Chalamila: Wanaume acheni unyanyasaji kwa wanawake

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema mwanamke ni mbegu, tunu, chachu, faraja, dira, mbunifu na shujaa katika familia na katika kuongoza taifa kwa ujumla endapo akipewa nafasi ya kuonyesha ujuzi wake.

Aidha, Chalamila amegusia suala la wanaume kuwaachisha wanawake kazi, jambo linalopelekea wanawake kuwa masikini. Amewasihi wanaume kuachana na tabia hiyo na badala yake wawajenge wanawake.

Pia, amewaambia wanawake kuwa yote yanawezekana endapo watakuwa na mshikamano na kuwa jeshi moja, akiwataka kutojiuliza "hivi nitaweza?"

Fauka na hayo, amewaambia wanaume waondoe ushamba wa unyanyasaji kwa wanawake kwa dhana potofu kwamba mwanamke akifanikiwa mwanaume amepoteza.

Hivyo, amewataka wanawake kuwa na mitazamo chanya kwao wenyewe na kwa waume zao, akiwashauri kujivunia kuwa wanawake kwani wakijithamini hakuna mwanaume atakayewadharau.

Chalamila pia amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, ikiongozwa na Dorothy Gwajima, akisema kuwa mwanamke ni jeshi kubwa.

Albert Chalamila amesema hayo leo Machi 8, 2025, katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa Mkoa wa Dar es Salaam yanayofanyika katika viwyanja vya Leaders Club.
 
Hizo ndo kauli za zamani........sasa hivi wanaume ndo wananyanyaswa na wanawake.
 
Back
Top Bottom