Chalamila: Uwekwe utaratibu wa kuweka Tozo kwa magari yanayoingia Katikati ya Jiji

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akizungumza alipotembelea Makao Makuu ya TFF, Ilala, Karume

"Tumeruhusu kila aina ya usafiri kuingia barabarani. Nafikiri mliwahi kunisikia wakati fulani nikasema... nilitania tu, lakini nilikuwa namaanisha. Ni ule utani wa kweli kweli. Nilikuwa nasema ukiruhusu kakorola kana namba A, namba A isitafsiriwe kwa tafsiri sisisi. Yaani, usifanye interpretation kwa direct translation.

Nilisema kwamba unaporuhusu kila kakitu kuingia kwenye barabara kuu, unasababisha foleni beyond necessity. Sasa wewe ukipita Morogoro Road, au ukipita barabara hizi za Mandela, utakuta kuna lori, utakuta kuna bajaji, kuna pikipiki, kuna guta, kuna baiskeli—baiskeli za madafu. Kuna mbuzi anavuka, kuna sijui kitu gani kinavuka.

Mimi ukinisikiliza with these jokes, unaweza ukadhani huyu bwana Chalamila hana akili huyu. Lakini nilianza ku-present ili kufanya preparedness. Kwa sababu sasa hivi nasukuma ajenda, sasa ya kuhakikisha tunazuia baadhi ya vyombo vya usafiri kutokuingia kwenye barabara kuu.

Lakini jambo la nne, Dar es Salaam ni maeneo ambayo vyombo vya usafiri vyote vinaingia for free katikati ya jiji. Ukienda nchi yoyote ile iliyoendelea duniani kote, parking yenyewe hata ukifika pale London, huruhusiwi kuipaki kwa muda wa zaidi ya saa moja; uwe umeshaondoa gari lako. Sisi kwetu, ukutoka Kibaha mtu anaingia, anapaki popote, anaweza akaacha gari hapo akaenda mpaka Dodoma hajatowa taarifa, gari ameliacha pale pale, halafu akarudi.

Kwahiyo nini maana yake? Ni kwamba lazima ili tuweze kupunguza vyombo hivyo, tuanze utaratibu wa kama uliopo kwenye mataifa mengine; kuweka fee unapoingia ndani ya jiji ili ilete discipline, kwamba usiingie jiji kushangaa, uingie kwenye uingizaji wa fedha."​

Watu wa Tarura wamegeuka traffic wanasimamisha magari mjini kukagua madeni ya parking huo usumbufu mnaoutupa hamuuoni? Unaenda mbele unakuta traffic nao wana ukaguzi wao madeni huo usumbufu nao bado hamuuoni? Unafika mbele unakuta magari yamesimamishwa kuna kiongozi anapita huo usumbufu nao hamuuoni? Unarudi fire unakuta askari wanaruhusu upande mmoja nusu saa ama kwa utashi wao huo usumbufu nao hamuuoni? Mnakimbilia kuweka tozo. Kiasi gani hicho ambacho unahisi mwenye gari lake analipenda atashindwa kulipa kuingia mjini? Mmeruhusu vituo vya boda bajaji, watu wanapanga bidhaa barabarani, nenda soko la Ilala barabara nzima imejaa bidhaa magari yanapita kwa taabu tena ni karibu na ofisi ya mkuu wa mkoa kama sio wa wilaya. Halafu mnawaza Tozo. Hivi mnajua wenye magari wanapitia adha kiasi gani kufika mjini? Yaani kabla hata hamjaweka tozo kuna baadhi ya waemamua kuyaacha magari nyumbani sababu hakuna amani wala uhuru wa kuendesha magari Dar es Salaam ni KERO.
 
Piga marufuku bajaji na bodaboda mjini,ziishie mapipa,amana,Banda la ngozi,veta,mivinjeni,salenda
Alafu uchaguzi ukikaribia
Vyama vyenu mnaanza
Kuwatumia,viongozi wenu
Mnawaita na kuwatia moyo
Na kuwaunga mkono! 😄

Mambo ya bodaboda,bajaji wenyewe walikosea tokea zamani,waliziruhusu bila kuangalia mbeleni kutakuwa na impact gani
Miaka ya nyumaa bajaji zilikuwa zinatumiwa na vilema tu na wao ndiyo walikuwa na ruhusa ya kuingia nazo mjini
Huyo mkuu wa mkoa asifikiri foleni husababishwa na magari tu,wakati mjini sehemu nyingi miundombinu ni mibovu
Barabara nyingi ziko kwenye ujenzi na zimesimama
Anaposema magari ni mengi awambie serikali ipige marufuku pia uingizaji wa magari

