CHAKRA: Gurudumu la nishati katika mwili wa mwanadamu

CHAKRA: Gurudumu la nishati katika mwili wa mwanadamu

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
UTANGULIZI

Chakra ni vituo vya nishati katika mwili wa mwanadamu. Vituo hivi vinaaminika kuunganishwa na ustawi wa kimwili, kiroho, na kihisia! Kulingana na Patanjali, baba wa sayansi za kiyoga, katika kitabu chake kiitwacho "The Yoga Sutras", kuna jumla ya chakra 114. Lakini katika somo letu tutajifunza 7 au 9 peke yake.

Kila chakra inahusishwa na rangi maalum na inasimamia kazi maalum katika mwili, kama vile afya ya kimwili, ubunifu, na hisia.

Kwa kuzielewa na kuziamsha chakra hizi, mtu anaweza kuboresha ustawi wake kwa ujumla na kuishi maisha yenye usawa zaidi.

Katika utangulizi huu, tutachunguza chakra 7, moja baada ya nyingine, zilizomo ndani ya mwili, na njia tofauti ya kuziamsha zote, na chakra nyingine 2 za ziada. Hizi 2, moja chini na nyingine juu, ziko nje kabisa ya mwili. Kwa hiyo, kwa jumla tutachunguza chakra 9.

Chakra ya 6 hujulikana kama "third eye" au jicho la tatu. Tutakapofika hapo tutajifunza kuwa kumbe hii dunia ya nje tunayoiona ni kivuli tu cha dunia ya ndani tusiyoiona, na kwamba macho ya kimwili ni kwa ajili ya dunia ya nje na jicho la tatu ni kwa ajili ya dunia ya ndani.

Tutajifunza pia jinsi ya kufumba na kufumbua kwa jicho la tatu, kwa kushirikiana na "pineal grand" (au antena ya jicho la tatu) na akili isiyotambua (au "subnconscious mind").

Baadaye tutajifunza kuhusu kanuni za ulimwengu. Kuna Kanuni au Amri 12 zinazoendesha ulimwengu huu kimwili! Kama tutakavyojifunza chakra, tutajifunza amri hizi moja baada ya nyingine hadi tuzielewe zote. Tukizielewa tutauelewa ulimwengu kwa kiwango cha juu.

Utafiti wa mada hizi umekamilika. Na usingekamilika bila Dipak Tanna, rafiki yangu wa kiroho. Dipak, huyo hapo kwenye picha upande wa kulia, ameshirikiana nami katika utafiti wa mada hizi tangu mwaka 2022; na hata sasa bado anaendelea kushirikiana nami.

Lengo la kufundisha mada hizi si kumbadili mtu dini au imani. Ni kusaka maarifa sahihi, pamoja na wasomaji wangu, kutoka katika kila pembe ya dunia hii ya kimazingaombwe. Hivyo, kuwa huru kujifunza mambo usiyoyajua.

Kwa upande wa kanuni za ulimwengu, mtu yeyote yuko huru kujifunza—hata kama wewe ni Mkristo au Mwislamu! Ni kanuni zilizoumbwa kwa ajili ya ulimwengu huu, bila kujali dini au imani ya mtu.

Watu waliofanikiwa sana katika dunia hii wanatumia chakra na kanuni za ulimwengu kutawala dunia; na hawataki mimi na wewe tuyajue maarifa haya, kwani watashindwa kututawala. Kuwa mmoja wao kwa kuanza na chakra.

—Enock Maregesi, mwanafalsafa na mwandishi wa vitabu
 
ROOT CHAKRA (MULADHARA):
CHAKRA YA KWANZA KABISA NA MSINGI WA CHAKRA ZOTE

ROOT CHAKRA, pia ikijulikana kama Muladhara, au chakra ya msingi kwa Kiswahili, iko chini kabisa ya uti wa mgongo. Chakra hii inahusishwa na kipengele cha Dunia cha asili; na inahusishwa pia na hisia zetu za msingi, uthabiti na usalama kwa jumla.

Chakra ya Muladhara ina wajibu wa kudumisha mshikamano wa mtu na uhalisia wake wa kimwili, na pia kumuunganisha mtu huyo na mwili wake kupitia mitetemo. Muladhara ni msingi wa chakra nyingine zote na inahusishwa pia na hisia za amani na usalama.

Chakra hii ya msingi inapokuwa sawa, yaani inapokuwa haina shida yoyote, mtu huwa anajisikia amani na salama ulimwenguni. Lakini pale inapokuwa na shida au haiko sawa, yaani pale inapokuwa haifanyi kazi sawasawa, mara nyingi mtu huwa anapata hofu, wasiwasi, kutojiamini na kutokutulia pia kwa akili yake.

Mtu anaweza pia kupata ugumu wa kushughulika na mambo ya msingi kabisa katika maisha yake, kama vile kuoga au kufanya kazi yoyote, na huenda akajisikia kujichukia au kutengana na mwili wake mwenyewe. Yaani, anaweza kujisikia kukata tamaa kabisa ya kuishi.

