GE2025 Chama cha AAFP yaahirisha mkutano wa kampeni kisa polisi kuingilia na kukuta gari iliyobandikwa picha ya Rais Samia

GE2025 Chama cha AAFP yaahirisha mkutano wa kampeni kisa polisi kuingilia na kukuta gari iliyobandikwa picha ya Rais Samia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Hiki ni kituko au ni bwebwe kuonyesha nao wanamsimamo mkali? Yani picha tu ndio uharishe mkutano, vipi gharama za kuandaa huo mkutano, vipi watu walifika?

Kwani kulikuwa na shida gani kuondoa gari hilo
===============
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Wakulima (AAFP), Kunje Ngombale Mwiru, amejikuta akiahirisha kampeni baada kukuta eneo la mkutano kuna gari limebandikwa picha ya mgombea wa CCM.

Tukio hilo lilitokea katikati stendi ya mabasi ya Kilwa Masoko mkoani Lindi jana, ikiwa ni muda tu wa kufika eneo hilo ili kuhutubia mkutano wa hadhara.

"Kwanza sakata lilianzia kwa polisi kudai kwamba hatutakuwi kufanya mkutano eneo hili, lakini pia kuwapo gari yenye picha ya mgombea wa CCM " amesema Ngombale.

Screenshot 2025-09-20 210601.png
 
Back
Top Bottom