Chalamila: Wanasema ni Kodi zetu, tukirudisha naamini hamtopata chochote

Chalamila: Wanasema ni Kodi zetu, tukirudisha naamini hamtopata chochote

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila leo tarehe 22 Septemba, 2025 amekabidhi magari mawili aina ya Toyota Land Cruiser Prado yenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni mia mbili hamsini na mbili kila moja (Tsh. 252,000,000) kwa wakuu wa wilaya za Ubungo na Kigamboni.​

Aidha Chalamila amekosoa tabia ya baadhi ya watu kupinga pale ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anapopongezwa kwa kufanya maendeleo huku wakidai kuwa maendeleo hayo yanatokana na kodi zinazotolewa na wananchi. Chalamila ameongeza kuwa pamoja na kodi zinazokusanya Rais Samia amekuwa akifanya jitihada binafsi kukusanya na kutafuta fedha kutoka vyanzo vingine kwaajili ya maendeleo ya nchi.
 
FB_IMG_1758545069266.jpg
 
Kumbe huwa mnakereka watu wakisema ni kodi zao!😁
 
Sasa kwani wanatoa mifukoni mwao.
Pia hizo ndizo job descriptions mmeajiliwa inabidi muwatumikie waliowaajiri na sio kuiba, wizi haitakiwi na mtachomwa moto, kumbuka muda si muda mnakuwa mavumbi mnaliwa na mafunza mnaoza huko mnakoenda mnakujua
 
Back
Top Bottom