Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Hivi kuna namna tunaweza tukawa tunajiridhisha na hizi statistics zinazotolewa na hivi vyama vya siasa?
Yaani hapa tunapigwa mchana kweupe! Nani na akili zake timamu aache CCM, CHADEMA au ACT ahamie ADC?
=====================
Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kimepokea zaidi ya wanachama na viongozi 30 kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na chama cha ACT Wazarendo katika Mkoa wa Tabora.
Soma pia: Mwenyekiti NCCR Mageuzi Wilaya ya Misungwi abwaga manyanga na kuhamia ADC
Tukio la kuwapokea wanachama na viongozi hao limeongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Shaban Itutu ambapo mbali na kuwapongeza amewataka kujiandaa kikamilifu kuhakikisha wanafanya maandalizi ya kutosha lakini pia wanachukua fomu kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
"Leo imekuwa ni zamu ya ACT Wazalendo, Chadema na CCM nao wamehamia kwenye chama cha ADC kimsingi nawakaribisha sana, tutawapa ushirikiano mkubwa sana . Tunawaomba sasa kwa vile gari limewaka tupate wagombea udiwani majimbo yote lakini pia tumpate mtu ambaye atakwenda kumng'oa Hussein Bashe katika uchaguzi ujao," amesema Itutu
Aliyekuwa Mwenyekiti wa vijana CCM tawi la Mkoroshoni Kata ya Nzega Mashariki, Hamisi Makumbusho amesema ugumu na uwepo wa sera zisizobadilika zimemwondoa CCM na kujiunga na ADC.
"Kuna mambo mengi ambayo yameendelea katika chama chetu nimeendesha lakini kuna ugumU fulani ulikuwa unatokea mimi sera zao zilikuwa haziniridhishi kama kiongozi ninayeongoza vijana katika tawi hilo. Kutokana na sababu hizo nimekaa nikafikiria na kufanya tathmini namna ya kupata chama sahihi ambacho kitaleta mabadiliko katika nchi yetu kwa sababu sera zimekuwa hizohizo ambazo hazibadiliki," amessma Makumbusho
Kwa upande wake aliyekuwa Katibu wa Ngome ya Wanawake na Mratibu wa Jimbo la Nzega Chama cha ACT Wazalendo, Godliver Mayunga amesema uwepo wa mipango isiyotekelezeka ndani ya chama hicho imemfanya kuachana nacho na kuhamia chama kingine.
"Kilichonifanya niondoke ACT Wazalendo walikuwa hawatekelezi sera ambazo zipo ndani ya chama, wanamipango mingi isiyotekelezeka yaani ni watu ambao tunakutana kwenye matukio tu lakini hatuna mipango endelevu ndani ya chama sasa mimi kwa vile sipendi na nimekuja kuona hiki tunachofanya ni udanganyifu kwa wananchi na ndani ya chama nikaona nitoke niingie katika chama ambacho ni sahihi," amesema Godliver.