⁵
Kuwa mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama haimaanishi yeye ni kamanda mkuu au amiri jeshi kwenye mkoa. Mkuu wa mkoa hana uwezo wa kuamrisha hata platuni moja ya jeshi, achilia2r mbali kikosi kizima.
Mkuu wa mkoa hana hata uwezo wa kuamrisha operesheni ya kipolisi mkoani mwake.
Mkuu wa mkoa au wilaya, anapokuwa mwenyekiti wa vikao vya kamati ya ulinzi na usalama, anakuwa kama mwenyekiti wa kamati ya arusi. Kwa vile uwezo wake unaishia kwenye kuongoza vikao lakini siyo kuwaamrisha makamanda wa majeshi au vikosi vya jeshi.
Vikosi vya jeshi katika kazi zao za kawaida, vinapokea amri kutoka kwa makamanda wa vikosi tu. Na kwa matukio makubwa ni baada ya tangazo la Amiri Jeshi Mkuu.