Ova
 
Waweke tozo pia kwa wanawake vibonge weusi kuingia mjini khaa

Wanabuni tu vyanzo vya mapato pasina kuangalia maisha halisi ya mtanzania
Amekwepa kusema tatizo la ukweli linalo sababisha foleni

Ova
 
Kwakweli huko Kariakoo kumekuwa ni vurugu mechi!
Ukitaka kukatiza barabara kwenda upande wa pili kwanza usimame Usali sala zote na ukumbuke kama ulishaweka mambo ya urithi sawasawa ndipo uvuke!
Na haieleweki uvuke taratibu au mbio mbio kama bodaboda wanavyokwenda mbio kwenye barabara ya mwendokasi utadhani wanasafiri kwenda Mtwara.
Mara paap unastukia umewekwa katikati kama sandwich 🥪 hujui ufanyeje na hawapunguzi mwendo !

Wanaovuka barabara wapo pia wazee wagonjwa na walemavu wa aina mbali mbali lakini hao mavijana wanaoendesha hizo pikipiki hawana habari kabisa na hiyo kitu ,
 
Sometimes inabidi ukiwa hapo katikati usimame kiubavu ubavu ili usikwanguliwe maana ukijiachia Kuna kugongwa mbele na nyuma 😅😅
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akizungumza alipotembelea Makao Makuu ya TFF, Ilala, Karume

"Tumeruhusu kila aina ya usafiri kuingia barabarani. Nafikiri mliwahi kunisikia wakati fulani nikasema... nilitania tu, lakini nilikuwa namaanisha. Ni ule utani wa kweli kweli. Nilikuwa nasema ukiruhusu kakorola kana namba A, namba A isitafsiriwe kwa tafsiri sisisi. Yaani, usifanye interpretation kwa direct translation.

Nilisema kwamba unaporuhusu kila kakitu kuingia kwenye barabara kuu, unasababisha foleni beyond necessity. Sasa wewe ukipita Morogoro Road, au ukipita barabara hizi za Mandela, utakuta kuna lori, utakuta kuna bajaji, kuna pikipiki, kuna guta, kuna baiskeli—baiskeli za madafu. Kuna mbuzi anavuka, kuna sijui kitu gani kinavuka.

Mimi ukinisikiliza with these jokes, unaweza ukadhani huyu bwana Chalamila hana akili huyu. Lakini nilianza ku-present ili kufanya preparedness. Kwa sababu sasa hivi nasukuma ajenda, sasa ya kuhakikisha tunazuia baadhi ya vyombo vya usafiri kutokuingia kwenye barabara kuu.

Lakini jambo la nne, Dar es Salaam ni maeneo ambayo vyombo vya usafiri vyote vinaingia for free katikati ya jiji. Ukienda nchi yoyote ile iliyoendelea duniani kote, parking yenyewe hata ukifika pale London, huruhusiwi kuipaki kwa muda wa zaidi ya saa moja; uwe umeshaondoa gari lako. Sisi kwetu, ukutoka Kibaha mtu anaingia, anapaki popote, anaweza akaacha gari hapo akaenda mpaka Dodoma hajatowa taarifa, gari ameliacha pale pale, halafu akarudi.

Kwahiyo nini maana yake? Ni kwamba lazima ili tuweze kupunguza vyombo hivyo, tuanze utaratibu wa kama uliopo kwenye mataifa mengine; kuweka fee unapoingia ndani ya jiji ili ilete discipline, kwamba usiingie jiji kushangaa, uingie kwenye uingizaji wa fedha."​

Iwekwe iwe kubwa kabisa Ili tujue hasara ya kuongozwa na viongozi aina hiyo
 
Viongozi wa ccm bwana, badala ya kujenga miundombinu mizuri kuingia katikati ya jiji ninyi mnafikiria kuwazuia watu wasiingie katikati ya jiji?! Wazo jingine; panueni jiji sio lazima kila kitu kilundikwe Posta na Kariakoo tu.
 
Ni kweli tozo iwekwe tena kubwa hasa malori mpaka bajaji na bodaboda
Lori likiharibika njiani litozwe faini
 
Back
Top Bottom