Chalamila alipotoshwa, Mhandisi Gabriel usikubali

Chalamila alipotoshwa, Mhandisi Gabriel usikubali

MenukaJr

Member
Joined
Apr 24, 2021
Posts
50
Reaction score
128
Mhandisi Robert Gabriel karibu Mwanza. Wenyewe tunaita Rock City, Jiji la Miamba. Wewe sio mgeni Kanda ya Ziwa, unatufahamu. Bado tunaimba na kuomboleza!

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila alipotoshwa na yeye akapotosha umma, wewe usirudie kosa hilo. Tafuta chapisho langu la June 9 lenye kichwa cha habari "RC Chalamila-Mwanza amepotosha au amepotoshwa!?", litakusaidia. Ukifika ofsini irudie taarifa ya ziara ya Rais Mkoani Mwanza. Itangazie Dunia, pamoja na mambo mengine Rais atatembelea na kufungua kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery) kinachomilikiwa kwa ubia baina ya kampuni tatu, katika hizo Kampuni ya STAMICO inaiwakilisha Serikali ya Tanzania kwa asilimia 25.

Taarifa ya Chalamila iliiondoa Serikali ya Tanzania katika umiliki huo, akaifanya kampuni ya Mwanza Precious Metals Rifinery (MPMR) kuwa Kampuni binafsi (Sekta binafsi). Hili ni kosa, zilikua dalili za kuiba hisa za (STAMICO) Serikali kama ilivyofanyika miaka ya nyuma kwenye Kampuni ya Celtel. Kama sio JPM kuzirudisha ndio tulikua tumeliwa hivyo hadi sasa. Hata nilipomwandikia hapa kumuomba Chalamila abadilishe statement yake aombe radhi, hakunisikiliza.

Mhandisi Gabriel, irudie taarifa hiyo. Iweke Serikali (STAMICO) katika position yake, Rais wa nchi hawezi kufungua kiwanda kinachomilikiwa kwa ubia na Serikali bila Serikali kutajwa. Haiwezekani! Usiwasikilize wanaosema hisa zetu ni kidogo (25%) hivyo hazina uamuzi katika Kampuni kwa hivyo kutozihesabu ni haki.

Hawa hawajui lolote kuhusu aina za umiliki wa biashara, wapuuze. Ingalikua wenye hisa kidogo hawatambulishwi katika umiliki, sisi tusingalitambulishwa katika umiliki wa kampuni ya kusafirisha mafuta ya EACOP ambapo tuna hisa 15% sawa na Uganda. Itambulishe Serikali katika umiliki wa MPMR utakuja kunishukuru baadae.

Usiwasikilize wenye kusema kuwa mabango ndio yamemuondoa Chalamila Mwanza. Hakuna Rais asiyependa Mabango kwa sababu ndio mawasiliano ya haraka kutoka chini kwenda juu. Mabango ndiyo yenye kumfahamisha Rais uwajibikaji wa watendaji wake, mabango yangalikua sababu Chalamila angaliondolewa baada ya mabango kusomwa.

Mabango hayaondolewi kwa kupigwa marufuku bali kutatua changamoto za watu. Kauli ya Chalamila kuhusu mabango ilikua ni ya uwajibikaji kwake na wenzake, sio kosa. Rais mwenyewe alisema mabango yasizuiliwe, kwa vyovyote vile hilo haliwezi kuwa kosa la kumuondoa Mkuu wa Mkoa. Nisikilize mimi, irudishe nafasi ya Serikali katika umiliki wa kiwanda cha kuchenjua dhahabu halafu usisahau kuwa Katibu Tawala uliyenaye hapo ametoka Ikulu.

Utanikumbuka baadaye!

MenukaJr,

Da'slama-Tanzania.
 
Naamini kuna sababu nyingine iliyofanya Chalamila akaondolewa ofisini tofauti na hiyo uliyoandika hapa.

Kama ulichokiandika kina ukweli basi watendaji wake Chalamila ndio watakuwa wamemponza, hivyo sikutegemea wewe uje hapa uanze kumlaumu Chalamila moja kwa moja wakati mtu hata miezi mitatu alikuwa bado hajamaliza ofisini.

