Chalamila: Wananchi wa Dar kufanyiwa vipimo vya afya bure kuanzia Julai 3 hadi Julai 8, 2026

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Albert Chalamila, leo Julai 2, 2026, amezungumza na waandishi wa habari na kutangaza kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imeandaa kampeni maalum ya upimaji wa afya na utoaji wa matibabu bure kwa wananchi kwa muda wa siku sita.

Akitoa taarifa hiyo, Chalamila amesema kampeni hiyo itaanza Julai 3 hadi Julai 8, 2026, ikiwa na lengo la kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi pamoja na kuwawezesha kupata uchunguzi wa mapema na matibabu bila gharama.

Ameeleza kuwa kuanzia Julai 3 hadi Julai 5, huduma hizo zitatolewa katika Shule ya Msingi Chamazi, iliyopo Wilaya ya Temeke. Baadaye, kuanzia Julai 6 hadi Julai 8, kampeni hiyo itaendelea katika Viwanja vya Tanganyika Pekas Kawe, Wilaya ya Kinondoni.

Hakuna Cha Bure Dar..maana itabidi kusimamisha Shughuli zako za kiuchumi kwa hizo siku kwa ajili ya foleni njiani/Barabarani na foleni kwenye huduma,na wengi hawatahudumiwa mpaka siku zitawaishia wakiwa kwenye foleni.
CCM ni hatari mno..kwanini wasitoe huduma nyumba kwa nyumba??Mbona kwenye chaguzi hupita nyumba kwa nyumba kuomba kura na kuhonga sukari na vipande vya sabuni.???
 
Albert Chalamila, leo Julai 2, 2026, amezungumza na waandishi wa habari na kutangaza kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imeandaa kampeni maalum ya upimaji wa afya na utoaji wa matibabu bure kwa wananchi kwa muda wa siku sita.

Akitoa taarifa hiyo, Chalamila amesema kampeni hiyo itaanza Julai 3 hadi Julai 8, 2026, ikiwa na lengo la kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi pamoja na kuwawezesha kupata uchunguzi wa mapema na matibabu bila gharama.

Ameeleza kuwa kuanzia Julai 3 hadi Julai 5, huduma hizo zitatolewa katika Shule ya Msingi Chamazi, iliyopo Wilaya ya Temeke. Baadaye, kuanzia Julai 6 hadi Julai 8, kampeni hiyo itaendelea katika Viwanja vya Tanganyika Pekas Kawe, Wilaya ya Kinondoni.

Siyo Tanganyika pekas, Packers
 
Whatever that is offered for free is very very expensive.
 
Hope atakuwa wa kwanza kufanya vipimo ili wengine tuige ,ingependeza zaidi kama majibu yake hasa kwa upande wa akili akatushirikisha wananchi wake ili tujue aina ya kiongozi anayetuongoza
 
Back
Top Bottom