Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemhakikishia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa hali ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka (Mwendokasi) ipo shwari licha ya tukio dogo lililojitokeza usiku wa kuamkia jana.
Amesema kuwa majira ya saa 12 jioni, kulijitokeza kikundi kidogo cha watu waliovamia na kufanya uharibifu katika baadhi ya vituo vya mabasi hayo, lakini hali hiyo imekwishadhibitiwa na mamlaka husika.
“Usafiri wa Mwendokasi upo shwari. Kikundi kidogo cha watu kilijaribu kufanya uharibifu jana usiku, lakini hatua zimechukuliwa na wale wasiokuwa na nia njema, watakipata hivi karibuni,” alisema Chalamila.
Kauli hiyo aliitoa wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kukagua hali ya usafirishaji katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Haraka kilichopo Kivukoni, Posta, jijini Dar es Salaam leo Oktoba 02, 2025.
Watafute mbinu mpya ya kuwatuliza Watanzania, hii ya kuwatisha Watanzania safari hii haitofanya kazi...
Njia bora kabisa ni kuhakikisha katiba mpya inapatikana na reforms zinafanyika..
Kuna vitu Chalamila havijui kuhusu Dar, na kwasababu sio mdadisi na badala yake muda wake wa mapunziko yuko kwenye beer hatakaa avijue. Yeye anahisi anaijua Dar kwasababu anajua Manzese.
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert Chalamila amemuahidi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa wale wote waliohusika na kushambulia mabasi yaendayo haraka(mwendokasi) pamoja na vituo vyake jana Oktoba 1, 2025 watachukuliwa hatua haraka sana.
Chalamila ametoa ahadi hiyo leo Oktoba 2, 2025 wakati Waziri Mkuu alipotembelea kituo cha mabasi hayo cha Kimara ili kujionea hali ya usafiri na usafirishaji.
"tunaamini wazo kubwa ilikuwa ni kukosekana kwa usafiri naomba nikuthibitishie Mheshimwa Waziri Mkuu wale wote ambao wamechukua hatua hiyo ya kufanya mambo hayo tutakula nao sahani moja" amesema Chalamila
Huyu ndio anazidi kuwamotivate raia October 29 wajitokeze kwa wingi kuwakomboa wenzao waliokamatwa wakipagania watoto wetu, wajawazito, wanafunzi wasafiri salama bila hofu ya kuumizwa.