Hata kama shida yako ni hiyo taarifa kuondoa umiliki wa serikali wakati kimsingi bado upo kama unavyodai, bado sioni sababu ya kumuondoa Chalamila ofisini kwa issue ambayo ingemalizwa ndani ya dakika chache tu kwa kufanyia marekebisho palipokosewa kwenye hiyo taarifa.
 
Kwa upande mwengine chalamila kuhamasisha wananchi waje na mabango, Ni kama katika mchakato wa kufufua UCHAFU huo ? Wa kuiondoa serikali katika ubia wa asilimia 25%

Mbona tunaweza kuja na Mada ya kwamba chalamila alifanyia preplanned trick kuwa outwon na ipatikane sababu nzuri ya kumuondoa kwenye uongozi
 
Kwamba huko Mwanza Rais wa JMT anaenda kufungua kiwanda cha kuchenjua dhahabu ambacho kinamilikiwa na Serikali kupitia STAMICO na mwekezaji na kuunda kampuni ya ubia kwa jina la Mwanza Precious Metals Refinery (MPMR).

Hili ni jambo jema lakini nashauri Serikali isiishie kwenye kujimilikisha hisa kwenye rasilimali za umma kama ilivyokuwa huko nyuma. Hata kama Serikali inamiliki hisa kidogo iwe hata asilimia 25, ni vema kampuni hiyo ikaorodheshwa kwenye soko la hisa DSE hata ikibidi ianzishwe Mwanza Stock Exchange ili sehemu ya hisa ziuzwe kwa wananchi taasisi na mashirika binafsi.

Kama hilo halitafanyika, tutegemee kuona kampuni mpya itakayowanufaisha wawekezaji na wateule wachache Serikalini na hasa vigogo wa STAMICO. Tusiruhusu historia mbaya ijirudie!!
 
Kwa upande mwengine chalamila kuhamasisha wananchi waje na mabango, Ni kama katika mchakato wa kufufua UCHAFU huo ? Wa kuiondoa serikali katika ubia wa asilimia 25%

Mbona tunaweza kuja na Mada ya kwamba chalamila alifanyia preplanned trick kuwa outwon na ipatikane sababu nzuri ya kumuondoa kwenye uongozi
Masalia ya magufuli yanaondolewa taratibu.
 
Mhandisi Robert Gabriel karibu Mwanza. Wenyewe tunaita Rock City, Jiji la Miamba. Wewe sio mgeni Kanda ya Ziwa, unatufahamu. Bado tunaimba na kuomboleza!

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila alipotoshwa na yeye akapotosha umma, wewe usirudie kosa hilo. Tafuta chapisho langu la June 9 lenye kichwa cha habari "RC Chalamila-Mwanza amepotosha au amepotoshwa!?", litakusaidia. Ukifika ofsini irudie taarifa ya ziara ya Rais Mkoani Mwanza. Itangazie Dunia, pamoja na mambo mengine Rais atatembelea na kufungua kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery) kinachomilikiwa kwa ubia baina ya kampuni tatu, katika hizo Kampuni ya STAMICO inaiwakilisha Serikali ya Tanzania kwa asilimia 25.

Taarifa ya Chalamila iliiondoa Serikali ya Tanzania katika umiliki huo, akaifanya kampuni ya Mwanza Precious Metals Rifinery (MPMR) kuwa Kampuni binafsi (Sekta binafsi). Hili ni kosa, zilikua dalili za kuiba hisa za (STAMICO) Serikali kama ilivyofanyika miaka ya nyuma kwenye Kampuni ya Celtel. Kama sio JPM kuzirudisha ndio tulikua tumeliwa hivyo hadi sasa. Hata nilipomwandikia hapa kumuomba Chalamila abadilishe statement yake aombe radhi, hakunisikiliza.