Kuna njia chache za kuiweka sawa chakra ya muladhara. Tahajudi ("meditation") na yoga ni njia nzuri za kuanzia. Kuzingatia mazoezi ya viungo. Kuzingatia mazoezi ya kifikra, kama vile kuwaza umejikita kwenye uso wa Dunia (tena ukiwa umeshikilia shina kubwa la mti ili usipeperushwe na upepo), kunaweza pia kusaidia kuleta usawa katika chakra hii.

Au kula vyakula vyenye matunda ya ardhini kama vile karoti, karanga, viazi, na mihogo kunaweza pia kusaidia kuiamsha upya chakra ya muladhara.

Kutumia muda wako mwingi katika asili, kama vile kutembelea mbuga za wanyama au kuogelea baharini au ziwani, au kuoga kwenye maporomoko ya maji au mvua mara kwa mara, kunaweza pia kuleta manufaa katika chakra hii ya msingi.

Kutembea bila viatu kwenye nyasi, au kwenye ardhi, kutumia muda kiasi milimani, au kutumia muda kiasi tu kuupenda na kuustaajabia uumbaji wa Mungu, nako kunaweza kusaidia kuiamsha na kuiweka sawa chakra hii ya rangi nyekundu.

Mrisho Mpoto, mwanamuziki wa Tanzania, ama anajua au hajui, huwa anaitumia vizuri sana chakra ya muladhara—pale anapokuwa anatembea peku. Maana yake ni kwamba, muda mwingi anapotembea bila viatu huwa anaonesha mapenzi yake kwa asili kupitia kipengele cha Dunia. Matokeo yake asili inampenda Mpoto kama Mpoto anavyoipenda asili.

Asili ikikupenda huna budi kufanikiwa, kwa kuwa sasa wewe na asili mmekuwa kitu kimoja.

Chakra hii inayowakilishwa na sayari ya Mirihi (au "Mars"), pamoja na madini kama vile "black tourmaline" au "red coral," inapoamshwa na kufanya kazi sawasawa, mtu anaweza kujisikia amani, salama, na kushikamana na asili au ulimwengu unaomzunguka.

Lakini kumbuka, sijasema kuwa kwa kuwa Mpoto anatembea peku basi na wewe utembee peku kama yeye. Hapana, sijasema hivyo. Kuna njia nyingi, kama nilivyozielezea hapo awali, zinazoweza kukufanya uwe kitu kimoja na asili na bado ukafanikiwa kama alivyofanikiwa Mpoto.

Wala sijasema ubadili imani yako na kufuata imani ya Kihindu au Kibuda! Unaweza kutembea peku, au kuyaamini maarifa haya, kwa hiari yako mwenyewe.
1684100134917.jpg

—Enock Maregesi, mwanafalsafa na mwandishi wa vitabu

Ambition plus paqwa
 
SACRAL CHAKRA (SVADHISTHANA):
CHAKRA YA PILI BAADA YA MULADHARA

SACRAL CHAKRA, pia ikijulikana kama Svadhisthana, au Chakra Takatifu kwa Kiswahili, ni kituo cha pili cha nishati kilichoko chini ya tumbo—chini kidogo ya kitovu. Chakra hii inahusiana na kipengele cha Maji cha asili; na inahusishwa na ubunifu, furaha, na hisia! Svadhisthana inatawala mahusiano yetu, uwezo wetu wa kujisikia raha, na uwezo wetu wa kuhusiana na wengine. Wakati chakra hii iko sawa na wazi, tunaweza kufurahia mahusiano yenye afya, kuwa wabunifu na kujiamini katika ujinsia wetu, na kueleza hisia zetu kwa uhuru.

Chakra ya Sacral inahusishwa na rangi ya machungwa. Kuitazama rangi hii kifikra, wakati wa tahajudi ("meditation") au yoga, kunaweza kusaidia kuiweka sawa chakra ya Sacral. Shughuli nyingine kama vile kucheza muziki, kuimba, au kupiga ala pia zinaweza kusaidia kuifungua na kuiweka sawa chakra ya Sacral, kwa sababu zinahusisha ubunifu na miondoko.

Kwa mujibu wa Dipak Tanna, guru na mwimbaji wa Tanzania, wakati chakra ya muladhara inawakilishwa na sayari ya Mirihi au ("Mars"), svadhisthana inawakilishwa na Zuhura (au "Venus"). Inawakilishwa pia na rangi ya machungwa; na madini kama vile almasi, zirconi, "sunstone", na yaspi nyekundu.

Aidha, svadhisthana inawakilishwa na kipengele cha Maji cha asili. Yaani, majimaji yote ya mwilini; kama vile jasho, mate, makamasi, mkojo, damu, pamoja na shughuli zote zinazoambatana nayo kama vile kukojoa, kupenga au kutema mate, yanawakilishwa na chakra hii takatifu.

