Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila leo Jumatatu Desemba 18, 2023 amesema kama kuna mkazi wa Dar es Salaam analalamika kuwapo kwa foleni katika jiji hilo, ahamie vijinini.
βKwa yeyote anayeendelea kulalamika mkoa huu labda una mambo mengi ikiwemo foleni, kuna vijiji vingi sana bado havijajaa wanaweza kuhamia huko.
βMkoa wa Dar es Salaam upo salama na hasa kwa wakati huu wakati wa kujiandaa na sherehe mbalimbali, kila mwaka wanaimarisha ulinzi lakini mwaka huu umeimarishwa zaidi,β amesema RC Chalamila.
Hayo ameyazungumza leo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya ustawi wa jamii na miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii yaliyofanyika jijini hapo.