markp
Senior Member
- Sep 26, 2013
- 194
- 327
Ilikuwa jambo rahisi sana kumkamta mh Mbowe kwakuwa jeshi la polisi ni mali ya ccm bila shaka. Ikawa rahisi pia kuchagua kesi ya kuanzisha ambayo ni ya ugaidi na uhujumu uchumi. Tatizo linalowakabili sasa ni kuwa walijipanga kumsumbua na kumtesa tu mbowe ili wengine waogope na mwisho walitegemea CDM wangepiga magoti na kumuomba mama amsamehe mbowe ngoma imekuwa tofauti na matarajio yao. CDM hawatii huruma wala kurudi nyuma kama ilivyotarajiwa badala yake wako tayari kuona kesi inafutwa au iendelee na mbowe ashinde au kushindwa. Huwezi kuamini watawala kama kesi itaendelea watatamani mbowe ashinde kesi kuliko wao kushinda kwakuwa watawala wakishinda mbowe atatakiwa kunyongwa au kufungwa maisha kitu ambacho watawala hawako tayari kitokee kwani kitaleta mwamko mpya na ari mpya kwa dunia nzima.
Haya washauri wa watawala kazi mnayo wengine mko humu. Mkitupa chakula mlichopika wenyewe kila mtu atawashangaa na mkisema mle mkumbuke kutapika marufuku. Nasema hamruhusiwi kutapika.
Haya washauri wa watawala kazi mnayo wengine mko humu. Mkitupa chakula mlichopika wenyewe kila mtu atawashangaa na mkisema mle mkumbuke kutapika marufuku. Nasema hamruhusiwi kutapika.