Chalamila omba wasaa ukutane na Mheshimiwa Rais uombe umueleze upande wako wa stori

Huyo Chalamila hana usafi wowote wa moyo kama unavyotaka kuwaaminisha watu.

Hivi unajua kuwa ile hukumu ya uonevu iliyomweka Sugu jela bila kosa, iliandaliwa na hakimu wakishirikiana na RC ofisini kwake? Unafahamu kuwa mahakama baada ya kukata rufaa, ilikubaliana na Sugu kuwa alionewa?

Tusiowaonee huruma watu wenye roho mbaya. Wananchi tusimame pamoja kupigania uongozi mzuri bila ya kujali itikadi za kisiasa maana sote tuna haki sawa, na hakuna aliye Mtanzania zaidi kumzidi mwingine.
 
Kama alisema hivyo, basi huyo ni bure kabisa.q
 
Icheki YouTube akipokea vifaa vya hospital aliongea ujinga sana.

Watu wengi wanaongelea ishu ya mabango sijui Ila hii hawaiongelei kabisa
Hiyo kauli then was the worst.

Hivi ni nani alimwambia watu wa Mwanza wanasema Magufuli aliuawa na mtu yeyote? Ni wajinga wachache sana huko twitter ndio wamekuwa wakiropoka hayo maneno. Labda huyo Chalamila ni miongoni kwa waliokuwa wakiandika kuwa Magufuli kauawa.

Mimi nipo Mwanza, sijawahi kumsikia mtu yeyote mtaani akisema Magufuli aliuawa. Hayo ya kuuawa yamekuwa yakizushwa mitandaoni na watu ambao uwezekano mkubwa hawaishi Mwanza.

Kwa kauli hiyo Chalamila alistahili kufukuzwa mara moja na kukamatwa na kuhojiwa ili aeleze ni nani ambaye amekuwa akieleza kuwa Magufuli aliuawa.
 
Chalamila anatatizo la kutopanga maneno,pia Hajui mipaka yake kiogozi na pia Hajui muktadha.
Mfano;
1: Kipindi Marehemu JPM unaumwa alisema kuwa yeye kaongea nae ni Mzima wa afya na kasaini mikataba huku akijua yeye siyo msemaji wa serikali kwa Jambo lile
2:kuweka masuala ya mapenzi kwenye duara ya rais
3:Si muufaka kuongelea masuala ya kifo cha JPM kwenye ziara ya rais
 
Nadhani lazima amewekwa kikaangoni amekosea sana.
 
Kama kaondolewa kwa kauli hiyo, matokeo yatakuwa hasi kwenye ziara. Moshi umefuka tusitie kuni moto ukawaka au mafuta kukalipuka
 
Raisi Samia alishaambiwa Chalamila, Hapi, Sabaya hawafai kurudishwa, akajifanya hasikii amevaa earphones aanasikiliza taarabu za kumsifia. Mwache ajifunze the hard way.
Ajifunze the hard way, my foot! Kwani Rais anapoteza nini au anaathirika vipi? Afterall Hiring and firing is her prerogative! Nyau we!

Sent from my itel A32F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo ile clip ya mabango ya matusi ilihaririwa ili ionekane alikuwa anasema watu waje hata na mabango ya matusi?
Ofcourse ile clip wameedit ili kuondoa context nzima ambayo Chalamila alimaanisha, Actually it seems the guy alikuwa akimaanisha kuwa ili kutekeleza agizo la raisi la kuacha watu wawe huru kubeba mabango, yuko ready kutolerate mabango hayo hata kama yanawatukana wao akina Chalamila wenyewe mbele ya rais.

Wahuni wakakata clip ile wakaiunganisha na sentensi ya nyuma ikaonekana kuwa anaruhusu watu wabebe mabango ya kumtukana rais kitu ambacho siyo kweli
 
Duh!

Kama unachosema ni kweli basi Samia naye ana matatizo [endapo kama hiyo ndiyo sababu iliyomfanya atengue uteuzi wake].

Anakuwa influenced kirahisi mno na mambo ya mtandaoni.
 
Duh!

Kama unachosema ni kweli basi Samia naye ana matatizo [endapo kama hiyo ndiyo sababu iliyomfanya atengue uteuzi wake].

Anakuwa influenced kirahisi mno na mambo ya mtandaoni.
Unless otherwise kama kuna sababu nyingine ya utenguzi wake, lakini kama ni hii basi mamlaka za uteuzi zimechemsha!
 
Hizi tengua teua mama zitamwangisha kichwa, sasa kuna haja ya ku deal na mfumo mzima wa chimbuko la mtu husika kabla ya kumteu historia ya familia ama ukoo wake ujulikane, wengine koo zao ni za kiwindaji na wacheza ngoma hivyo familia ama ukoo wa namna hii ukiupa namna yeyote ya uongozi lazima ni pasua kichwa.
 
Naendelea kusema sisi watu wa IT ni watu wabaya sana
Yeyote aliyesomea mambo ya information & communication technology ukae naye mbali...
hamna kitU cha ajabu hapo yeyote naweza edit kwenye simu ukafanya hivyo
 
Aisee nimeiangalia tena hiyo clip.

Kuna uwezekano mkubwa sana kuwa imeungwa ungwa ionekane kama kweli kasema watu waje na hata mabango ya matusi.

Mwanzoni anaongea akiwa peke yake.

Baadaye pale anapozungumzia mabango yenye matusi, kuna mtu mwingine kakaa pembeni yake.

Yawezekana kweli kuna mchezo mchafu hapo.

<blockquote class="twitter-tweet"><p lang="in" dir="ltr">Albert Chalamila kabla hajatenguliwa Mwanza.<a href="https://twitter.com/hashtag/KitengeUpdates?src=hash&amp;ref_src=twsrc^tfw">#KitengeUpdates</a> <a href="https://t.co/Yrfqtpyoly">pic.twitter.com/Yrfqtpyoly</a></p>&mdash; Maulid Kitenge (Mshambuliaji) <a href=" ">June 11, 2021</a></blockquote> <script async src="https://platform.twitter.com/widgets.js" charset="utf-8"></script>
 
Kijana ni mapepe hajatulia kichwani. Aliropoka, wale waliokuwa pembeni wakabaki wamepigwa butwaa hawaamini wanachosikia.
 
Umeona eh!, Wamehariri!

Wamepandishia clip juu ya clip nyingine!

Huu mchezo siyo mzuri kabisa

Ni matumizi mabaya ya ICT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…