Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema hana taarifa za maandamano ya Chadema yaliyotangazwa kufanyika Januari 24, mwaka huu akisema anachojua siku hiyo ni ya kufanya usafi.
Akizungumza leo Jumatatu Januari 15, 2024 katika mkutano wake na watendaji wa Serikali kuhusu tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko, Chalamila amesema watu wanahusisha shughuli ya usafiri aliyoitangaza na maandamano ya Chadema ambayo yeye anadai hana taarifa nayo.
Hata hivyo, amesema wakati baadhi ya watu wakihusisha tukio hilo la kufanya usafi na maadamano ya Chadema, yeye hana taarifa hizo kwa kuwa anayepaswa kuzitoa ni Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro.
"Mimi sina taarifa za maandamano na pia shughuli za watu wengine haziwezi kusimamisha shughuli za Serikali, ninachojua siku hizo ni kampeni kabambe ya kufanya usafi," amesema Chalamila.
Aidha, kuelekea Janauri 23 na 24 mwaka huu ambayo ilitangazwa kuwa siku ya usafi utakaohusisha vyombo vya ulizi, Chalamila, amewaonya wananchi wabishi kutoa fedha kwa ajili ya kuzoa taka.
Amesema siku hiyo ni ya usafi kabambe, lakini ana taarifa za baadhi ya wananchi kugomea kutoa tozo ya taka, hivyo kuwaonya kuwa siku hiyo ya usafi watachukuliwa hatua.
Kadhalika Chalamila amesema kuna haja ya kutengenezwa sheria ndogondogo za kusimamia utekelezaji wa utoaji fedha ya kuzoa taka ili atakayekaidi achukuliwe hatua mara moja.
"Kuzolewa taka sio jambo la hiari bali ni la lazima kwa kuwa umezizalisha mwenyewe na zisipotolewa zitaleta magonjwa," amesema Chalamila.
Katika hatua nyingine, ameomba wadau mbalimbali kujitokeza kutoa vifaa vya kufanya usafi siku hiyo ya Januari 23 na 24 huku akitangaza kila wiki usafi utakuwa ukifanyika.
Amesema Januari 20 anategemea kuanza kugawa vifaa vya usafi katika vyombo vya dola.
Mwananchi
Pia soma:

- Mbona CHADEMA mnalalamikia zoezi la usafi wakati RC Chalamila hajalaumu maandamano yenu?
- CHADEMA msitishwe na RC Chalamila
- Albert Chalamila: Usafi wa Wanajeshi hautoathiri maandamano ya CHADEMA
- Sina hakika kama RC Chalamila anaweza kuligusa kundi hili katika Maandamano ya CHADEMA
- Tetesi: - Chalamila adaiwa kuhusika na ufutaji wa kipindi Wasafi FM
- Kauli za mkuu wa mkoa Chalamila kuhusu siku ya usafi Januari 24
- Umoja wa Vyama vya Siasa: Hatukubaliani na Maandamano ya CHADEMA, walijitenga nasi, sasa hivi wanatushirikisha
- Umoja wa Vyama vya Siasa: Hatukubaliani na Maandamano ya CHADEMA, walijitenga nasi, sasa hivi wanatushirikisha
- Abdul Mluya: Sisi tulishapigwa, kama CHADEMA wanataka maandamano wajipange na familia zao mbele wapate ladha yake
- Ni aibu kubwa sana kwa CHADEMA kufanya maandalizi ya maandamano Arusha wakati wananchi na mkoa upo kwenye majonzi na simanzi ya kupoteza wapendwa wao
- Hivi vile vyama 13 vya upinzani, vilivyoamua kuungana na CCM, kuwapinga Chadema, wanajisikiaje hivi sasa baada ya kuona maandamano hayo yamefanikiwa?
- Kitatokea nini endapo Vyama Vingine vya Upinzani vitajiunga na maandamano ya CHADEMA?
- Je, CHADEMA wataahirisha maandamano kufuatia kifo cha Edward Lowassa?
- Dkt. Slaa athibitisha kushiriki maandamano ya CHADEMA jijini Mwanza
- RC wa MBEYA atuhumiwa kuhujumu maandamano ya CHADEMA Mbeya
- Mwanza: Wananchi Wakesha kwenye ofisi za CHADEMA ili kuwahi Maandamano
- CHADEMA yaahirisha Maandamano ya Karatu kwa sababu ya Mafuriko
- Polisi watia fora maandamano CHADEMA: Polisi wanaanza kuelewa kuwa upinzani siyo uadui!
- Chadema: Sasa Maandamano yatakuwa Utamaduni wetu wa maisha
- Wenje na Chief wanaongelea makubaliano chadema na polisi juu ya maandamano yao
- Nitashiriki kuzuia maandamano ya CHADEMA Januari 24, 2024
- CHADEMA Diaspora kufanya Maandamano makubwa Ulaya na Marekani muda wowote kuanzia sasa
- Joti anayapinga maandamano ya CHADEMA?
- Maandamano ya Chadema yaanza kuiunguza CCM, Viongozi wake waweweseka
- Kwanini CHADEMA watashindwa mapema kuelekea 2025 hata baada ya maandamano?
- CHADEMA kuwa chama cha Maandamano!
- Maandamano CHADEMA yasogezwa mbele
- Polisi kuyapiga marufuku maandamano ya chadema!!
- EFM wakejeli maandamano ya CHADEMA
- Maandamano ya CHADEMA ni jogging hayana impact kwa mtawala
- Maandamano ya CHADEMA yamekosa umuhimu, mvuto na ushawishi
- CHADEMA tafakarini kama maandamano ya Februari 15 ni sahihi
- Hivi waratibu wa maandamano ni CCM au CHADEMA, mbona CCM wanayaongelea sana?