Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Dogo hiyo elimu ya saving uliyoipata isikufanya ukawa kipofu, shukuru Mungu kwa kuwa neema imekufikia ila usilaumu kwa wale walioshindwa kulipa hiyo ada, hiyo hela ambayo unasema watu kwa siku au kwa mwezi wange-save ndio hiyo hela watu kwa siku ndio anaitumia kwa ajili ya chakula kwa siku.

Je hivi unajua kuwa kuna mtu kwa mwezi analipwa Tsh. 150,000 je ulishapiga mahesabu huyu mtu kwa siku anapata kiasi gani (Tsh.5,000). Je huyu mtu ataishi vipi kwa kiwango hiki anachopata ? Kuna nauli, kuna kodi ya chumba cha giza kuna chakula cha mchana, asubuhi na usiku nk.
 
Mkuu kwenye hiyo 150,000 mtu akiamua kusave 10,000 anabaki na 140,000. Tuseme kwa mwezi atumie 60,000 ya chakula yaani kila siku 2,000 anabaki na 80,000. Let's say kapanga nyumba ya 40,000 kwa mwezi anabaki na 40,000 ya nauli. Ukiona mtu anaingiza 150,000 kwa mwezi halafu kaanzisha familia au kampa mtu mimba ujue bado hajajitambua.
 
wengi wameajiriwa serikali, wana bima. wanauhakika wa miamala so hawawezi kujua ni kiasi gani watu mtaani wanataabika.
 
Huwa unaonekana Una akili kumbe ukipngea Una pumba kiasi hiki? Mikasi na gloves alizosema chalamila zinatumiwa na wajawazito au na madaktari? Yaani ni Sera ya Afya mgonjwa kumnunulia Daktari vifaa?
 
Unataka kusema huwezi kupata 50,000/= Kwa miezi 8? Bwashe mimba siyo chafya
Kwani hiyo elfu khamsini ndiyo utaratibu wa mjamzito kujifungua kwenye hospitali ya serikali?
Nadhani kama ingekuwa ni utaratibu wa kuchangia huduma za afya huyo mama asingepiga simu kwa mkuu wa mkoa kuuliza huo utaratibu.
Chalamila kakosa hekima na busara kwa hili.
 
 
Alikuwa na Bima?
Vifaa vya kujifungulia ni shi.ngapi?

Hoja hapo ni kuwa utaratibu wa malipo ulikuwaje, je walimpa control number au ni mkononi.
Kama hayo yote huyajui imekuwaje umuunge mkono Huyo mlevi mwenzio? Leo mama mjamzito wa kununua mikasi na gloves za madaktari?
 
wengi wameajiriwa serikali, wana bima. wanauhakika wa miamala so hawawezi kujua ni kiasi gani watu mtaani wanataabika.
Waajiriwe wapi, wanakaa kwa shemeji zao hata bei ya mkate hawaijui, wanakuta kila kitu mezani wanahisi familia zote zipo hivyo kumbe huyo shemeji na dada yao wanapambana kweli
 
Maajabu hayaishi duniani
Yeye mkuu wa mkoa anapata
Gari bure
Dereva bure
Afya bure
Umeme bure
Vocha bure
Airtime bure
Nk nk bure
Na bado anàlipwa miposho kibao bure.
Bila kusahau mshahara mkubwa tu nao ni bure.

Aliyeshiba hamjui mwenye njaa!
 
Unajua Masharti ya hiyo Bima ? Hivi mnadhani watu wanahangaika na NHIF kwanini ?
wewe unayejua ndio utuelezee

mimi kwa namna nnavyomuona
1.ana bima yeye,mke wake na watoto wake watatu

wawili kati ya hao mke wake alijifungua kwa operation 1.kahama hosp 2.muhimbili kwa hiyo bima

nje ya hapo magonjwa haya ya kwetu kawaida maralia,uti na hay mengine naona wanatumia hiyo bima..kijana wake alilazwa siku 4 temeke ikatumika hiyo bima

na anachangia between 30,000-60,000 kwa mwezi na ananieleza hela yake haikatwi(sina uhakika)

sasa kwa maisha yetu ya kitanzania si nafuu

uje na maelezo changamoto ya hiyo bima
ndio namna tunapeana uelewa mzee wangu
 
Huna cha maana unachokielewa hao
 
Huu uzi sijausoma, ila naungana na Chalamila. Mimba nyingi haziji bahati mbaya. Na hata zikija bahati mbaya, kitendo cha kuiacha ikue inamaana ni sahihi unahitaji mtoto.
Sasa kwa miezi yote tisa unasubiri kujifungua, huwezi ukaikusanya hiyo 50,000 wewe na mumeo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…