Chakula cha sikukuu

Thad

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2017
Posts
13,380
Reaction score
31,566
Heri ya Pasaka wana JF

Nimezoea miaka yote siku za sikukuu kama hizi naalikwa na ndugu,jamaa na marafiki kwenda kula nao sikukuu ila hali imekuwa tofauti pasaka hii, mpaka sasa sijapata mwaliko wowote....

Naombeni mnishauri na mnifundishe chakula gani kizuri nitakachoweza kupika/kuandaa na kuifurahia sikukuu.

Kinywaji niameamua kuandaa juice yenye mchanganyiko wa maziwa, maembe, pasheni, parachichi, ukwaju na asali.
 
Nasubiri waje..ila nielekeze ulipo nije kudoea maana si kwa juice hyo
 
Kama unapenda ugali basi ugali kwa samaki wa kukaanga na mchicha pembeni itapendeza.
 
Asubuhi anza kwa chai ya rangi kwa matembele. Mchana pata zako mabumunda shushia juisi ya bamia. Jioni isindikize kwa senene wa kuchoma na ulanzi mkali mkuu.Jus'kidding,boss!
 
Unasema ukweli hiyo juice au unatania?? lol

Kuhusu chakula me naona ni vema ule chakula ukipendacho maana hapa watu watalutakia vyakula wapendavyo wao labda wewe hupendi... swali lako ungelileta kua kuna chakula flani unataka kupika ila huwezi hivyo unaombwa kuelekezwa.

Ila sijui kwanini nimeitazama post yako kwa jicho la tatu ipo kama inayoomba mwaliko vile hehehehe.

Wisdom will kill me walai.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] my dear nashukuru kwa kung'amua kuwa nimeomba mwaliko kijanja lakini bado sijakaribishwa. Naomba unielekeze namna ya kupika biriani ili nipambane tu na hali yangu!

Hiyo juisi ni ya kweli ndugu. Ni juisi flani amazing sana.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] my dear nashukuru kwa kung'amua kuwa nimeomba mwaliko kijanja lakinu bado sijakaribishwa. Naomba unielekeze namna ya kupika biriani ili nipambane tu na hali yangu!

Hiyo juisi ni ya kweli ndugu. Ni juisi flani amazing sana.
 
Kama unapenda ugali basi ugali kwa samaki wa kukaanga na mchicha pembeni itapendeza.
Asante kwa ushauri wako japo hiki ndio chakula changu cha mara kwa mara itabidi tu nile hiki hiki maana sioni dalili ya kufunzwa pishi jipya hapa.
 
Nasubiri waje..ila nielekeze ulipo nije kudoea maana si kwa juice hyo
Wamegoma kuja kunielekeza, ila juisi yetu tayari njoo tunywe hiyo hiyo tu [emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Karibu kwangu ule mama. Nimepika kuku wa kukaanga nyama roast wali pilau na viazi vya kukaanga. Ila naenda kula kwa kigogo ntakusindikiza na picha wakati ukinywa juice yako ya kuongeza nguvu za kike. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Asante dear! Ngoja nijisogeze pande zako ili nije kufaidi hilo pilau.
Ebu kwanza, unaenda kula kwa kigogo yupi cepholacaudo / Mr Miller au nani? [emoji12]
 
Asante dear! Ngoja nijisogeze pande zako ili nije kufaidi hilo pilau.
Ebu kwanza, unaenda kula kwa kigogo yupi cepholacaudo / Mr Miller au nani? [emoji12]
Tuanze na hiki.

Kigogo mwingine sio shemeji zako [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wow! Ushanitia njaa mwenzio [emoji39] [emoji39] [emoji39] ila kwa kuwa kabila langu linaniruhusu wacha tu nile kwa picha [emoji12]
Bado sijakutia njaa vizuri mama kuwa mpole [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bado sijakutia njaa vizuri mama kuwa mpole [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Haya bi mdada nipe nipe, mwisho wa siku nitachagua picha ya kushushia juisi yangu. [emoji39] [emoji39] [emoji39]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…