Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Huyo Chalamila hana usafi wowote wa moyo kama unavyotaka kuwaaminisha watu.Mimi naamini kabisa ndani ya moyo wako wewe ni mtu mzuri. Una sense of humor ambayo bahati mbaya wengine hawaielewi.
Naamini kilichokukuta safari hii ni watu wamekupiga fitna hasa wale Waliochukua clip ya sauti yako na kuikatakata kisha kuunganisha vipande.
Naamini kabisa kwenye ile clip hukumaanisha kuwa watu wabebe mabango ya kumtukana rais, bali ulitaka kuonyesha kuwa hutozuia bango la mtu yeyote hata kama anawatukana nyie watendaji wa mkoa.
Nikikulinganisha na mtu kama Sabaya au Makonda wewe ni Saint kabisa huna roho ya kikatili na kishenzi.
Sasa kutokana na hilo, Omba miadi na mheshimiwa rais, Chukua video nzima za press conference yako na waandishi wa habari, mueleze mheshimiwa rais kuwa waandishi wameikata hiyo taarifa na "kukutake out of context" kwa sababu za kiuchonganishi.
Pia muombe radhi mheshimiwa rais kwa kumkwaza, maana teua tengua nayo ni kazi, lakini pia inaweza kumpa picha mbaya mbeke ya umma kuwa hayuko makini kwenye teua zake.
Ndugu Chalamila, wewe ni kiongozi mzuri sana, ila sasa utani ulikuwa mwingi lakini naamini kabisa kwenye hii ishu umekuwa "framed".
Tafuta namna ya kukutana na mheshimiwa rais umuelezee kirefu issue yako.
Lengo siyo uteuliwe, bali lengo liwe ni kuweka rekodi sawa!
Usiitishe press conference hivi karibuni kujisafisha, wewe tulia ila jisafishe kwanza mbele ya mamlaka
Hivi unajua kuwa ile hukumu ya uonevu iliyomweka Sugu jela bila kosa, iliandaliwa na hakimu wakishirikiana na RC ofisini kwake? Unafahamu kuwa mahakama baada ya kukata rufaa, ilikubaliana na Sugu kuwa alionewa?
Tusiowaonee huruma watu wenye roho mbaya. Wananchi tusimame pamoja kupigania uongozi mzuri bila ya kujali itikadi za kisiasa maana sote tuna haki sawa, na hakuna aliye Mtanzania zaidi kumzidi mwingine.