Mhandisi Gabriel, irudie taarifa hiyo. Iweke Serikali (STAMICO) katika position yake, Rais wa nchi hawezi kufungua kiwanda kinachomilikiwa kwa ubia na Serikali bila Serikali kutajwa. Haiwezekani! Usiwasikilize wanaosema hisa zetu ni kidogo (25%) hivyo hazina uamuzi katika Kampuni kwa hivyo kutozihesabu ni haki. Hawa hawajui lolote kuhusu aina za umiliki wa biashara, wapuuze. Ingalikua wenye hisa kidogo hawatambulishwi katika umiliki, sisi tusingalitambulishwa katika umiliki wa kampuni ya kusafirisha mafuta ya EACOP ambapo tuna hisa 15% sawa na Uganda. Itambulishe Serikali katika umiliki wa MPMR utakuja kunishukuru baadae.

Usiwasikilize wenye kusema kuwa mabango ndio yamemuondoa Chalamila Mwanza. Hakuna Rais asiyependa Mabango kwa sababu ndio mawasiliano ya haraka kutoka chini kwenda juu. Mabango ndiyo yenye kumfahamisha Rais uwajibikaji wa watendaji wake, mabango yangalikua sababu Chalamila angaliondolewa baada ya mabango kusomwa. Mabango hayaondolewi kwa kupigwa marufuku bali kutatua changamoto za watu. Kauli ya Chalamila kuhusu mabango ilikua ni ya uwajibikaji kwake na wenzake, sio kosa. Rais mwenyewe alisema mabango yasizuiliwe, kwa vyovyote vile hilo haliwezi kuwa kosa la kumuondoa Mkuu wa Mkoa. Nisikilize mimi, irudishe nafasi ya Serikali katika umiliki wa kiwanda cha kuchenjua dhahabu halafu usisahau kuwa Katibu Tawala uliyenaye hapo ametoka Ikulu.

Utanikumbuka baadaye!

MenukaJr,

Da'slama-Tanzania.
Ona ili jinga nalo!!
 
Mhandisi Robert Gabriel karibu Mwanza. Wenyewe tunaita Rock City, Jiji la Miamba. Wewe sio mgeni Kanda ya Ziwa, unatufahamu. Bado tunaimba na kuomboleza!...
Something fishy is cooking here...kunahitajika uchunguzi wa kina...Kwani usipoweka neno serikali ndiyo inaondoa uhalali wa hizo hisa 25%

Kwanini unam pre-empty Mkuu wa Mkoa ajaye?

There is untold story here...Umakini unahitajika, msimwingize Mh. Rais kwenye shida zenu...Kabla ya Mh. Rais kuingizwa chaka hii kitu iangaliwe kwa jicho la tatu
 
Mhandisi Robert Gabriel karibu Mwanza. Wenyewe tunaita Rock City, Jiji la Miamba. Wewe sio mgeni Kanda ya Ziwa, unatufahamu. Bado tunaimba na kuomboleza!....
Mimi sijakuelewa. Hebu rudi kwenye microphone tena utueleweshe vizuri.

1. Kwamba, huo mgawanyo wa hisa miongoni mwa wanahisa/wamiliki wa hiyo kampuni ya MPMR ni wa maneno tu au uko kisheria na kimaandishi/kimkataba?

2. Kama ni wa kisheria, sasa inawezekanaje matamshi tu ya RC kwa kupitiwa au kukosea yatengue uhalali wa serikali kumiliki hisa 25%?

NOTE:
å Aliyekuwa RC Mwanza ndugu Chalamila Albert iko sababu nyingine iliyomfanya aondolewe kwenye nafasi hiyo

å Hii unayoitaja, niungane na wengine kusema kuwa hai - make sense hata kidogo. Na kwa ufupi sana ni kuwa, huyu (Chalamila) kwa kauli na matendo yake hakuwa ana qualify kuwa kiongozi ktk level ya u - RC.

å Huyu anatakiwa apekekwe Chuo cha Sanaa Bagamoyo akawe mkufunzi huko!
 
Mradi unaandiko na hatua za utekelezaji chini wizara madini nk, kwamba taarifa ya RC iondoe share za serikali Kama zipo!?
Shangaa na wewe....Hii kelele inaashiria jambo nyuma ya hii kitu, jiwe limetupwa gizani lika bonda mtu akasahau halikulengwa kwake...
 
Back
Top Bottom