DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemhakikishia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa hali ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka (Mwendokasi) ipo shwari licha ya tukio dogo lililojitokeza usiku wa kuamkia jana.
Amesema kuwa majira ya saa 12 jioni, kulijitokeza kikundi kidogo cha watu waliovamia na kufanya uharibifu katika baadhi ya vituo vya mabasi hayo, lakini hali hiyo imekwishadhibitiwa na mamlaka husika.
“Usafiri wa Mwendokasi upo shwari. Kikundi kidogo cha watu kilijaribu kufanya uharibifu jana usiku, lakini hatua zimechukuliwa na wale wasiokuwa na nia njema, watakipata hivi karibuni,” alisema Chalamila.
Kauli hiyo aliitoa wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kukagua hali ya usafirishaji katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Haraka kilichopo Kivukoni, Posta, jijini Dar es Salaam leo Oktoba 02, 2025.
Pia Soma: GE2025 - Chalamila: Mwendokasi umepoteza Ladha, mtu mwenye tai hawezi tena kupanda