Chai Jaba walijitangaza wakasikika. Ilikuwaje wakashindwa sokoni?

Tangazo chai ya maziwa alafu uhalisia chai ya rangi tulienda test tunaona mbona chai nyeusi tukarudi zetu chai bora haikuwa na upinzani πŸ˜‚πŸ˜‚

lakini pia chai jaba kampuni hasili yake ni kenya kwaiyo walishindwa fanya biashara ya ushindani tz ila kenya wanafanya poa walijaribu kuvuka mipaka
 
Inawezekana bidhaa yao haikuweza kukonga mioyo ya wapenda chai.
 
Ile kampuni iliuzwa, alinunua Tatepa na kuiondoa sokoni kimkakati! Ni kama Kilimanjaro alivyonunua Maji Afrika ya Iringa na kuyaondoa sokoni, kuacha uzalishaji. Hii inaitwa "Strategic Acquisition", unamnunua emerging competitor na kuondoa/kubadili jina la bidhaa sokoni ili ibaki bidhaa moja. Tatepa ambao ndio wenye brand/bidhaa ya Chai Bora, walinunua Chai Jaba.
Chai Jaba, na yeye alikuwa anachukua Chai, Mbeya, Iringa kama Chai Bora.

Nje ya mada: Majani ya chai ni biashara ya nzuri yenye faida kubwa, kuna soko kubwa sana nje la black tea. Pia majani haya ya jero jero tunatumia ni majani grade ya mwisho, grade nzuri huuzwa nje na bei kubwa.
 
Nakumbuka walipita na helicopter wameichora picha ya chai jaba wanazunguka nayo kuitangaza.

Kitambo sana hiyo.
 
Kwani Juisi ya Yeboyebo ilipotelea wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…