Chakula mixer pombe kali

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Posts
38,342
Reaction score
88,625
Basi enzi hizo tuko chuo kuna rafiki zangu walikuja kutoka Marekani wakanialika lunch na marafiki zangu apartment kwao.
Tukaenda na rafiki zangu watatu jumla tukawa wanne.
Kufika wakatuchomea nyama ya mbuzi wakailowesha na JD ila bila sisi kujua. Sasa muda wa kula nikaanza kuona kama nalewa flani na tumbo likaanza kukata. Nikawa naogopa kuuliza rafiki zangu.
Kumbe nao walikua wanapitia hali kama yangu. Basi nikamwambia mwenyeji mbona kama najihisi kulewa kuna nini. Akaniambia nyama aliweka JD. Nikawaambia wenzangu nao wakafungka wanajisikia vibaya flani hivi.

Hiyo picha ni leo mchana tena kuna rafiki zangu walipikiwa hivyo na mmoja wa gf zao. Nikakumbuka nilivyolewa bila kujua.
 
Yeees jd,whiskey,tequila,ni nzuri saaana kwenye kumarinate nyamaa esp za kuchomaa ,kuku yaaan ni balaaaa...makange ya chicken wings u can also mix jd na asali,soya black pepper ....


Ila kwenye kulewa nahisi walizidishaa saanaa nachojuaaa inakuwa na flavour ya pombe kwa mbali
 
My dear Mzigua90 ngoja nikupe fundisho la maakuli leo.

Mara nyingi wakati wa kupika nyama wazungu hupendelea kuweka pombe (hata beer wakati mwingine). Mara nyingi hutumia white wine.

Kutumia kilevi kwenye chakula kuna maana nyingi;

- flavour: pombe inachanganyika vizuri na mafuta na maji hivyo inasaidia kuongeza harufu nzuri kwenyc hakula chako. Kwa hili pombe inatumika tu kama seasoning.

- Pia kwa case ya nyama, inasaidia sana kuondoa harufu kali ya nyama (especially kama mbuzi). Unaweka kidogo tu maana ukiweka nyingi nayo inaharibu protini iliyopo kwenye nyama. Siri: tumia pombe nzito kwa red meat na pombe nyepesi (gin nk) kwa nyama nyeupe na seafood.

- Mbadala wa maji: hii nayo usiitumie sana. Hasa wakati unamalizia kupika, badala ya kuongeza maji basi unaweza kuongeza pombe.


Hao wamarekani wako kuna uwezekano mkubwa waliweka hiyo JD mwishoni mwa mapishi kwa mantiki hiyo kilevi chote hakikutoka. Generally ni ngumu kulewa kwa chakula kilichopikwa na pombe maana heat inaua uwezo wa kinywaji kile kukulevya.

Alternative nyingine, kwa kuwa umesema kuliambatana na maumivu ya tumbo, huenda your body doesn't react well to alcohol.

Ila mpaka ule nyama za kukulevya..nawe utakuwa mlafi. Yani inakubidi ule hasaa kama vile hizo nyama ndo lunch na dinner. Very rarely mtu utalewa kwa chakula kilichopikwa na pombe.
 
Yes kwenye kulewaa hapo ndo maana na mm nimesema itakuwa walizidisha au sijui walipikaje bt pombe mara nyingi huwa zinatumikaa kwenye nyama sana sana .....
 
Yes kwenye kulewaa hapo ndo maana na mm nimesema itakuwa walizidisha au sijui walipikaje bt pombe mara nyingi huwa zinatumikaa kwenye nyama sana sana .....

Tunatofautiana. Kuna mtu akinywa glass analewa mwingine mpaka amalize chupa.

Mimi nashukru sana pombe nina allergy nayo. Nitaumwa tumbo (kama alivyoelezea Mzigua) lakini huwa silewi (anyway..sijawahi kufikia threshold yangu). Aisee nimeshawahi kujaribu kunywa shots nne vodka na niliendelea ku-function kama kawaida. Shida inakuja asubuhi tumbo linauma sana. Vivyo hivyo kwa kahawa. Si nimeshajiamulia zangu mimi maji, juice na chai. Pombe situmii asilani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…