Munyaluganda
Member
- Jul 13, 2022
- 7
- 21
Albert Chalamila Mhenga wa Kale
Sijui unamfahamu mkuu wa mkoa aliyewahi kufukuzwa kwa kashifa ya mabango? Huyu bwana mimi namuita Mwamba kwa sababu kutimuliwa ukuu wa mkoa tena na mwanamke na akabaki bila kujinyonga kwa Mhehe sio jambo dogo kabisa na anakwambia kufukuzwa ni laana inayomuandama tangu akiwa mdogo kwani hata alipokuwa kidato cha kwanza aliwahi kufukuzwa kisa amecheza juu ya meza ya Mwalimu na kuivunja hapo huyu Mhenga alikuwa akisoma shule ya sekondari Malangali iliyopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Ukibahatika kukutana na huyu bwana ni mtu mkarimu sana ila shida yake kubwa ni kwamba hapendi kuendweshwa. Wote waliosoma nae shule ya msingi Ikangamwani mwaka 1992 wanakwambia alianza kupishana na mwalimu wa Hesabu mlangoni akiwa darasa la tatu.Huyu bwana maisha yake yote hapendi Hesabu.
Huyu mwamba anakwambia siku aliyowahi kuwa na furaha sana ni siku aliyopata mke na anasema kipindi kilichokuwa kigumu kwake ni pale alipokuwa anafanya mtihani wa kidato cha sita kwa usimamizi maalumu wa polisi maana kwa kipindi hicho alikuwa ametimuliwa shule kabisa. Ukimsikia Chalamila huyu bwana ni mtata sana yaani alinishangaza kweli alipoamua kurudia mtihani wa kidato cha sita alipopata one ya pointi 7 mwaka 2004 na kupata one ya 5 mwaka 2005 baada ya kurudia,kama unabisha kaangalie matokeo ya kidato cha sita mwaka 2004 shule ya sekondari Malangali.
Mwamba anatushauri vijana tujikubali na hizi hali zetu za manati maana yeye wakati anasoma pale UDSM kwa shahada ya kwanza aliwahi kupenda binti wa IFM na akamhaidi kumtoa auti ila kumbe mwamba hana ela anajikaza tu kadi yake ya benki iko dhofuli hali. Aliingia ATM na kuweka kadi yake na muda wote ATM ilimuandikia neno hili “INSUFICIENT FUND PLEASE REMOVE YOUR CARD” mwamba aliendelea kushupaza shingo pale mpaka kadi ikamezwa. Ndipo akamwambia baby wake, aaaaaaaaaaaaah ona sasa kadi yangu imemezwa na pesa yangu yote ilikuwa humo. Binti akasema oooooooooh sory my babyyyyyyyy. Chalamila anasema ukweli yule binti hakuwa type yangu kabisa maana mimi nilikuwa Mwalimu naye alikuwa Mhasibu kwahiyo ilibidi tu apende kitengo chake cha pesa.
Waafrika wengi huwa tuna tabia ya kudharau cha kwetu na kuthamini sana cha wangine ila mwamba anapenda lugha yake ya Kiswahili kupita maelezo na ndicho kinachompatia mkate wa kila siku mpaka leo maana ameanza kazi akifundisha Kiswahili katika Chuo cha Kikatoliki Mwenge Moshi pale, akaenda SAUT na kumalizia Chuo Kikuu cha Iringa kabla hajaamia kwenye siasa mwaka 2017.
Huyu bwana anaamini kwamba hakuna kitu kinachokuja kwa bahati katika maisha ya mwanadamu isipokuwa KUFA tu ndiko huja kwa bahati ila mambo mengine yote huandaliwa maana mpaka anachaguliwa kuwa mkuu wa mkoa alikuwa mwanyekiti wa CCM mkoa wa Iringa. Mwamba anaamini sana katika kujaribu na ndio maana mdogo wake wa mwisho alipata ziro kidato cha nne ila sasa anasomea udaktari katika moja ya chuo kikuu mashuhuri huko Urusi.
Chalamila anasema wanafunzi wote wanaosoma UDSM wanasitahiri kupatiwa ulinzi maana hupitia nyakati ngumu sana wakati wakisoma yaani professa kuongea kingereza mwanzo wa kipndi hadi mwisho ni jambo la kawaida sana pale. Kusoma UDSM mwaka wa kwanza mpaka mwaka wa tatu na mwanafunzi atoke bila hata kujua ofisi moja ya maprofessa waliomfundisha ni jambo la kawaida sana pale.
Kwa mara ya kwanza mwamba aliporipoti pale UDSM, baada ya kipindi professa alimwambia amfate kwa sababu alikuwa na shida ya course work ila Professa alipoingia kwenye Pantoni kivukoni Chalamila aliendelea kumsubili Professa akijua ameingia ofisini maana aliona kama mlango ukifunguka na kujifunga maana mwamba alikuwa ametokea kijijini sana huko Mufindi ndanindani.