Chalamila: Wasio na nia njema na mwendokasi watakipata 'Very Soon'

Huyo mkuu wenu mnashindwa nini kupiga hilo bichwa lake lililokaaa kama boga.

Vitisho akamtishie mke wake huko. Mpuuuzi sana
 
Mle nao na keki ya taifa kwa pamoja🐼
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert Chalamila amemuahidi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa wale wote waliohusika na kushambulia mabasi yaendayo haraka(mwendokasi) pamoja na vituo vyake jana Oktoba 1, 2025 watachukuliwa hatua haraka sana.

Chalamila ametoa ahadi hiyo Oktoba 02, 2025 wakati Waziri Mkuu alipotembelea kituo cha mabasi hayo cha Kimara ili kujionea hali ya usafiri na usafirishaji.

"tunaamini wazo kubwa ilikuwa ni kukosekana kwa usafiri naomba nikuthibitishie Mheshimwa Waziri Mkuu wale wote ambao wamechukua hatua hiyo ya kufanya mambo hayo tutakula nao sahani moja" amesema Chalamila Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam

Pia Soma: Mabasi mapya ya Mwendokasi ya MOFAT yaanza kubeba Abiria Gerezani–Mbezi
Your browser is not able to display this video.
 
Alafu moja ya kichochezi kikubwa cha maandamo kwa upande wa dachlamu ni huyu jamaa , kauli zake ziliwapendeza sana wanufaika na kuwakwaza sana wananchi kama kweli yalitimia huyu nae hana bahati
 
Kuna vitu Chalamila havijui kuhusu Dar, na kwasababu sio mdadisi na badala yake muda wake wa mapunziko yuko kwenye beer hatakaa avijue. Yeye anahisi anaijua Dar kwasababu anajua Manzese.
Ajabu ni kwamba jamaa ni born town kabisa wa hapa hapa darisalama...maana mimi alikuwa mwalimu wangu mkuu mwaka 2006 pale Tabata wazazi...kimanga...!

Ila tokea alivyo ibukia kwenye uongozi wa serikali nikaanza kumuona akiwa tofauti na ninavyo mfahamu...sijui huwa wanafanyagwa nini wakipewa madaraka..!​
 
Waanze na wasimamizi wa mradi. Kutoka magari zaidi ya mia moja na kitu hadi mabasi 30 ni zaidi ya ubujumu uchumi
 
Tunapiga mawe hadi reform zifanyike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…