kuna umuhim wa kualika watutoka nje ya jamii kwakuwa hiki nikikao cha mikakati hawa jamaa hatuwahitajii kwasasa tujipange tukishakuwa namuelekeo ndotunaweza kuwaalika napo lada baada ya vikao viwili mpaka vitatu vijavyo ni maoni tu wakuu kama kunaulazima sio mbay

Nami naungana nawe Mkuu KASOPA kwamba kikao hiki kiwe na agenda za kutupa DIRA, baada ya hapo tutafahamu mahitaji yetu na kuwatafuta wataalamu katika vikao vijavyo. Kwa kuwa huu utakuwa mwendelezo wa CHAI DAY iliyofanyika mwaka jana na wengi wetu tutakuwa tunashiriki kwa mara ya kwanza, itakuwa vyema kama Mkuu MALILA ataweza kutujuza yaliyojiri mwaka jana na utekelezaji wake.
 
Nami naungana nawe Mkuu KASOPA kwamba kikao hiki kiwe na agenda za kutupa DIRA, baada ya hapo tutafahamu mahitaji yetu na kuwatafuta wataalamu katika vikao vijavyo. Kwa kuwa huu utakuwa mwendelezo wa CHAI DAY iliyofanyika mwaka jana na wengi wetu tutakuwa tunashiriki kwa mara ya kwanza, itakuwa vyema kama Mkuu MALILA ataweza kutujuza yaliyojiri mwaka jana na utekelezaji wake.

Moja ya matokeo ya chai day ya mwaka jana ni mimi kukutana na kanyagio uso kwa uso, na kutekeleza yote tuliyojipangia ktk kikao kile. Tumetekeleza kwa kiwango kikubwa na pressure imekuwa kubwa,hasa members kuongezeka, jamani mambo yote yanawezekana chini ya jua. Tukionana tutajadiliana vizuri.
 
wakuu wa JF, heshima zenu!! nachukua nafasi hii kuwafahamisha kuwa baada ya kujadili kwa kina masuala ya kilimo na ufugaji kupitia hapa JF (hasa kupitia thread yaTujiunge na kuanzisha JAMII FARM na baada ya kujadiliana na baadhi ya members kwa kupitia PM tumeona ni vema tufanye mkutano maalum kujadili masuala ya uwekezaji katika kilimo na ufugaji. Madhumuni ya mkutano huu ni kubadilishana taarifa na uzoefu katika uwekezaji katika sekta ya kilimo na ufugaji. aidha itakuwa ni kikao muafaka katika kupeana taarifa mbalimbali za fursa katika kilimo na ufugaji. Huu utakuwa ni mwendelezo wa mkutano tuliofanya mwaka jana.

Kwa msingi inapendekezwa kwamba mkutano huu ufanyike tarehe 5 Februari 2011 jijini Dar es salaam.

majukumu yaliyo mbele yetu ili kufanikisha mkutano huu ni kama ifuatavyo:


  1. tutengeneze kamati ndogo itakayokuwa na jukumu la kufanya maandalizi
  2. kutafuta ukumbi kwa ajili ya kufanyia mkutano huu (pendekezo la kwanza ni Lunch time hotel iliyopo along Mandela Road karibu na External na Kituo cha Hostel). aidha tutaulizia sehemu nyingine pia
  3. Kupata idadi kamili ya washiriki - uzoefu ni kuwa kuna watu wanasema watahudhuria halafu hawaji na hivyo kupelekea waandaaji kutoa hela zao mifukoni kugharamia ukumbi (kuziba mashimo).
  4. kutayarisha ajenda za mkutano na kutafuta watoa mada (kikubwa ni kubadilishana taarifa na uzoefu na kufahamu fursa zilizopo katika kilimo na ufugaji).



baadhi ya members ambao nafahamu wanajihusisha na kilimo na ufugaji (baadhi siwajui kwa sura ila kupitia posts zao) ni vema wakahudhuria ikiwa ni pamoja na Malila, ELNIN0, Mgombezi, newmzalendo, African, cheusimangala, kasopa, Njowepo, Majimoto, MAAMUNA, Masikini_Jeuri, len, MpendaTz, Realtor, Mutensa hawa ni baadhi ya wale niliona post zao na some wameshaonyesha vitendo - lakini samahani kwa ambao sijawataja maana mpo wengi na siwezi kuwamaliza.

Kuanzia leo mpaka tarehe 29 Januari tutakuwa tunachukua confirmation za watu (kufikia tarehe 24 au 25 tutakuwa tumeshajua ukumbi ni kiasi gani na gharama zake).

Tunaanza kukaribisha confirmation pamoja na maoni kuhusu agenda, time za kuanza mkutano na nini kifanyike ili kuwa na mkutano wenye mafanikio.

nawasilisha!

Mkuu Kanyagio, confirmation tunafanyia hapa hapa jukwaani au kuna utaratibi mwingine wa kuconfirm. Kama ni hapa jukwaani count me in.
Pia naunga mkono venue iliyopendekezwa.
 
nazidi kuwashukuru wote ambao wameonyesha nia ya kushiriki. kuhusu ukumbi kwa kweli itategemea na idadi ya watu. saa ya kuanza mimi nategemea mapendekezo yenu - Mkutano wetu utachukua kati ya masaa 2-3 kutegemeana na ajenda!!
 
Kwa kweli ni wazo zuri sana ila sisi tulio nje ya Tanzania tunakosa nafasi ya kushiriki na kujuana uso kwa uso na ndugu zetu. Nami nijumlishe kwa maongezi na mengineyo
 
Mkuu Kanyagio nashukuru kwa hii taarifa, mimi pia nitaudhuria. Mchango kidogo kwenye agenda, baada ya kufahamiana:

  1. Kujadili muundo wa kuanzisha hii farm; Company limited, company imited by guarantee and having no share capital? Saccos? NGO?... Mamuzi ya muundo utatokana baada ya kujadili lengo kuu la kuanzisha farm, dira yetu na malengo kwa ujumla.
  2. Kuchagua uongozi
  3. Mpango kazi
Pamoja...
 
Nitapenda kuhudhuria. Kila siku huwa naamini kabisa ardhi ndio kila kitu na kilimo cha kisasa kinaweza kabisa kubadilisha maisha yetu ya kiuchumi!
Naomba mwaandaji anaitumie namba yake ya simu kwenye PM ili tuwasiliane!
 
wazo la kuregister Jamii Farm ni la msingi.Nashauri washiriki tuanze kufikiria muundo wa kuendesha huo mradi.and how to Institutionalize our Ideas for the next 3 generations 🙂
 
Moja ya matokeo ya chai day ya mwaka jana ni mimi kukutana na kanyagio uso kwa uso, na kutekeleza yote tuliyojipangia ktk kikao kile. Tumetekeleza kwa kiwango kikubwa na pressure imekuwa kubwa,hasa members kuongezeka, jamani mambo yote yanawezekana chini ya jua. Tukionana tutajadiliana vizuri.

Malila hii nilikuwa sijaisoma!! imenifurahisha sana!!. inabidi unaanza!!
 
Back
Top Bottom