Wakati chakra hii takatifu iko nje ya usawa, tunaweza kupata hisia za hatia, aibu, au ukosefu wa amani katika mahusiano yetu. Tunaweza pia kuwa hatupendi kabisa kukosolewa, au tunapenda sana kuwakosoa wengine.

Dalili za kimwili kama vile maumivu ya chini ya mgongo, masuala ya uzazi, au maambukizi ya kibofu cha mkojo, yanaweza pia kuonesha hitilafu katika chakra ya Sacral.

Njia mojawapo ya kufanya chakra ya Sacral ifunguke na kufanya kazi vizuri ni kufanya mazoezi ya kujitunza (au "self-care"). Oga maji ya moto, tumia muda wako mwingi katika mazingira asilia, na jizoeshe kufanya shughuli za kiakili kama vile tahajudi au yoga.

Kuona mwanga wa machungwa kifikra, unaozunguka sehemu ya chini ya tumbo lako, chini ya kitovu, pia kunaweza kusaidia chakra ya Sacral ifunguke na kufanya kazi yake sawasawa.

Chakra ya Sacral ikishafunguka na kufanya kazi yake sawasawa, tunaweza kupata furaha katika mahusiano yetu. Tunaweza kuwa huru kufanya lolote, na tunaweza kueleza hisia zetu kwa uhuru zaidi hali kadhalika. Zawadi ya chakra ya Sacral ni kuweza kuungana na wengine, kwa njia sahihi na yenye maana.
1684100296397.jpg

—Enock Maregesi, mwanafalsafa na mwandishi wa vitabu
 
SOLAR PLEXUS CHAKRA (MANIPURA):
CHAKRA YA TATU INAYOWAKILISHWA NA JUA

SOLAR PLEXUS CHAKRA, pia ikijulikana kama Manipura, au Chakra ya Vito kwa Kiswahili, ni chakra ya tatu iliyoko tumboni, juu kidogo ya kitovu. Chakra hii inahusiana na kipengele cha Moto cha asili; na inahusishwa na uwezo binafsi, nia, na dhamira; na pia ikiwakilishwa na jua na rangi ya manjano. Solar plexus inawajibika kwa nishati inayochochea shughuli zetu za kimwili na kiakili, pamoja na uwezo wetu wa kufanya maamuzi na kuchukua hatua.

Chakra ya solar plexus ndiyo chanzo cha nguvu zetu za kibinafsi, kujiamini na kujithamini. Ni kituo cha nishati yetu ya kimwili na kiakili, na nyumbani kwa dhamira yetu. Inatusaidia kudhihirisha malengo na matamanio yetu, na kuchukua hatua kuunda maisha tunayoyataka. Wakati chakra ya solar plexus iko sawa na inafanya kazi vizuri, tunahisi kuwezeshwa na kuyadhibiti maisha yetu.

Chakra hii ya solar plexus inapokuwa nje ya usawa, yaani, inapokuwa haifanyi kazi sawasawa, tunaweza kujisikia dhaifu, kutokuwa na utulivu wa kihisia, na kushindwa kufanya maamuzi au kuchukua hatua. Tunaweza pia kuhisi wasiwasi, woga, au kulemewa na mambo. Dalili za chakra ya solar plexus isiyokuwa sawa zinaweza kujumuisha matatizo katika mfumo wa usagaji wa chakula, uchovu, na ugumu wa kuzingatia mambo.

Kurejesha usawa katika chakra hii ya manipura, ni muhimu kufanya mazoezi ya kujijali, kujipenda, na kauli chanya. Ni muhimu pia kuungana na asili, pamoja na kufanya mazoezi ya yoga, tahajudi na kupumua. Kujihusisha na madini na vito, kama vile "sunstone", "citrine", jicho la chui, na rubi (mawe maarufu sana miongoni mwa wachawi na waganga), kunaweza pia kusaidia kuiweka sawa na kuiponya chakra ya solar plexus.

Chakra ya solar plexus ni sehemu muhimu ya mfumo wetu wa nishati, na ni jambo la muhimu kwetu kudumisha usawa wake, ili tuishi maisha yenye tija na usawa. Kwa kuchukua fursa ya kuikuza chakra hii adhimu, tunaweza kurejesha usawa wake; na pia kuunda msingi thabiti wa afya yetu ya kimwili, kiakili na kiroho.
1684100450361.jpg

—Enock Maregesi, mwanafalsafa na mwandishi wa vitabu
 
HEART CHAKRA (ANAHATA):
CHAKRA YA NNE KATIKA MFUMO WA CHAKRA SABA

HEART CHAKRA, pia ikijulikana kama Anahata, au Chakra ya Moyo kwa Kiswahili, ni chakra ya nne katika mfumo wa chakra saba. Iko katikati ya kifua. Hii ndiyo chanzo cha upendo usiokuwa na masharti, huruma, furaha, na amani ya ndani. Ni daraja kati ya ulimwengu wa kimwili na wa kiroho, unaoturuhusu kuungana na nafsi zetu za juu na njia yetu ya kiroho.

