Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Ni kawaida kuwa na hasira lakini usifanye mambo ukiwa na hasira.
Unapoacha kuongea na watu, basi acha kuwaongelea pia, yani unakuta mtu ameamua asiongee na Etugrul Bey lkn cha kushangaza unakuta anamzungumzia huyo legend.
Katu usiruhusu kuvunjiwa heshima yako au kushusha thamani yako ili watu wakupende,hata uwaridhishe vipi hawata kupenda.
Kile watu wanachofikiria kuhusu wewe hakihusiani na kile unachojifikiria wewe binafsi.
Mda na matatizo yatadhibitisha ukweli wa thamani yako kwa watu.
Kataa wazo ambalo hulipendi,ila usikatae wazo kwakuwa tu humpendi mtu huyo.
Waheshimu watu hata kama hawastahili heshima yako,kama hauwezi basi kaa kimya.
Usishiriki katika mijadala na mtu ambaye mda wote anajiona yupo sahihi.
Ni hayo tu!