Chama cha ACT Wazalendo wataka ripoti ya TAKUKURU iwekwe wazi

Chama cha ACT Wazalendo wataka ripoti ya TAKUKURU iwekwe wazi

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Waziri Kivuli wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora ACT Wazalendo, Shangwe Ayo, ametaka ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa Tanzania (TAKUKURU),ili iweze kujadiliwa kwa kina na wananchi

Shangwe ametoa kauli hiyo ikiwa imepita siku moja tokea taarifa ya TAKUKURU kuwasilishwa Kwa Rais na kusema Uwazi wa ripoti hiyo itawasaidia wananchi kujua jitihada za kupambana na rushwa nchini kama zinafanikiwa au nchi inarudi nyuma

Amesema haitoshi kuwa na taarifa nzuri,isiyoonyesha Uwazi wa watu waliochukuliwa hatua Kwa maksos yaliyoainishwa katika taarifa zilizopita.

SHANGWE.jpeg


"Tunafahamu kwa sasa ripoti ni mali ya Rais na baada ya kuwasilishwa kwake haitolewi Kwa umma kama inavyotolewa ripoti ya CAG, usiri huu hauna afya kwa mapambano ya rushwa"
amesema.

Shangwe ameongeza kuwa ni wakati wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya marekebisho madogo ya Sheria namba 11 ya Takukukuru ya mwaka 2007 ili kuweka takwa la lazima kisheria kuweka ripoti hiyo wazi.

Source: EATV
 
madam do you know what political science is, if you know then you are luck but if you don't know then wait the applicability of political science you will find that no body who is talking about CAG report
 
Back
Top Bottom