Chakula kipi ni kizuri kwa kufanya watoto wa nguruwe wakue na wawe na afya?

Pastory Kimaryo

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
967
Reaction score
668
Habari ya muda huu wajasiriamali wenzangu.

Kama mada inavyojieleza kwenye kichwa cha habari hapo juu ni vyakula gani vizuri kwa ajili ya vibwagala, mimi binafsi natumiaga makombo ila bado sioni kama yanaleta tija sana kwao sasa nataka nijue kama kuna chakula cha dukani ambacho ni kizuri au mchanganyiko wowote unaofaa.
 
Mkuu. Makombo ni ziada tu.
Nadhani pumba na mashudu mixer ndo safi kwao.

Mwone mzoefu akupe hata jinsi ya kuwapimia kadri wanavyoongezeka kukua
 
Achana na imani kuwa nguruwe anakula kila kitu. Ubora wa chakula huamua ubora wa nyama pia. Nyie ndio nyama zenu zikija mjini tunawalaumu wapishi wa kitimoto kumbe ni mfugaji alikuwa analisha nguruwe wake makombo ya kwenye kumbi za harusi.
 
Umeingia kwenye ufugaji kabla ya kupata elimu nzuri ya ufugaji, ulipaswa kufahamu nguruwe anahitaji lishe bora kabla haujaanza ufugaji. Lishe ya makombo itakupa matokeo duni. Tafuta machapisho na vitabu vinavyoelezea lishe bora ya nguruwe, watembelee wafugaji wazoefu pia waone wataalam wa mifugo.
 
Mkuu. Makombo ni ziada tu.
Nadhani pumba na mashudu mixer ndo safi kwao.

Mwone mzoefu akupe hata jinsi ya kuwapimia kadri wanavyoongezeka kukua
Dah, thanks mkuu umenifumbua kitu, kuna haja sasa ya kusoma ufugaji wa kitaalamu wa hawa wadudu
 
Dah thanks mkuu
 
Nashukuru kwa ushauri
 
Unachanganya pumba ya mpunga,ya mahindi,mashudu ya alizeti,soya/uduvi/dagaa,pigboost,mifupa,chokaa na chumvi.Nikituli nitakueleza namna yakuchanganya.
Dah, sisi wafugaji uchwara ndio tutakoma safari hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…