Chakra ya moyo inahusishwa na rangi ya kijani na kipengele cha Hewa cha asili. Inawakilishwa na Mwezi. Siku yake ni Jumatatu. Na vito vyake ni "moonstone" na lulu. Wakati chakra hii iko wazi na inafanya kazi kama inavyotakiwa, huwa tunapata hisia za upendo, huruma, na mahusiano mazuri na wengine.

Chakra ya moyo inawajibika kwa mtiririko wa upendo, huruma, na fadhili kutoka katika mioyo yetu hadi kwa wale walio karibu nasi. Pia ni kitovu cha akili yetu ya kihisia na uwezo wetu wa kuzielezea hisia zetu. Chakra hii inapokuwa haifanyi kazi vizuri, tunaweza kupata hisia za chuki, huzuni, kutengwa, na wivu.

Anahata inahusishwa pia na tezi ya uvumba (au "thymus gland"). Tezi hii ndiyo inayowajibika kwa afya ya mfumo wetu wa kinga ya mwili, na haitafanya kazi ikiwa anahata haifanyi kazi. Anahata inapokuwa sawa, huwa tunakuwa na mfumo thabiti wa kinga ya mwili—pamoja na hisia nzuri zaidi ya ustawi wetu kiafya.

Kuiweka chakra ya anahata katika mfumo wake asilia, ni muhimu sana kufanya mazoezi; yatakayokuza ustawi wetu wa kihisia kama vile tahajudi, yoga na umakini wa akili. Pia ni muhimu kustawisha mahusiano yetu na wengine, na kuonesha huruma na upendo wetu usiokuwa na masharti yoyote. Tunaweza pia kutumia vito kusaidia kuifungua chakra hii, kama vile "quartz" ya waridi na pia "aventurine" ya kijani.

Chakra ya moyo ndiyo kitovu cha ustawi wetu wa kiroho; na inapowekwa sawa, tunaweza kupata furaha ya kweli na uhusiano mzuri na ulimwengu unaotuzunguka. Kwa kuikuza na kuiweka sawa chakra hii, tunaweza kuunda maisha ya amani ya ndani na furaha ya kweli yatakayoangazia nje uhusiano wetu—pamoja na mazingira yetu.

Unaposikia mganga anasema nyota yako imechafuliwa au imeibwa, kinachochafuliwa au kuibwa ni chakra. Yaani, chakra ndiyo nyota. Wachawi wanaweza kufunga chakra moja au zote, hivyo kukuletea matatizo makubwa sana katika maisha yako.

Mchawi anaweza kukulisha chakula fulani kichawi au katika hali ya kawaida. Kwa kuwa chakula kile hakitaendana na mfumo wa mwili, kitafunga chakra (au nyota) aliyokusudia.

Suluhisho kuu la tatizo la nyota ni tahajudi, yoga, vito, mazoezi ya viungo na kifikra, na mapenzi ya kweli kwa ulimwengu unaokuzunguka. Chunga sana chakra zako, hasa anahata.
1684100632042.jpg

—Enock Maregesi, mwanafalsafa na mwandishi wa vitabu
 
THROAT CHAKRA (VISHUDDHA):
CHAKRA YA TANO DUME-JIKE GETI LA ULIMWENGU WA ROHO

THROAT CHAKRA, pia ikijulikana kama Vishuddha kwa Kisanskriti, au Chakra ya Koo kwa Kiswahili, ni chakra ya tano katika mfumo wa chakra saba za mwilini. Iko katikati ya koo. Hii ndiyo chanzo cha mawasiliano, kujieleza na ubunifu. Inahusishwa na rangi ya bluu na kipengele cha Anga cha asili.

Chakra ya koo inawakilishwa na sayari ya Utaridi (au "Mercury"). Inawakilishwa pia na vito kama vile "lapis lazuli", "aquamarine", na "turquoise". Siku yake ya juma ni Jumatano, na ina nguvu ya kiume na kike au "ying" na "yang" kwa pamoja. Nguvu hizi hufanya kazi kwa pamoja kuleta usawa ulimwenguni.

Kila chakra ni ama dume au jike. Lakini chakra ya koo ni dume-jike au "ying-yang". Chakra tano za mwanzo zinahusika na ulimwengu wa mwili, mbili za juu zinahusika na ulimwengu wa roho. Chakra ya koo ni mpaka au geti kati ya ulimwengu wa mwili na ulimwengu wa roho. Ndiyo maana ina nguvu ya kiume na nguvu ya kike kwa wakati mmoja.

Kila kitu hapa ulimwenguni kina nguvu ("energy") ya kiume au ya kike, kulingana na kanuni ya ulimwengu iitwayo "Gender" au Jinsia. Lakini chakra ya koo inazo zote mbili kwa sababu ya umuhimu wake wa kuunganisha chakra mbili za juu na tano za chini za msingi.

