Chakula cha wanasayansi nje ya dunia

Chakula cha wanasayansi nje ya dunia

storyteller

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2014
Posts
1,511
Reaction score
1,844
Wanajamvi, wasalaam

Nimekua nikiwaza kuhusu vifaa vinavyoenda kufanya tafiti kwenye sayari zingine mf. Apolo, vifaa hivi nina hakika vimetengenezwa kuwa na mwendikasi kwa kuzingatia vigezo vingi, mf. Uzito na idadi ya watu wataokapanda, vifaa vya uchunguzi vitakavyobebwa n.k

Swali langu ni kwamba, wanaapolo(wanasayansi wanaoenda kufanya tafiti nje ya dunia) wanaopanda mule maisha yao yanategemea chakula, sasa,
Je, wakati wa uundaji wa hivyo vyombo(apolo) huwa wanaweka buti la misosi, je, debe ngapi za dona na maharagwe zinaweza kuingia?

Na kama hawabebi chakula, huwa wanakula nini katika kipindi chao cha uchunguzi huko angani.?

Nawasilisha.
 
Na mi nasubiri jibu, ila uki google utapata majibu
 
usiwaze sana huwa wanakunywa vidonge vya kutuliza njaa
 
huko angani wana vituo vyao vya kuhifadhia mizigo ikiwemo vyakula
 
A hahahahaha haha, kaka umenikumbusha kipindi nipo mtoto kulikuwa na katuni ya TOm and jerry, ilikuwa inahusu trip ya kwenda mwezini. Mle kuna professor alitengeneza magic foods kwa kutumia unga, ukiweka drop ya maji ile unga unabadilika kutokana na contents zake. Mfano unga ni wa beef burger basi chakula kinabadilika na kuwa beef burger. Wakaenda nao mwezini siku zote ndo nilikuwa chakula chao.
 
Wanajamvi, wasalaam

Nimekua nikiwaza kuhusu vifaa vinavyoenda kufanya tafiti kwenye sayari zingine mf. Apolo, vifaa hivi nina hakika vimetengenezwa kuwa na mwendikasi kwa kuzingatia vigezo vingi, mf. Uzito na idadi ya watu wataokapanda, vifaa vya uchunguzi vitakavyobebwa n.k

Swali langu ni kwamba, wanaapolo(wanasayansi wanaoenda kufanya tafiti nje ya dunia) wanaopanda mule maisha yao yanategemea chakula, sasa,
Je, wakati wa uundaji wa hivyo vyombo(apolo) huwa wanaweka buti la misosi, je, debe ngapi za dona na maharagwe zinaweza kuingia?

Na kama hawabebi chakula, huwa wanakula nini katika kipindi chao cha uchunguzi huko angani.?

Nawasilisha.

Umeuliza maswali ya muhimu. Kwa ufupi niseme hakuna binadamu aliyewahi kusafiri angani zaidi ya kilomita laki 4. Safari ya mwisho ya binadamu anga za mbali ilikuwa ni mwezini mwaka 1972. Kwa sasa kuna Kituo cha Kimataifa cha Anga (International Space Station) kilichopo kilomita zaidi ya 420 angani, ambacho huzunguka dunia kila baada ya dakika 90 kwa mwendo kasi wa maili 18,000 kwa saa. Katika kituo hicho huwepo wanasayansi wanaoishi na kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi hasa sayansi ya anga za juu.

Kituo hicho hupata mahitaji kutoka duniani. Wanasayansi (wakiwemo wa Marekani) hupelekwa na kurudishwa duniani na chombo cha safari za anga cha Urusi kinachoitwa Soyuz baada ya kile cha Marekani, Shuttle, kusitisha huduma.

Safari za anga za mbali hufanywa kwa kutumia vyombo peke yake. Kwa mfano, NASA ilituma chombo, New Horizons, kwenda kuchunguza sayari ya Pluto, ambayo Jumuiya ya Kimataifa ya masuala ya anga ilishaiondoa kwenye orodha ya safari. Chombo hicho kilisafiri maili zaidi ya bilioni 3 kwa muda wa miaka 9.5 na mwaka huu ulipita Pluto ambapo imethibitisha kuwa ni sayari.

Jibu la swali lako kwa uhakika ni kwamba binadamu hajawahi kwenye umbali wa kilomita zaidi ya laki 4 (Mwezini).
 
A hahahahaha haha, kaka umenikumbusha kipindi nipo mtoto kulikuwa na katuni ya TOm and jerry, ilikuwa inahusu trip ya kwenda mwezini. Mle kuna professor alitengeneza magic foods kwa kutumia unga, ukiweka drop ya maji ile unga unabadilika kutokana na contents zake. Mfano unga ni wa beef burger basi chakula kinabadilika na kuwa beef burger. Wakaenda nao mwezini siku zote ndo nilikuwa chakula chao.

