TANZIA Chaki (Jaffar Kasmali) mchezaji wa Cosmopolitan na timu ya taifa amefariki leo New York

Usichokijua ni bora unyamaze kimyaa.Unadhihirisha ujahili wako.
Mimi niliishi mtaa wa Lumumba kabla ya uhuru ninaifahamu vizuri Cosmo na sababu ya kifo cha Cosmo. Hizi timu tatu Yanga, Simba na Cosmo zilikuwa na mtazamo wa waswahili, waarabu na washihili, kubali kataa.
 
Washihili ndio kina nani?Wana asili ya wapi?Cosmopolitan FC ilianzishwa mwaka 1956 na wachezaji wa asili zote na ndio maana ya jina hilo Cosmopolitan ili kuwa timu isiyofungamana na timu kubwa za Simba,na Yanga.Ilichukua ubingwa 1967.Wachezaji mashuhuri waliowahi kuichezea ni pamoja na Katinko,Jumanne Masimenti na Mohamed Bakari Tall.
 
Kwa kweli umebarikiwa sana kwa uwezo wako wa kuandika simulizi, hata kama ni habari ya kawaida unavyoandika inavutia sana ni kama vile unahadisia habari kwa mdomo wako yaani ni kama unazungumza, ni kipaji kwa kweli.
 
Mimi niliishi mtaa wa Lumumba kabla ya uhuru ninaifahamu vizuri Cosmo na sababu ya kifo cha Cosmo. Hizi timu tatu Yanga, Simba na Cosmo zilikuwa na mtazamo wa waswahili, waarabu na washihili, kubali kataa.
Cosmo Washihiri,Sunderland aka Simba Waarabu na Yanga Wandengereko, Wamatumbi hohe hahe akina yakhe Wananchi waswahili,makuli wa bandarini, Yanga ndio timu ya Wananchi asilia hasa hawa watu wa Pwani
 
Kama hauwajui washihiri basi siwezi kujadiliana na wewe, asante kwa kushiriki.
 
Kama hauwajui washihiri basi siwezi kujadiliana na wewe, asante kwa kushiriki.
Hakuna watu wanaoitwa washihiri.Makabila ya wayemen yanajulikana.Katika makabila yote ya Yemen hakuna watu wanaoitwa washihiri.Kama ni jina la utani la wafanyabiashara wa nguo kutoka Yemen inawezekana.Hamna kabila la kutoka Yemen linaitwa kiasili washihiri.Umekaririshwa kimazoea.
 
Inna li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun.

Habari nzito hii. Ndiyo kwanzza naiona hapa.

Kaka zetu hao, mdogo wake, Maleki bado yupo Upanga, Mwenyekiti wa CCM.

Mwenyezi Mungu awarehem ndugu zetu wote wanaotutangulia, aturehem na sisi tunaofatia. Amiin.
 

Alama Mohamed Said kuna mtu mmoja pembeni yangu hapa nimemuonesha hii habari, kwanza kasikitika sana halafu kanambia, nikukumbushe walikuwepo pia (Difu), Abuu (Marwa), Jamil (Dennis Law). Kitwana (Douglas). Marande. Mohamed Msomali.


Mwenyezi Mungu awarehem wote waliotangulia. Amiin.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…