Chalamila amepaniki mpaka anawatishia maisha wafanyabiashara, adai akiwachimba mkwara hawataamka tena

Chalamila amepaniki mpaka anawatishia maisha wafanyabiashara, adai akiwachimba mkwara hawataamka tena

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mkuu wa mkoa, Albert Chalamila amefika Kariakoo kujaribu kufungua maduka lakini katika harakati hizo ameweka vitisho vilivyopitiliza..

Chalamila: Aliyekubali kufungua afungue na yule ambae atamletea mkwara mtu yeyote yule aliyekubali kufungua naapa mbele ya Mwenyezi Mungu, hapo ndipo nitakapoonesha shoo nzima. Wewe unakuja unamletea mkwara, mimi nitakuchimba mkwara na hautaamka tena, na hili naomba niwaeleze ndugu zangu wa Kariakoo, utoto ukizidi hatuwezi kufikia hapo"

Kingine Chalamila amesema andapo akienda kukaa Kariakoo na kukagua kodi na risiti hamna mfanyabiashara atabaki kuendelea kufanya biashara Kariakoo, kama Serikali inajua kodi zilizowekwa hazina uhalisia na hazilipiki na watu hawalipi kwanini wanaziweka? Mwisho ni kosa la jinai kutishia maisha ya mtu.

Pia, soma=> Chalamila awasili Kariakoo awaambia Wafanyabiashara “Fungueni maduka, Biashara sio Siasa”
 
Hichi kijumba kinafanya nini hapo kariakoo
Screenshot_20240624-122736.png
 
Mama aandike twita na kutoa amri.... Wenye leseni ya biashara mfungue maduka na TRA nendeni mkaangalie ambaye hajafungua mfute leseni yake ili afanye kazi nyingine.

Magu alikuwa anasema hajarubiwi.
 
Uwezo wa kufunga madanguro na kukamata machangudoa anao kwa saaaanah ila biashara na utawala bora ni zero minus.
 
Ningekuwa mimi ndio Rais, ningetoa agizo ndani ya masaa 6 biashara zifunguliwe na ambaye angegoma ingekula kwake mazima
 
Back
Top Bottom