Mkuu una miaka mingapi sasa mbona hiyo katuni haivuki miaka mitano toka imetoka mm mzee na bado naangalia katuni na wanangu raha sana
 
Imetoka siku nyingi sana niko Std Six kama sikosei, hizi za sasa ni collections tuu za zamani ndo hawa machunga wanatembeza barabarani. Ingia you tube ndo zipo latest zaidi.
 
Umeuliza maswali ya muhimu. Kwa ufupi niseme hakuna binadamu aliyewahi kusafiri angani zaidi ya kilomita laki 4. Safari ya mwisho ya binadamu anga za mbali ilikuwa ni mwezini mwaka 1972. Kwa sasa kuna Kituo cha Kimataifa cha Anga (International Space Station) kilichopo kilomita zaidi ya 420 angani, ambacho huzunguka dunia kila baada ya dakika 90 kwa mwendo kasi wa maili 18,000 kwa saa. Katika kituo hicho huwepo wanasayansi wanaoishi na kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi hasa sayansi ya anga za juu.

Kituo hicho hupata mahitaji kutoka duniani. Wanasayansi (wakiwemo wa Marekani) hupelekwa na kurudishwa duniani na chombo cha safari za anga cha Urusi kinachoitwa Soyuz baada ya kile cha Marekani, Shuttle, kusitisha huduma.

Safari za anga za mbali hufanywa kwa kutumia vyombo peke yake. Kwa mfano, NASA ilituma chombo, New Horizons, kwenda kuchunguza sayari ya Pluto, ambayo Jumuiya ya Kimataifa ya masuala ya anga ilishaiondoa kwenye orodha ya safari. Chombo hicho kilisafiri maili zaidi ya bilioni 3 kwa muda wa miaka 9.5 na mwaka huu ulipita Pluto ambapo imethibitisha kuwa ni sayari.

Jibu la swali lako kwa uhakika ni kwamba binadamu hajawahi kwenye umbali wa kilomita zaidi ya laki 4 (Mwezini).

Pamoja na maelezo yako mazuri, lakini hujajibu swali. Hawa wanasayansi walioko kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga, huwa wanakula chakula cha aina gani? Je kuna vyoo? Na je katika mwenzo kasi wa Km 18,000 kwa saa, mwanadamu anaweza kwenda haja?
 
Supply and logistics mkuu

Kila baada ya miezi sita chakula na material nyingine zintaumwa huko juu kwa kutumia unmanned space shuttles

Mara nyingi zinatumwa kutoka Baikanour Cosmodrome,Kazakhstan nchi ya uangalizi wa Roscosmos(Russia)

Na kwa miaka ya karibuni kuna watabe wengine wame join industry kama SpaceX nchini ya Elon Musk,Orbital Sciences etc
 
Umeuliza maswali ya muhimu. Kwa ufupi niseme hakuna binadamu aliyewahi kusafiri angani zaidi ya kilomita laki 4. Safari ya mwisho ya binadamu anga za mbali ilikuwa ni mwezini mwaka 1972. Kwa sasa kuna Kituo cha Kimataifa cha Anga (International Space Station) kilichopo kilomita zaidi ya 420 angani, ambacho huzunguka dunia kila baada ya dakika 90 kwa mwendo kasi wa maili 18,000 kwa saa. Katika kituo hicho huwepo wanasayansi wanaoishi na kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi hasa sayansi ya anga za juu.

Kituo hicho hupata mahitaji kutoka duniani. Wanasayansi (wakiwemo wa Marekani) hupelekwa na kurudishwa duniani na chombo cha safari za anga cha Urusi kinachoitwa Soyuz baada ya kile cha Marekani, Shuttle, kusitisha huduma.

Safari za anga za mbali hufanywa kwa kutumia vyombo peke yake. Kwa mfano, NASA ilituma chombo, New Horizons, kwenda kuchunguza sayari ya Pluto, ambayo Jumuiya ya Kimataifa ya masuala ya anga ilishaiondoa kwenye orodha ya safari. Chombo hicho kilisafiri maili zaidi ya bilioni 3 kwa muda wa miaka 9.5 na mwaka huu ulipita Pluto ambapo imethibitisha kuwa ni sayari.

Jibu la swali lako kwa uhakika ni kwamba binadamu hajawahi kwenye umbali wa kilomita zaidi ya laki 4 (Mwezini).
Kaa ujue na hili kuwa hakuna binadamu aliyewahi kufika Mwezini.
 
Back
Top Bottom