Umewahi kusikia watu wanaitwa dume-jike? Wenye jinsia mbili? Watu hao hutawaliwa na chakra ya koo, na wana nguvu sana hasa ya maneno. Wakikulaani laana yao lazima ikupate! Tutajifunza zaidi kuhusu kanuni hii katika mada za kanuni 12 za ulimwengu hapo baadaye, baada ya mada za chakra.

Chakra ya koo inahusishwa pia na hisia ya kusikia, pamoja na uwezo wa kujieleza kwa njia ya uwazi na ya kujiamini. Inawajibika kwa mawasiliano, kwa maneno ya kutamka na ya kimoyomoyo. Pia inahusishwa na uimbaji, uzungumzaji mzuri, na ubunifu wa mtu katika kuelezea hisia zake.

Wakati chakra ya koo iko sawa na inafanya kazi barabara, mtu huwa na uwezo wa kuwasiliana kwa uwazi na kwa ufanisi zaidi, na hujieleza kwa njia nzuri na yenye afya ya mawasiliano. Pia huwa na uwezo wa kuelezea ubunifu wake kwa njia ya kujenga na yenye mantiki. Wakati chakra ya koo imezibwa au haiko sawa, inaweza kujidhihirisha katika maisha ya mtu kama changamoto ya mawasiliano, ugumu wa kujieleza, na kutoweza kupata hata ubunifu wa sauti yake mwenyewe.

Kutibu chakra ya koo, ni muhimu kufanya mazoezi ya tahajudi, kupumua kwa uangalifu, na mikao ya yoga. Pia ni muhimu kufanya mazoezi ya kuimba na kuzungumza, kwani shughuli hizi husaidia kufungua kituo cha nishati ya koo. Shughuli nyingine zinazoweza kusaidia kufungua na kuing'arisha chakra ya koo ni pamoja na kusema ukweli, kuandika habari, na kujihusisha na shughuli za ubunifu kama vile uchoraji au kuandika vitabu.

Wakati chakra ya koo iko wazi na inafanya kazi vizuri, mtu anaweza kueleza ukweli wake wa ndani na ubunifu wake kwa uwazi na kujiamini. Pia ni muhimu kuzingatia mawasiliano ya mtu na kujieleza kwake, kwa kuwa hizi ni zana zenye nguvu ambazo zinaweza kutumika kuunda mahusiano mazuri na yenye maana.
1684100763084.jpg

—Enock Maregesi, mwanafalsafa na mwandishi wa vitabu
 
THIRD EYE CHAKRA (AJNA):
CHAKRA YA SITA. CHAKRA YA JICHO LA TATU

THIRD EYE CHAKRA, pia ikijulikana kama Ajna, au Chakra ya Jicho la Tatu kwa Kiswahili, ni chakra ya sita katika mfumo wa chakra saba za msingi. Iko katikati ya paji la uso, sambamba na katikati ya macho, na inahusishwa na kipengele cha Mwanga cha asili. Chakra hii inahusishwa pia na hisia, ufahamu, na uangavu wa kiakili.

Chakra ya jicho la tatu ni lango la mifumo ya juu ya ufahamu, na inadhaniwa kuwa ni chanzo cha hekima yetu ya ndani. Wakati chakra hii iko sawa na wazi, tunaweza kuufikia ufahamu wetu wa ndani na hisia yetu ya ndani, ikituruhusu kufanya maamuzi kulingana na mwongozo wetu wa kiroho, badala ya akili yetu ya kimantiki. Tunaweza pia kupata uzoefu wa maono, uwezo wa kuona mambo nje ya ulimwengu huu.

Ajna inahusishwa na hisia ya kuona, kwa hiyo ni muhimu kuhakikisha kuwa macho yetu yana afya. Kumtembelea daktari wa macho mara kwa mara, kupumzika vya kutosha, na kupunguza kukutana na mwanga wa buluu vyote vinaweza kusaidia kuyaweka macho yetu ya kimwili katika hali ifaayo.

Chakra ya jicho la tatu inahusishwa pia na rangi ya nili na mafuta muhimu ya ubani, mrujuani na msandali. Nili ni rangi ya buluu iliyoiva yaani kati ya buluu na zambarau. Tahajudi, kuandika, na kushikamana na asili au ulimwengu, kunaweza pia kusaidia kufungua na kuiweka sawa chakra ya jicho la tatu.

Chakra ya ajna inawakilishwa na sayari ya Zohali (au "Saturn"). Inawakilishwa pia na vito kama vile yakuti ya buluu ("blue sapphire"), amethisto ("amethyst"), na tanzanaiti ("tanzanite"). Siku yake ya juma ni Jumamosi, na ina nguvu ya kiume na kike au "ying" na "yang" kama ilivyo chakra ya koo.

