Wanajamvi, wasalaam
Nimekua nikiwaza kuhusu vifaa vinavyoenda kufanya tafiti kwenye sayari zingine mf. Apolo, vifaa hivi nina hakika vimetengenezwa kuwa na mwendikasi kwa kuzingatia vigezo vingi, mf. Uzito na idadi ya watu wataokapanda, vifaa vya uchunguzi vitakavyobebwa n.k
Swali langu ni kwamba, wanaapolo(wanasayansi wanaoenda kufanya tafiti nje ya dunia) wanaopanda mule maisha yao yanategemea chakula, sasa,
Je, wakati wa uundaji wa hivyo vyombo(apolo) huwa wanaweka buti la misosi, je, debe ngapi za dona na maharagwe zinaweza kuingia?
Na kama hawabebi chakula, huwa wanakula nini katika kipindi chao cha uchunguzi huko angani.?
Nawasilisha.