Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya, Aprili 08, 2025, Katibu Mkuu wa CHAKAMWATA, Mwalimu Meshack Kapange amesema Halmashauri mbalimbali nchini Tanzania zinadaiwa na Walimu lakini hadi sasa hakuna malipo yoyote yaliyotolewa ambapo chama cha walimu Tanzania CWT kwa kushirikiana na Halmashauri mbalimbali nchini isipokuwa mkoa wa Singida pekee, zinadaiwa mabillion ya fedha.
Kutokana na madai hayo amesema chama cha kutetea haki na maslahi ya Walimu Tanzania kimepanga kuchukua hatua za kwenda mahakamani kufungua kesi ikizingatiwa katika mikoa yote Tanzania ni mkoa wa Singida pekee yake ambao hauna shida na Chama cha kutetea haki na maslahi ya walimu CHAKAMWATA.
Pia, ameeleza kwa zaidi ya miaka 30 Walimu wamekuwa wakilazimishwa kujiunga na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na kwamba walimu hao wamekuwa wakikumbana na maonezi mbalimbali ikiwemo kuingiziwa makato ya CWT bila ridhaa ya walimu.
"Kuingiza makato kwenye mshahara wa mfanyakazi kinyume Cha ridhaa yake ni kosa la jinai. Sheria ya ajira na mahusiano kazini kifungu cha 28 kinakataza mwajiri kuingiza makato kwenye mshahara wa mfanyakazi bila mfanyakazi kuridhia labda hayo makato yawe ya lazima kama vile makato ya kodi ya Serikali lakini mengine ni lazima mfanyakazi aridhie," amesema katibu mkuu huyo na kuongeza.
"Kutokana na hayo yote, tumeorodhesha mikoa yotena wilaya zote, tuna Halmashauri 125 nchi nzima katika, ni mkoa wa Singida peke yake ndio hauna nongwa na CHAKAMWATA na tumeorodhesha pesa ya mwalimu aliyokata katika wanachama kumi na mbili elfu mia mbili thelathini na moja asilimia moja ya CWT na asilimia moja ya CHAKAMWATA tunakwenda mahakamani kufungua kesi na kabla ya kufungua kesi tumeshawapekea waajiri wote nchi nzima barua ya notice (kusudio la kuwashtaki) na wanatakiwa kutujibu ndani ya siku 30 na tunawadai jumla ya shilingi bilioni 12 million 326 laki tisa na sitini elfu na 571 na senti tisini.
Hizi fedha wanatakiwa kulipa CWT na wanatakiwa kushirikiana na hao waajiri kwasababu anayeingia kwenye mishahara ni mwajiri halafu anampelekea CWT (Chama cha walimu). Kwanini Serikali kuu itoe maelekezo lakini TAMISEMI ikiuke maelekezo, Halmashauri zikiuke maelekezo ndio maana nchi haiendelei kwasababu kuna kutokuwepo kwa nidhamu kwenye mifumo yetu ya utawala na mifumo yetu ya uongozi", ameeleza katibu mkuu wa CHAKAMWATA Taifa, Mwalimu Meshack Kapange.
Baadhi ya Walimu wanasema wanasubiri mwezi mmoja wa barua waliyoitoa ili kutaka malipo kwa walimu ya zaidi ya shilingi billion 12 lasivyo wataenda mahakamani kushtaki ili walimu kupata stahiki zao na wamejiunga na Chama hicho kwasababu kimejidhatiti kutetea maslahi ya walimu bila ubaguzi wa walimu waajiriwa na wasio ajiriwa.
Pia soma ~ Kuna hili suala la Walimu kutoka CWT kuhamia vyama vingine vya Wafanyakazi, sisi Walimu wa Mbeya DC limekuwa changamoto