Kuvaa vito vya yakuti, amethisto au tanzanaiti kwenye mikufu, pete au bangili, kutasaidia sana kufunguka kwa chakra ya jicho la tatu. Kwani mawimbi ya nguvu ya sumaku-umeme kutoka katika vito hivyo huendana na mawimbi ya nguvu ya sumaku-umeme ya chakra ya jicho la tatu, kiasi cha kuipa chakra hiyo nguvu kubwa ya kufunguka na kufanya kazi vizuri.

Tahajudi, yoga, na kutoa sauti ya "AUM" (iitwayo "beej mantra") kwa muda mrefu mara kwa mara, kunaweza pia kusaidia sana kuifungua na kuiweka sawa chakra ya jicho la tatu.

Josè Silva, mwandishi wa kitabu kiitwacho "Mind Control Method', anasema kuwa ikiwa mtu anataka kuijua na kuidhibiti dunia yake ya ndani hana budi kujifunza jinsi ya kutumia jicho la tatu ipasavyo. Anasema kuwa mbinu nzuri zaidi ya kufungua jicho la tatu ni kutafuta kwanza sehemu iliyotulia, hususan usiku kabla ya kulala.

Kisha fumba macho yako ya kimwili. Vuta pumzi nyingi na kuitoa taratibu mara tatu au zaidi, kutuliza fikra zako nyingi. Kisha, ukiwa bado umefumba macho, geuza macho yako kana kwamba unaangalia juu kwenye paji la uso. Utahisi shinikizo fulani katikati ya paji la uso. Shinikizo hilo ndiyo nishati yenyewe ya jicho la tatu, na hadi hapo jicho la tatu linakuwa limeshaanza kufunguka kwa ajili yako.

Kama anavyosema Quazi Johir, mhamasishaji wa jicho la tatu katika tovuti ya YouTube, unachotakiwa kufanya baada ya hapo ni kuhakikisha kifikra kuwa unaona mwanga wa buluu mbele ya paji lako la uso. Katikati ya mwanga huo, hakikisha unaona namba 333, kisha chini yake 222, kisha chini yake tena 111, ili akili yako iende sasa katika hatua ya "alpha" ya ubongo wako. Ukishaona "111" maana yake ni kwamba umeshaingia katika hatua ya "alpha" ya ubongo wako, na sasa uko tayari kufokasi katika jambo unalolitaka.

Kwa mujibu wa Johir, katika hatua hiyo ya "alpha" fikiria tatizo lako! Kisha kifikra lipeleke tatizo hilo moyoni, na lifanye kuwa jambo linalokusumbua sana. Baada ya hapo hesabu kimoyomoyo tatu hadi moja, kisha (kifikra hivyohivyo) lirushe tatizo hilo kwa nguvu hadi juu kabisa ya kichwa chako (ambako sasa ni mbinguni). Ukifanya hivyo, shida yako tayari umeshamkabidhi Mwenyezi Mungu aishughulikie na si kazi yako tena kuifikiria.

Fikiria sasa suluhisho la tatizo lako. Kama ulivyofikiria tatizo, fikiria suluhisho hivyohivyo. Ukiwa bado uko kwenye hatua ya "alpha", lione jawabu la tatizo lako moyoni. Lifanye jawabu hilo kuwa kubwa sana moyoni mwako. Yaani, jione unafurahia sana kupata suluhisho la tatizo lako.

Kisha, baada ya kuhesabu tatu hadi moja, lishike lile tatizo na kulirusha kwa nguvu hadi nje kabisa ya kichwa chako (yaani mbinguni kwa Mungu Baba). Quazi Johir anasema, baada ya hapo shida yako imekwisha. Subiri siku tatu, kama bado hujapata jawabu, rudia tena; ila fanya hivyo kila baada ya siku tatu hadi jawabu lipatikane.

Chakra ya jicho la tatu inatuwezesha kuitazama dunia yetu ya ndani, wakati macho ya kimwili yanatuwezesha kuitazama ya nje. Dunia ya nje ni kivuli tu cha dunia ya ndani. Umewahi kusikia watu wakisema "Dunia hii ni 'illussion'"? Maana yake ni kwamba dunia hii ni kivuli na dunia halisi ni ya ndani.

Ni sawa na kusimama kando ya kioo. Wewe ni dunia ya ndani, kivuli chako upande wa pili wa kioo ni dunia ya nje—hii inayoita "illussion". Ukitaka kubadili dunia yako ya nje lazima ubadili dunia yako ya ndani kwanza, kwa sababu kivuli hakiwezi kubadilika chenyewe. Na hutaweza kufanya hivyo bila nsaada wa chakra ya jicho la tatu.

