Chakula Cha Dagaa na ugali

Chakula Cha Dagaa na ugali

JEJUTz

Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
75
Reaction score
197
Safisha dagaa na uwaweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia dagaa wakaange kidogo kisha tia chumvi, pilipili, curry powder, turmeric, na nyanya chungu, koroga vizuri mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri kisha tia nyanya na ufunike. Pika mpaka nyanya iive kisha kamulia limao,na pia hakikisha nyanya chungu zimeiva kidogo(usiache mpaka ziive sana manake zitavurugika pindi utakapotia tui la nazi) kisha malizia kwa kutia tui la nazi na uache lichemke mpaka rojo ibakie kidogo. Hakikisha nyanya chungu na zimeiva ndo uipue. Na hapo dagaa wako watakuwa tayari kwa kuliwa na ugali.
 

Attachments

  • IMG-20240823-WA0007.jpg
    IMG-20240823-WA0007.jpg
    69.7 KB · Views: 19
Safisha dagaa na uwaweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia dagaa wakaange
Ukifanya hivyo utaunguza kitunguu,usingoje vitunguu viwe brown ndo utie dagaa!
 
Back
Top Bottom