Chalamila omba wasaa ukutane na Mheshimiwa Rais uombe umueleze upande wako wa stori

Raisi Samia alishaambiwa Chalamila, Hapi, Sabaya hawafai kurudishwa, akajifanya hasikii amevaa earphones aanasikiliza taarabu za kumsifia. Mwache ajifunze the hard way.
The only way.
 
Yaani wewe unamchukia Chalamila kisa sugu tu..???!!

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Huwa hakuna mtawala asiyependa wateule wanamfagilia.
Magufuli akifanya uchawa sana wakati wa utawala wa BWM na JK na waliweza kumvumilia ufisadi wake na madudu yake na hii ni kwa sababu alikuwa pia aiwasurprise kwa bidii ya kazi

Hatukatai kufanya uchawa wa akili ambao ndio Jiwe alifanya hasa kwa BWM kwa kujituma sana kwenye majukumu yake; sasa hawa wakina Mwigulu wanakuja na bajeti mbovu mbovu za kusamehe kodi wacheza kamari na kuwatoza kodi masikini kwa kuongeza bei za vocha za Simu!!! Mbona wenzetu Zanzibar wameifurahia bajeti yao kwa kutoa unafuu wa kodi?

Kwanini msije na pendekezo la kupunguza mishahara na malupulupu ya Viongozi wakiwemo Wabunge kama njia ya kupunguza matumizi ya serikali? Mishahara yao iwe na uwiano na mishahara mingine nchini na pia hali ya uchumi wa nchi!
 
Acha kumpotezea muda. Mshauri arudi Iringa aanze kuangalia jimbo lenye mbunge legelege aanze kujiimarisha ili 2025 aingie mjengoni na kugombea uspika. Mufindi ya Malangali au Kalenga kutamfaa. Hata Ismani Lukuvi ameshachokwa amezidi mno majivuno na dharau.

Sent from my TECNO P701 using JamiiForums mobile app
 

Ushauri wako ni mzuri, aende Iringa ajipange kuchukua jimbo la ISMANI kwani Lukuvi hana mvuto tena. Na yeye ana advantage ya kuwa alikuwa Mwenyekiti wa ccm mkoa!!!
 
Mizaha na masikhara vimemponza
Ile ni "saa mbovu" au mpaka angechojoa ndipo watu wangelijua ni "fyatu?" Hakuna utani kwenye kauli "kuua atakayehisiwa..., kelele ni chakula cha pombe!!!" Tufanye tu kwamba na "mamlaka yamemtania..."
 
Mkuu sio lazima awe mkuu wa mkoa ndo aishi.maisha inabidi yaendelee sometimes vyeo Kama hivi sijui hata watu wanavitaka vya Nini unaishi unamuogopa mtu kuliko mungu
Fisiemu wengi wanaamini katika maisha ya kisiasa ndio maana husikii wanaovurunda kujiuzulu "mpaka wafukuzane" ndo zinawakaa sawa!!!
 
Time out mzee wa kuripuka kiberiti na mafuta ya petrol. Chalamila jiandae kupanda basi la Mwanza to Dodoma, then lala dodoma kwani utakuwa umechoka sana kwani ulishasahau usafiri wa public, kesho yake amka mapema panda gari za Dodoma to Iringa utamkuta Rev. Msigwa stendi anakusubiri akupe lift kwenye V8 lake la maroon hadi kwako. Then ujiandae kuwa mbeba mafaili ya DC wa Iringa yule aliyewatukana bodanboda ila akastuka na kuomba radhi hapo hapo sasa kabadilika kweli hadi anapita mtaani na baiskeli.
 
Ni aibu kuwa na nutcase kama Chalamila kwenye utumishi mkubwa kabisa wa umma.
Uchapakazi wake akalimie vitunguu Iringa, ofisi ya umma inahitaji watu serious na sio comedians.
Nipe rekodi ya thread yangu au post yoyote niliyotaka Chalamia aondolewe Ukuu wa mkoa!, Haipo

Mimi nimekuwa nikimkubali huyu jamaa siku nyingi tu maana nimchapakazi hodari
 
Chalamila ni mjomba wako??
Aliwasulubu sana makamanda Mbeya lakini bado una mahaba naye yaliyopitiliza!
Infact pale alikuwa anamzungumzia rais in a very positive way.

Alichagua maneno yenye Ukakasi kidogo lakini The overall message ilikuwani kuwataka watu wamuelewe, wampe ushirikiano mheshimiwa rais katika kuleta maendeleo katika mkoa wao.
 
Wewe ni msemaji wa chalamila? Watanzania wengine bwana hovyo Sana.
Tatizo baadhi ya watanzania wenzetu wanafikiri mtu akiwa kiongozi au mtu mkubwa kiumri hakosei. Chalamila hafai hata kuwa katibu kata, lilikuwa ni swala la muda tu.
 

Hivi wabongo tuna nini? Kwani alipoteuliwa aliitwa pembeni kuombwa ushauri? Kazi imekwisha..it is that simple. Akajipange upya atafute namna nyingine ya kuendesha maisha. Hii nafasi ya kuteuliwa siyo permanent. Yaani it's like hii nafasi ilikuwa ya kwake..nah...waTz wengi wakipewa nafasi wanaweza kuifanya hii kazi. Hii ni kazi ya upendeleo haina taaluma. Ndo maana ukitenguliwa huna pa kulalamika. Unahudumu kwa matakwa ya mteuaji.

Kama hakulijua hilo is a compound fool!
 
kwa hiyo unataka kusema zimeungwa speech mbili tofauti na venue tofauti?
 
Umeona eh!, Wamehariri!

Wamepandishia clip juu ya clip nyingine!

Huu mchezo siyo mzuri kabisa

Ni matumizi mabaya ya ICT
Kwahiyo nyie mnadhani wenye Nchi hawakuwepo hapo wakati anaongea?!?
Anyway tukirudi kwenye mada.. Sio rahisi kupewa audience na Rais eti ujieleze kwa kosa ambalo umetumbuliwa nalo.. Maana hiyo audience yenyewe inaamuliwa na watu wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…