Kwa kuifungua na kuiweka sawa chakra ya jicho la tatu, tunaweza kuufikia ufahamu wetu wa ndani; hivyo kuturuhusu kufanya maamuzi yenye hekima na busara. Tunaweza pia kuonja uzoefu wa mifumo ya juu ya ufahamu, kupata uangavu juu ya kusudi la maisha yetu, na kushikamana na Mungu wetu wa mbinguni.
1684100933587.jpg

—Enock Maregesi, mwanafalsafa na mwandishi wa vitabu
 
  • Thanks
Reactions: BRN
CROWN CHAKRA (SAHASRARA):
CHAKRA YA 7 KATIKA MFUMO WA CHAKRA 7

CROWN CHAKRA, pia ikijulikana kama Sahasrara, au Chakra ya Taji kwa Kiswahili, ni chakra ya saba katika mfumo wa chakra saba za msingi. Iko juu ya kichwa katikati, na inahusishwa na nishati ya uhusiano wa kimungu na ufahamu wa kiroho. Chakra ya taji inahusishwa na rangi nyeupe na urujuani (au "violet"), na kipengele chake ni Fikra. Sayari yake ni Mshtarii (au "Jupiter"), na siku yake ya juma ni Alhamisi.

Chakra ya taji ndiyo chanzo cha muunganiko wetu wa kiroho na ulimwengu wa kimwili. Ni chanzo cha hisia zetu, uelewa na ufahamu wa juu. Inahusishwa na muunganiko wetu wa kiroho pamoja na uungu, na muunganiko wetu kwa uhalisia wa maisha yetu.

Wakati chakra ya sahasrara imefunguliwa na inafanya kazi vizuri, mtu anaweza kuunganishwa na nafsi yake ya juu, kupata mwongozo wa kimungu, na kupata maarifa kuhusu kusudi lake maishani. Pia anaweza kutambua muunganiko wa viumbe vyote, na kupata hisia ya kuwa kitu kimoja na ulimwengu unaomzunguka.

Chakra ya taji inapokuwa sawa, mtu anahisi kushikamana na mamlaka ya juu na pia kuwa na imani ya kina na uaminifu katika ulimwengu. Anakuwa mtu mwenye hisia zaidi, mbunifu zaidi, na muwazi zaidi kwa mamlaka za juu za ufahamu. Anakuwa mjuzi zaidi wa njia yake ya kiroho, na mazoea yake ya kiroho yanakuwa na maana zaidi kwake. Pia anakuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na upendo usiokuwa na masharti yoyote, kukubalika, na anakuwa na amani ya moyo hali kadhalika.

Kwa upande mwingine, wakati chakra hii ya taji imezibwa, mtu anaweza kuhisi kutengwa na chanzo chake cha kiroho, au kuhisi kutengwa na kusudi la maisha na uhalisia wa maisha yake, na pia kutengwa na nafsi yake mwenyewe ya juu. Anaweza kuhisi kupotea, kuchanganyikiwa, na kufadhaika moyo. Anaweza pia kupata hisia za hatia, aibu, na kukata tamaa.

Chakra ya taji inaweza kuwekwa sawa kupitia mazoea mbalimbali ya kiroho kama vile tahajudi, yoga, na kuimba (au "mantra", hasa "beej mantra" iitwayo "AAH" au "OM" ya kimyakimya). Mbinu za taswira, kama vile kuona kifikra kuwa mwanga mweupe unatoka juu ya kichwa chako na kusambaa mwili mzima, zinaweza pia kusaidia kufungua na kuiweka sawa chakra ya taji. Kwa kuongezea, vito kama vile amethisto, yakuti ya manjano, topazi ya manjano, "howlite", na "quartz ya kioo, vinaweza pia kutumika kusaidia kufungua na kuiweka sawa chakra ya saba.

Chakra ya saba ni sehemu muhimu ya safari yetu ya kiroho. Inapokuwa sawa, mtu anaweza kupata hisia ya kina ya uhusiano na Muumba pamoja na nafsi yake ya kweli. Anaweza pia kupata wasaa wa kuchungulia ndani ya kusudi la maisha yake, kumruhusu kuishi maisha yenye uradhi na maana kwa wote.
1684101107255.jpg

—Enock Maregesi, mwanafalsafa na mwandishi wa vitabu
 
EARTH STAR CHAKRA:
"CHAKRA YA MABILIONEA" ILIYOKO INCHI KUMI NA MBILI CHINI YA MIGUU

EARTH STAR CHAKRA, pia ikijulikana kama Vasundhara, au Chakra ya Nyota ya Dunia kwa Kiswahili, ni kituo cha nishati kilichoko takriban inchi sita hadi kumi na mbili chini ya miguu. Ni sehemu ya mfumo wa nishati ya binadamu, pamoja na chakra nyingine kuu saba, ambazo zimepangwa kuanzia chini kwenye uti wa mgongo hadi kichwani katikati. Chakra ya nyota ya dunia inahusishwa na kipengele cha Dunia cha asili, na inasemekana kuwa ndiyo msingi mkuu wa mfumo wa nishati ya binadamu. Inaaminika kuwa ndiyo chanzo cha nishati ya mshikamano, ambayo husaidia kuiweka miili yetu ya kimwili, kihisia, kiakili na kiroho katika usawa.

