Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Chalamila yupo sahihi; kuna Bima ya elfu 40. Unajua Mkeo ni mjamzito, huna Pesa. Kata hata hiyo

Waajiriwe wapi, wanakaa kwa shemeji zao hata bei ya mkate hawaijui, wanakuta kila kitu mezani wanahisi familia zote zipo hivyo kumbe huyo shemeji na dada yao wanapambana kweli
🤓🤓
Acha hasira
Kwani ni kosa mtu kuwa na ndugu na kukaa na ndugu wenye vipato?
 
watu weusi ni bure kabisa, wao ni dezo tundio mfumo wa maisha yao
 
Kwema Wakuu!

Chalamila hapa nitamtaja kama Mhusika bila kuhusisha cheo chake. Ni aina ha watu ambao hawana breki za kuongea na watu wa aina hii mara nyingi huongeaga UKWELI mchungu ambao wakati mwingine huweza kuwaacha watu mdomo wazi.

Chalamila kadiri unavyompa nafasi na Muda WA kuongea ndivyo anavyoweza Kuropoka mambo ambayo ni magumu. Kwa Sisi tunaojua watu aina yake hatuwapagi nafasi Sana ya kuongea au kuwauliza maswali Tata ambayo yatamfanya ajichie.

Chalamila ni kama Kina Tundu Lisu. Tofauti Yao ni Moja. Mmoja anajua kujenga hoja wakati mwingine hawezi kujenga hoja ila wote wanaweza kuwa wanasema ukweli uleule wa Jambo lilelile.

Wasema ukweli mara nyingi hawanaga Staha. Hiyo huwafanya kuitwa roporopo.

Tukirudi kwenye hoja ya Chalamila kuhusu Wajawazito. Yupo sahihi Kabisa

Serikali sio kama imeweza Kabisa lakini angalau inajaribu kujitahidi Kusaidia watu hasa watu wa chini ingawaje zipo changamoto za kiutendaji na kifedha.

Kuna Bima ya CHF kama sijakosea ambayo kwa mwaka ni elfu 40,
Mambo inayotibu Bima hii ni Magonjwa ya kawaida yote.
Ujauzito
Ultrasound
X-ray
Kujifungua na Upasuaji mdogo
N.k.

Hivi mtu unajua Kabisa unaenda kuzaa mtoto au umembebesha Mimba Binti au Mkeo. Kwa nini usiweke angalau kwa siku elfu Moja Miatano kwa siku kisha mwisho wa mwezi wa Kwanza wa Ile Mimba ukate Bima ya elfu 40 kwaajili ya kumsaidia Mkeo au huyo uliyempa Mimba

Au kama umetelekezwa, sio sababu ya kukosa Bima ya elfu 40 kwa Sababusiku hizi Fursa za uzalishaji na kujipatia kipato ni Haki Sawa baina ya Mwanaume na mwanamke. Nikimaanisha huna haja ya kumtegemea Mumeo au mwanaume wakati Fursa zimetolewa Sawa.

Kata Bima ya elfu 40 kwaajili yako kama mwanamke mjamzito.

Na sio kulialia kumtafutia mtu Lawama kwa Jambo linalokuhusu mwenyewe ambalo umerahisishiwa.

Mambo ya huruma huruma, burebure ndio yanaharibu jamii.

Tunajua nchi yetu ni Maskini na jamii zetu nyingi ni Maskini ndio maana serikali kwa sehemu nayo imerahisisha kwa upande wao. Sasa mwaka mzima ushindwe Kutafuta elfu 40 ulipie Bima ati utake serikali ikuhudumie. Huo kama sio Ukengemaji ni nini?

Chukua Bima ya 40 Kisha andaa pesa ya kujifungulia ya dharura na ya uzazi
Hayo ndio majukumu yenyewe. Pumbavu.

Tupo kwa ajili ya wengi wenye kuhitaji msaada wanaoustahili

Tupo hapa

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
Tuna bima Tena kubwa na bado kuna matibabu tunaambiwa hayana bima ,hakuna jambo tanzania tumekuwa serious
 
Back
Top Bottom