Ile kampuni iliuzwa, alinunua Tatepa na kuiondoa sokoni kimkakati! Ni kama Kilimanjaro alivyonunua Maji Afrika ya Iringa na kuyaondoa sokoni, kuacha uzalishaji. Hii inaitwa "Strategic Acquisition", unamnunua emerging competitor na kuondoa/kubadili jina la bidhaa sokoni ili ibaki bidhaa moja. Tatepa ambao ndio wenye brand/bidhaa ya Chai Bora, walinunua Chai Jaba.
Chai Jaba, na yeye alikuwa anachukua Chai, Mbeya, Iringa kama Chai Bora.
Nje ya mada: Majani ya chai ni biashara ya nzuri yenye faida kubwa, kuna soko kubwa sana nje la black tea. Pia majani haya ya jero jero tunatumia ni majani grade ya mwisho, grade nzuri huuzwa nje na bei kubwa.