Chalamila omba wasaa ukutane na Mheshimiwa Rais uombe umueleze upande wako wa stori

Chalamila omba wasaa ukutane na Mheshimiwa Rais uombe umueleze upande wako wa stori

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Mimi naamini kabisa ndani ya moyo wako wewe ni mtu mzuri. Una sense of humor ambayo bahati mbaya wengine hawaielewi.

Naamini kilichokukuta safari hii ni watu wamekupiga fitna hasa wale Waliochukua clip ya sauti yako na kuikatakata kisha kuunganisha vipande.

Naamini kabisa kwenye ile clip hukumaanisha kuwa watu wabebe mabango ya kumtukana rais, bali ulitaka kuonyesha kuwa hutozuia bango la mtu yeyote hata kama anawatukana nyie watendaji wa mkoa.

Nikikulinganisha na mtu kama Sabaya au Makonda wewe ni Saint kabisa huna roho ya kikatili na kishenzi.

Sasa kutokana na hilo, Omba miadi na mheshimiwa rais, Chukua video nzima za press conference yako na waandishi wa habari, mueleze mheshimiwa rais kuwa waandishi wameikata hiyo taarifa na "kukutake out of context" kwa sababu za kiuchonganishi.

Pia, muombe radhi mheshimiwa rais kwa kumkwaza, maana teua tengua nayo ni kazi, lakini pia inaweza kumpa picha mbaya mbeke ya umma kuwa hayuko makini kwenye teua zake.

Ndugu Chalamila, wewe ni kiongozi mzuri sana, ila sasa utani ulikuwa mwingi lakini naamini kabisa kwenye hii ishu umekuwa "framed".

Tafuta namna ya kukutana na mheshimiwa rais umuelezee kirefu issue yako.

Lengo siyo uteuliwe, bali lengo liwe ni kuweka rekodi sawa!

Usiitishe press conference hivi karibuni kujisafisha, wewe tulia ila jisafishe kwanza mbele ya mamlaka
 
By any means ishu ya mabango haijamuondoa Ila statement yake aliyotoa alipokuwa anaongea na wananchi baada ya kupokea mashine za hospital alikosea sana. Huwezi kusema kwamba wananchi wa mwanza wasimchukulie Rais anawachukia eti wasiamini maneno kwamba yeye ndio alimuua Magu, hivi kweli hii ni statement ya kuongea wakati ambapo Rais anapanga kwenda kufanya ziara?

He is the author of his own book.
 
Hii tabia ya wana bavicha kula matapishi inachosha sana!

Si wewe ulikuwa unademka humu kila siku kwamba atolewe?
Nipe rekodi ya thread yangu au post yoyote niliyotaka Chalamia aondolewe Ukuu wa mkoa!, Haipo

Mimi nimekuwa nikimkubali huyu jamaa siku nyingi tu maana nimchapakazi hodari
 
ile ya hospitali kwamba wanamwanza wasimchukie samia hajamuuua magufuli is the worst of all time.
Naamini jamaa yupo kwenye kundi linaloamini hiyo conspiracy theory,mwingine huyu hapa tena naskia alikuwa kiongozi wa wanafunzi chuo kikuu
Screenshot_2021-06-11 Instagram.png
 
By any means ishu ya mabango haijamuondoa Ila statement yake aliyotoa alipokuwa anaongea na wananchi baada ya kupokea mashine za hospital alikosea sana. Huwezi kusema kwamba wananchi wa mwanza wasimchukulie Rais anawachukia eti wasiamini maneno kwamba yeye ndio alimuua Magu, hivi kweli hii ni statement ya kuongea wakati ambapo Rais anapanga kwenda kufanya ziara?

He is the author of his own book.
Infact pale alikuwa anamzungumzia rais in a very positive way.

Alichagua maneno yenye Ukakasi kidogo lakini The overall message ilikuwani kuwataka watu wamuelewe, wampe ushirikiano mheshimiwa rais katika kuleta maendeleo katika mkoa wao.
 
Nani alimwambia kwamba wananchi wa Mwanza wanamtuhumu Rais wa sasa kuhusika na kifo cha Magu? Kiongozi anayeropoka namna hii in the middle of ziara ya Rais Kanda ya ziwa huyu hafai ukichukulia yeye ndio mkuu wa mkoa Mwanza.

Hakupaswa kutoa Ile kauli aisee. Hiyo ni kama uchonganishi huwezi kumuacha kiongozi wa hivyo.
 
Raisi Samia alishaambiwa Chalamila, Hapi, Sabaya hawafai kurudishwa, akajifanya hasikii amevaa earphones aanasikiliza taarabu za kumsifia. Mwache ajifunze the hard way.
 
Kabla ya hayo huwa wanajulishwa kwanza, sema tu jamaa sikio la kufa
 
Back
Top Bottom