Chakula tunachokula kinasafirishwa vipi mpaka sehemu za siri?

kufanakupona

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2015
Posts
522
Reaction score
421
Nimegoogle sana,nimefikiria sana,nimeangalia michoro sana,bado sijapata jibu.
Nataka nifahamu,chakula tunachokula,au kinywaji tunachokunywa,inakuwaje kuwaje mpaka kinafikia sehemu za siri(za -me au -ke).Huwa tunasikia chakula fulani kinatibu sehemu za siri,maana yake kinaenda sehemu za siri,sasa process yake ipoje mpaka kufikia sehemu za siri?
 
Chakula kinasafiri mwilini kwa mtiririko huu.
Chakula huingia mdomoni na kusagwa sagwa kuwa vipande vidogo ili kuongeza surface area na kusaidia kipite vizuri kwenye alimentary canal.
Wakati wa utafunaji, mate huwa na vimeng'enya (enzymes)vinavyosaidia kumeng'enya (digest) wanga.
chakula husafiri kwenye tyube inayoitwa alimentary (food) canal inayoanzia mdomoni hadi mkunduni.
Tyube hii imegawanyika ktk maeneo yafuatayo: Mdomo, aesophagus, stomach, utumbo mwembamb, utumbo mpana na mukundu (cloaka).
Chakula husafiri kutoka mdomoni hadi kwenye tumbo kwa kutumia 'mwendo kasi' ujulikanao kama Peristalisis.
Kikifika tumboni mmeng'enyo huanza kutegemea na aina ya chakula.
Mfano vitamini zote huwa ni water soluble or fat soluble kwa hiyo hizi hunyonywa moja kwa moja toka tumboni hadi kwenye mishipa ya damu.
Madini kama Carbohydrates na Protein humeng'enywa kwa kutumia vimeng'enya vinavyoitwa Enzymes... Zoezi la kumeng'enya chakula hufanyika kwenye utumbo mwembamba.
Chakula kilichomengenywa hunyonya na mishipa ya damu ya kwenye utumbo na hiki chakula hupitishwa kwenye maini kunyonywa sumu kabla ya kusambazwa mwilini.
Yale makapi ya chakula husafirishwa toka kwenye utumbo mwembamba hadi utumbo mpana.. Kwenye utumbo mpana zoezi la kunyonya maji maji hufanyika na kufanya kinyesi kuwa kigumu.
Maji husafirishwa kupitia damu hadi kwenye figo ambayo inahusika na kubalance kiasi cha maji mwilini.
Kile kinyesi kwenye utumbo mpana husafirishwa hadi kwenye mukundu ambao umezibwa na sphincter muscles.. Hii ni misuli ambayo iko controled na voluntary muscles.. Pale mtu anapolegeza his sphincter muscles, mukundu hutanuka na zoezi la kuny.a ndio hufanyika.
 
Na hiyo tube inayotoka mdomoni hadi kunako inaitwaje?
 
Alimentary (food) canal.. Biology ngumu jaman lol!
Anamaanisha alimentary canal au food canal.
Bios mziki,mi' mwenyewe nilikimbiaga,maneno kibao ya kigiriki na kilatini.
 
Ahsante kwa update nzuri mkuu Kodofan.
Bado Niko palepale,tube inayotoka mdomoni hadi sehemu za siri inaitwaje?(kama kuna uwezekano)
 
Jaman si nimekwambia inaitwa "ALIMENTARY CANAL"
Niwie radhi kama nimekukera Mkuu
Hapo sasa nimepata picha alimentary canal imeungana na artery inayoelekea sehemu za siri.
Kuna haja ya kudadavua uhusiano kati ya alimentary canal na sex organs.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…