Chakra hii wengine wamefikia hata hatua ya kuipa jina la utani la "Chakra ya Mabilionea" au "Chakra ya Mafanikio", kwa kuwa chakra hii (pamoja na muladhara) hutoa uimara wa mtu katika kufanya mambo, msimamo na kutokukata tamaa anapoishi kwenye sayari hii.

Kama nilivyosema hapo awali, vasundhara iko takriban inchi 12 (au sentimeta 30) chini ya miguu yako ikikuunganisha na dunia ya ajabu inayosemekana kuwa chini ya ardhi, katikati ya sayari ya Dunia, iitwayo "Hollow Earth". "Hollow Earth" ni dunia inayosemekana kuwa na viumbe wenye nguvu na akili sana. Inajulikana kitaalamu kama "Seventh-Dimensional Hollow Earth". Fanya utafiti wako kuhusiana na maajabu haya. Chakra ya nyota ya dunia inaimarisha uhusiano wako na dunia zote mbili, pamoja na kusudi lako kwenye dunia hii. Inakupa hisia ya kupendwa, kukaribishwa, na kuwa duniani kwa wakati huu katika maisha haya.

Chakra hii ya mabilionea imeunganishwa na chakra ya muladhara (chakra yetu ya kwanza), ambayo iko chini kabisa ya uti wa mgongo. Inaaminika kuwa ndiyo msingi wa maisha yetu, na ndiyo msingi wa chanzo cha afya yetu ya kimwili, kihisia, kiakili na kiroho. Wakati chakra hii iko sawa na inafanya kazi kama kama inavyotakiwa, tunahisi usalama na kujiamini sana katika uwezo wetu wa kuunda na kutimiza ndoto zetu.

Chakra ya nyota ya dunia inahusishwa pia na rangi ya kijani kibichi, na mara nyingi huwakilishwa na nyota yenye ncha sita. Nyota hii inasemekana kuwakilisha pande sita za Dunia ambazo ni kaskazini, kusini, mashariki, magharibi, juu, na chini; na vipengele vinne vya asili ambavyo ni hewa, maji, moto na dunia.

Wakati chakra ya nyota ya dunia iko sawa, tunaweza kuhisi kushikamana na Dunia pamoja na nishati ya asili au ulimwengu. Tunaweza pia kujisikia thabiti, salama, na kujiamini katika uwezo wake wa kuishi pamoja na asili au ulimwengu. Tunaweza kutimiza ndoto na malengo yetu kwa urahisi, na kubaki tulivu na wenye msimamo wakati wa dhiki na changamoto.

Kuiweka sawa chakra ya nyota ya dunia ni muhimu kutumia muda wetu mwingi katika asili, kufanya mazoezi ya msingi kama vile yoga na tahajudi, na kutumia muda wetu mwingi kila siku kushikamana na Dunia. Pia ni manufaa kufanya mazoezi ya maono na kutamka kauli chanya za mafanikio, zinazolenga kuungana na kuwa kitu kimoja na Dunia. Zaidi ya hayo, kula mlo kamili wenye afya, kuepuka vyakula vilivyochakatwa kwa madawa mbalimbali, na pia kushiriki katika mazoezi ya kawaida, kunaweza kusaidia kuiweka chakra ya nyota ya dunia katika hali nzuri.

Kuhitimisha mada hii, chakra ya nyota ya dunia ni kituo muhimu cha nishati kilichoko takriban inchi sita hadi kumi na mbili (au sentimeta 30) chini ya miguu. Inahusishwa na kipengele cha Dunia, na ni msingi wa mfumo wa nishati ya binadamu. Wakati chakra hii iko sawa, tunaweza kuhisi kushikamana na Dunia pamoja na nishati ya ulimwengu, na kutimiza ndoto na malengo yetu kwa urahisi. Kuiweka chakra hii katika hali nzuri ni muhimu kutumia muda wetu mwingi katika asili, kufanya mazoezi ya viungo na akili, na kula kiafya chakula kilichokamilika.
1684104143275.jpg

—Enock Maregesi, mwanafalsafa na mwandishi wa vitabu
 
How? maana naona ni ngumu sana na unaweza kuadapt hiyo life style lakini usione effects zozote yaani nisione umuhimu wowote
Ukifanya meditation, ukabadilisha ulaji, ukabadilisha aina ya vinywaji na ukatumia spiritual stones for chakras utaanza kyona mabadiliko kwa kasi
 
Ukifanya meditation, ukabadilisha ulaji, ukabadilisha aina ya vinywaji na ukatumia spiritual stones for chakras utaanza kyona mabadiliko kwa kasi
hapo kwenye ulaji na vinywaji sijui ni vipi vinafaa hayo mawe sijawahi hata kuwaza uwepo wa hiko kitu so inshort tu nothing i know about them
 
Back
Top Bottom